Tunamashaka na wanaojilipua kwa vazi la uislamu,huwenda wana ajenda zao

Kijana kijana

JF-Expert Member
Mar 11, 2018
2,546
2,616
Kumekuwa na sikitiko kubwa kwa baadhi ya vikundi vya kigaidi ambavyo vinajulikana kwa majina ya kiisilamu kuwa na vitendo vichafu ambavyo hata uisilamu unakataza.

Mfano jamaa wa alqaida wanaweza kuvaa bomu wakaingia katika kumbi za mikusanyiko wakajiachia na wakawa wanaitakidi wao ni peponi kwa wanawake wazuri ambao chuchu zimesimama unakobeka mpaka koti,macho mazuri na hawaendi hedhi n.k.hawa wanawake kwa mujibu wa imani yetu tunaamini wapo na ndyo mana hawa jamaa wakiambiwa hivi wanapata kuchachawa na kutaka kujiripua,ila je ni kweli katika uisilamu kujiripua kunakubalika?

Kiukweli ni jambo halikubaliki japo kuna baadhi ya watu wanasema hakuna waislamu wasokubali hayo matendo kwa kuwa wale ni wenzao,sababu ni kuwaa wale wanaofanya yale wanasura za kiislamuu hivyo mtu asiyekuwa muislamu vigumu kumuambia sisi hatukubi matendo yale...

Matendo kama yale hayakubaliwi katika uisilamu hata kidogo kwa sababu kwanza ni katika kuuwa nafsi yako mwenyewe na hilo jambo la kujiua halikubaliki kabisa kwa mujibu wa ayaa

[ AN-NISAAI - 29 ]
Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.

Aya inakataza watu kujiuaa lakini pia je hao wanaowauwa kwa mabomu hata kama sio waisilamu jee uisilamu unasemajeeee kuhusu kuuwa watu bila sababu??
Anasema mola

[ AL - BAQARA - 194 ]
Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu.

Hapo inaonyesha kwamba yule wakumshambulia ni yule aliyeanza kukushambulia kwanzaa sio kuanza wewe kushambulia ukalivaa bomu ukaenda kujiua na kuua wenzio wasio na hatia.

KWA HILI LA KUJIRIPUA MBONA JAMAA WAKO MBALI NA UISLAMU KABISA WALA WASIJINASIBISHE NAYO,NA NDYO MANA SERIKALI YA SAUDIA INAKAMATA WATU WENYE FIKRA HIZO WAKIBAINIKA TU KWA SABABU NI WATU HATARI WALIRIPUA MPAKA PALE MAKKA SASA HAO LENGO NINI KAMA SIO UHUNI TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio huenda,wanaajenda zao kwelikweli Ukitaka uulewe ugaidi vizuri na malengo yake anzia kwa wale hashashins ndo utapata picha nzuri.pia tafuts movie inaitwa the path of blood.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom