Tunakushkuru Jk kwa Kusema tatizo la Mafuta lina zungumzika na utatuzi wake ni huu?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunakushkuru Jk kwa Kusema tatizo la Mafuta lina zungumzika na utatuzi wake ni huu?.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jan 28, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1]Bila ya Wz’bar kutokuwa na imani na Raisi Shein , nilazima amuwajibishe haraka sana Ali Juma Shamuhuna kuendelea kushikilia wizara nyeti alionayo kabla ya kuleta asari zaidi.[/h]Written by Hassan10 // 28/01/2012 // Habari // No comments

  [​IMG]Ili uheshimike Mh Shein Muondoshe Shamuhuna na sio kumbadilishia wizara.
  Wazanzibar hivi sasa tumeingiwa na kiwewe na kutokuwa na imani na yoyote yule alie husika kwa njia moja au nyingine kusaidia hujuma za rasilimali za Zanzibar kuporwa,huyo tunamchukulia kuwa sio mzalendo wa Wananchi wa Zanzibar bali ni msaliti na sirahisi kuashiwa iwe ni funzo kwa wengine.
  Swala ni jee nikweli maneno ya Ali Juma Shamuhuna kuwa ni yeye tu mwenye kujuwa ombi hili la Serekali ya Muungano kwenda kimya kimya bila Mawaziri wa Smz na Serekali yake wakiwemo Wajumbe wa Baraza la Uwakilishi kuomba nyongeza Zaidi za Millli 200 za Bahari kuu ambayo iko upande wa Zanzibar na sio swala la Muungano wala halijawahi kuwa la Muungano ?
  Ikiwa Mh Ali Juma Shamuhuna kakiri wazi wazi mbele ya Baraza na Wajumbe wa Baraza letu la Uwakilishi ambalo ndio uti wa mgogo wa Serekali ya Mapinduzi ya watu wa Zanzibar kuwa suala hili ni yeye tu anajuwa lakini mawaziri na wajumbe wa Baraza hawajuwi, jee lakujiuliza wzanzibar alikuwa na nia gani ktk swala nyeti kama hili ambalo sio la Muungano wala sikwamba yeye ni Shamuhuna ni naibu Waziri wa Bibi Tibaijuka Waziri wa Ardhi na Makazi wa Bara?.
  Hapa nilazima Baraza letu tukufu la Uwakiilishi lipate jibu sahihi kutoka Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu swala hili la Ali Juma Shamuhuna lakuvunja Katiba ya Zanzibar na kuzarau Baraza na Wajumbe wa Baraza kuwaona kuwa sio lolote wala Chochote, na kinacho zungumzwa mule kwenye Baraza hakina nguvu yoyote .
  Hii sio kuvunja tu Katiba ya Zanzibar Mh Shamuhuna ,bali nikuzarau na kuleta kejeli katika Serekali halali iliochaguliwa na watu wa Zanzibar, mimi hainingii akilini kuwa Ali Juma Shamuhuna kuwa yeye yuko juu kuluko Katiba ya Zanzibar na baraza lake hata kama ni Waziri halali wa Ardhi.
  Kwa upande wa wananchi wa Zanzibar kuhusu asari za swala hili
  Hili swala ni zito na kubwa ambalo tukiliangalia kiundani asari zake mbeleni ni kubwa mno na zinaweza kuleta maafa na mazara ya mangamizi kushinda hata kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander .
  Meli ya Mv Spice Islander imezama kwa uzembe na tumepoteza ndugu zetu na tukashkuru M/mungu na hukumu ya walio fanya Allah ndio mwenye kujuwa kwa vile tayari wameshafika katika mbele ya haki na kila muhusika akajikukuta kuchukuwa au kubeba jukumu lakini roho za wazulumia bado hawaja poteza.
  Lakini swala hili mtu anakiri wazi wazi na kifua mbele kuwa mimi ndio muhusika mkuu ambalo ni swala nyeti na lenye kuhusu hatma ya wananchi wote wa Zanzibar katika rasilimali zao na hatma ya nchi yao huko mbeleni?.
  Jee tuseme Mh Ali Juma Shamuhuna hajuwi kuwa hili swala ni la hatari na linaweza kuzaa na kuibua mafa? Ni nchi ngapi ulimwenguni wachilia zilizo ungana nchi na nchi ndani ya nchi zenyewe zinamwaka damu kwa kupora mali za upande huu kwenda upande mwengine na wale wenye haki kuzalilishwa, jee leo ambapo rasilimali za Zanzibar kama bahari ambazo haziko kabisa ktk Muungano kama vile Tanzenet,Zahabu,Makaa ya mawe Gus ya Songosongo na almasi za Mwaduwi?.
  Jee Mh Shamuhuna hujijuwi au hujitambuwi kazi yako na Wazifa wako kuwa wewe ni Waziri wa Smz Serekali ya Mapinduzi ya Watu wa Zanzibar na sio Naibu waziri wa Tibaijuka?.
  Sasa vipi ujikubalishe na kujitowa muhanga kwa jambo kubwa kama hili linalo husiana na rasilimali zisizo za Muungano kulipeleka katika mambo ya Muungano wakati halimo kabisa,wewe nikama nani?.Au ndio kutuletea mtafaruki na mafa kwa wananchi wa Zanzibar?.
  Maana hatari ilopo mbeleni nikuwa Tanzania Bara wameshindwa kuyatowa mafuta katika Muungano haliyakuwa Wazanzibar wenyewe hawataki na wameshapitisa mswada katika Baraza la uwakilishi kuwa mafuta hayamo katika Muungano kama vile rasilimali za Tanzania Bara.
  Vipi wewe Mh Shamuhuna ulishukuwe swala kama bahari haliko kabisa katika mambo ya Muungano ulipeleke katika Muungano, una zamira gani wewe mbele ya wananchi wa Zanzibar?.
  Maana bila ya Bahari ilioko Zanzibar tena sehemu isio ungana kabisa na bahari kuu ya Tanganyika leo waje kuidai kuwa ya Muungano na wewe kutowa mgono wa Baraka katika wizara yako bila kuwajulisha mawaziri na Wajumbe wa Smz.
  Ulikusudia nini wewe?, kwa upande wa Tanzania Bara wangefanikiwa hili au Wakifanikiwa hili basi maangamizi makubwa yatatokea zidi ya Wazanzibar kulinda rasilimali zao kuporwa katika kigezo cha Muungano.
  Hakuna shaka kuwa huu ni uchokozi ulio wazi , haingii akilini kabisa kuwa mtu abiruke upande wa bili wa Uwa wako kuja kuchuma matunda yako kitu ambacho kiko ndani ya uwa wako na yeye hakimuhusu kabisa huu ndio uchokozi fika.
  Lengo la Watanzania Bara nikuomba bahari kuu ya Zanzibar na kuingiza utata mwengine katika kero za Muungano ili waweze kuleta meli lao ambalo hivi sasa liko katika ukanda wa Mtwara kuja kuhamia bahari ya Zanzibar kufyonza mafuta ya Zanzibar ambayo tayari wanazo report fika kuwa ukanda wa bahari kuu ya Zanzibar kuna mafuta mingi.
  Jia pekeyake yakuyapata mafuta hayo ni ujanja huu wasiri waliotaka kutumia kwa kuwashirikisha hawa mazalim wa Zanzibar wanaojita na kujifanya kumia na Zanzibar kumbe ni makatili zidi ya Wazanzibar.
  Ikiwa Wazanzibar hatukujifunga kimbwewe na hili basi mwambao wa bahari kuu ya Zanzibar tutaletewa vikosi vya ulinzi na mamanuari ili kuwaekea ulinzi wenye kuchima mafuta na rasilimali nyingine wachimbe kwa utulivu.
  Sasa chakujiuliza na kumuliza Raisi wa Muungano Jk kusema swala la mafuta lisutugawe na kuvunja Muungano linazungumzika na tunaweza kulitowa?
  Sasa jee kutowa wenyewe ni ujanja huu wa kutumia techknick hii ya wizi? Mimi siamini kabisa kuwa swala hili viongozi wa Smz hawalijuwi akiwamo Makamo wa Pili Mh Seif idi katika Baraza kukataa na kuwa analijuwa Ali Juma Shamuhuna tu kwa Zanzibar ? huu ni uongo tena zahiri.
  Jee tuseme huyu bibi Tibaijuka ni muongo na kama nimuongo basi viongozi wa serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Rais Shein ankanushe huyu Bibi?.
  Tukirudi kwenye kujitetea Waziri wa Ardhi na Makazi Profisa Tibaijuka tumnukuu.
  (Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema mpango huo umewashirikisha wajumbe na viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
  Waziri Tibaijuka alisema jambo hilo ni la Muungano wa Tanzania wala si la wizara yake, ndiyo maana waliamua kuwashirikisha wenzao wa Zanzibar.
  Ujumbe uliokwenda Marekani uliwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, si Tanzania Bara pekee kama alivyodai Jussa, hakuna haja ya kuvutana juu ya jambo hili.
  Aliongeza kuwa hawezi kukurupuka katika kulishughulikia jambo hilo bila Rais Jakaya Kikwete na Dk. Mohamed Shein kulifahamu, kwani yeye hana mamlaka nalo na aliukuta mradi huo ukiwa na miaka miwili.
  Waziri Tibaijuka alisema mchakato wa kuongeza eneo la ziada ulipitiwa na kushirikishwa kwa kamati mbalimbali, SMZ na Baraza la Mawaziri, ambapo wizara yake ilipewa baraka za kuendelea nalo.)
  Sasa Wazanzibar hapa ndipo tunapo changanyikiwa na kuchindwa kujuwa yupi mchawi wetu na majukumu ya viongozi wetu wa Smz kazi zao ni nini?.
  Ikiwa Mh Makamo wa pili wa Raisi Seif Idd na Mawaziri wenzake katiba baraza la Uwakilishi na ni part ya Serekali Wanasema hawajuwi kuhusu jambo hili na Mh Shamuhuna kukiri kuwa ni yeye tu mwenye kujuwa ? Sasa mtehani upo hapa Jee yupi mkweli na Yupi muongo? Ali Juma shamuhuna na Serekali yake ya Smz au Bibi Anna Tibaijuka ?.
  Hii ndugu zangu nihatari na tukifanya mchezo mchezo tunaweza Serekali yetu ya Mapinduzi ya Zanzibar na baraza lake tukufu la BLW inaweza kuonekana Serekali isio imara na zaifu na kufahamika kuwa ni Serekali ya Pwagu na Pwaguzi.
  Maana hivi sasa kuna ishara tosha kuwa Shamuhuna hakuhishemu katiba wala mamuzi ya wajumbe wa baraza letu la Uwakilishi aliono yote hayo hayana maana.
  Pale wajumbe wetu wa Baraza la Uwakilishi wanaposema kuwa wenzetu wa Tanzania Bara hawaheshimu mamuzi halali ya Baraza la Uwakilishi wanafanya zarau, basi zarau kubwa ni sisi wenyewe .
  Mfano mdogo tu ni huu wa Shamuhuna,ikiwa wewe mwenyewe hujiheshimu nani ata kuheshimu?
  Sasa ikiwa sisi wenyewe Wazanzibar hatuna msimamo moja anatokea mtu kama Ali Juma Shamuhuna anakuwa na mamuzi yake bila kuingiliwa au kutaka uchauri, jee hii niserekali gani? Si hio ya Pwagu na Pwaguzi?.
  Shakufanya Wazanzibar hivi sasa ni kujifunga kimbwewe ili Donda lisipowe likipowa tumeumia na hawa Watanganyika watatafuta tecnick nyingine mpaka wafanikiwe lengo lao.
  Hivi sasa nikumbinya Shamuhuna katika Baraza la Uwakilishi ili atupe majibu wazi kuwa ni nani na nani walioshiriki katika hujuma hii?, na likibainika hilo nilazima viongozi wenye majukumu wa Smz wawawajibishe na tusiwe na mambo ya kimjomba mjomba hatutokwenda.
  Na Nilazima tufunguwe kesi kwa Waziri asio wa Tanzania Bara Tibaijuka kutaka kupora mali zisizo za Muunngano na kuishirikicha UN katika hujuma hio,ikiwa Tibaijuka anasema kapata Baraka basi atatwambia ni kutoka kwa nani na nani ili tutawajuwa wachawi wetu.
  Hiyi inayo zungumzwa kuwa Mh Shein ,Saif Idd,Kificho na Hamad Rashid kuwa wote ni katika mtandao moja inawezekana nikweli na wala tusipuze nilazima lifanyiwe kazi ili kujuwa mchawi wetu ni nani na nani?.
  Ali Juma Shamuhuna kapata mkono wa Baraka na sio peke yake wako watu nyuma yake inasemekana Baada ya kupewa Shein uraisi wa condition za kuyapeleka mafuta Bara na kula kipo kisicha kuwa sio halali kulinda na kuwenzi Muungano na kujikubalisha kuwa Waziri katika baraza la mawaziri la Tanganyika aliekewa wafuasi wake wa kusaidiana kazi ili lengo litimie.
  Yani katika tetesi Kificho yumo Seif Idd, Na Hamad Rashid alipewa kazi ya kukivuruga chama ili hofu kubwa ni kuvunja nguvu ya cuf kwa vile tayari ni part ya Serekali ya mapinduzi ya Zanzibar.
  Kwa hio Wazanzibar wenye kuitafuna Zanzibar ni Wazanzibar wenyewe.
  Mungu ibariki Zanzibar na tulinde na maduwi wa Zanzibar.


  www.mzalendo.net
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  u mwehuu! Znz ni sehemu ya jamhuri
  ya muungano
   
Loading...