Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hujui source of money? Nchi hii kwani ina upungufu wa vyanzo vya mapato? Tatizo letu ni collection and allocation tu, pesa ziko nyingi sana.

Je ushajiuliza hiyo nyongeza ya posho za wabunge imetoka wapi? Nadhani hauko nchini, kwani kama ungekuwepo ungekuwa unafahamu mapendekezo ya tucta ni yepi katika kutaka nyongeza ya mishahara na vyanzo vya kuongeza mapato.

Hatahivyo najua ulishachagua upande, na hakuna mshangao kusikia kauli kama hii toka kwako.

Mapendekezo ya tucta ndio yapi? share na watu basi wewe si unajua? nipe source of money??

Maswali mengi naona ni kuongeza matumizi ya serikali (yale yale) bila kueleza pesa itatoka wapi??

Collection na allocation nayo ni chanzo? au; collection na allocation inahitaji mkakati; mkakati unahitaji pesa pia..
 
Toa ugonjwa Wako hapa,hebu thibitisha vyuo vipi vya ukristo vilikuwa hoi before 1992 tatizo waislamu mnathamini mno ubwabwa,madrasa,matamuko nk.muda huo wa kristo wanautumia kuitisha harambee kuwezesha ujenzi wa mahospitali,shule,vyuo nk

Usingeandika niliyo undeline nisingekujibu; lakini nilipo undeline unawatukana waislam wote Tanzania; wewe unawalisha waislam; wewe ndio unaendesha shule zao? wewe ndio unaendesha misikiti yao?? acha hizo..

Truce must be told; MoU ni uwizi wa feza za umma kuendeleza miradi ya kanisa ambayo kila mtu anajua ni ghali sana; tunachotaka hizo pesa za umma (zikiwemo za waislam) zikaboresha shule za kata;dispensaries etc.. tutaendelea kulipia hospitali za kanisa kama tunataka huduma zao;

acheni kuendekeza udini kwenye mali za pamoja ala!
 
Dada tunakushukuru sana kwa kutupa nafasi hii. mimi naomba uwasilishe kilio cha watu wasio na watu wa kuwasemea. hawa ni poli na maafisa wa usalama wa taifa. kwa kweli wanafanya kazi basi tu. mishahara yao ni midogo haiendani na hali ya maisha pia hasa wa usalama wa taifa ambao hata kukopa kwenye mabenki hawaruhusiwi. nani ndugu yangu wa damu ni shiida tupu amenipa hali halisi kwa kweli inasikitisha. mafuu waliopo dar. lakini ukweli ni kwamba usalama wa taifa ilikuwa zamani na wanataabika sana mishahara yao ni midogo hawana rushwa na kazi yao ni ngumu vitendea kazi wanatumia wakubwa tu dar huko mawilayani maafisa ni kutia aibu, ndio maana wengine wanajilewea tu. mkawasaidie hawa ndio washauri wa rais ndio maana unaona hatuendi. MSISAHAU HILI WADAU.
 
Mapendekezo ya tucta ndio yapi? share na watu basi wewe si unajua? nipe source of money??

Maswali mengi naona ni kuongeza matumizi ya serikali (yale yale) bila kueleza pesa itatoka wapi??

Collection na allocation nayo ni chanzo? au; collection na allocation inahitaji mkakati; mkakati unahitaji pesa pia..

Mapendekezo ya tucta yatafute hata hapa JF utayapata.

Na zaidi ya tucta, asasi mbalimbali zimekuwa zikiishauri serikali namna ya kuongeza makusanyo, nitakushangaa kama utakuwa hujawahi kuyaona.

Collection and allocation ni kukuonyesha kwamba hata sasa fedha zipo za kutosha kuwalipa. Nimekuuliza mbona nyongeza ya posho ya wabunge imepatikana? Mbona Jairo aliweza kukusanya zaidi ya milioni mia nne? Pesa zipo tena nyingi sana.
 
Kero ya Muungano! TANGANYIKA KWA NINI IUAWE! tunachotaka!
serkali3! au serkali1! isipowezekana muungano huu wa kisanii UFE, Na usiwe na kumbu kumbu!
 
wananchi wa kemondo,muleba na hasa ihangiro wanalia na sanaa ya serikali. Kwanza serikali imeua bei ya kahawa,then ikasema bungeni,limeni jatrofa,wananchi wakadanganyika kulima,nakwambia nenda leo uone,hamna anayetaka hata kusikia kilimo icho,pia jatrofa zimeua migomba yote na sasa wameanza kuishi kama jangwani.
 
Kero yangu mimi ni kuhusu ukomo wa mtumishi wa umma, mara kadhaa sasa tumekuwa tukiteuliwa wastaafu mbalimbali kushika ofisi za umma. Hivi kwa nini tulidesign mfumo wa kustaafu tukiwa na miaka 60???Mimi nadhani kunasababu za msingi za kumpumzisha mtumishi aliyetumikia hadi kufikia muda huo.

Kwangu haiingii akilini kwa mtu mwenye umri wa kustaafu kushika ofisi za Umma kama balozi, Mkurungenzi, Mwenyekiti wa Tume etc. Kama mtu huyu ana nguvu apewe nafasi kwenye vyama vya siasa na sio kurudishwa tena kwenye utumishi wa umma. Kwani hakuna vijana wa kushika hizo nafasi??au tunasubiri hadi vijana nao wastaafu ndio wapewe hizo post???

Nionavyo mimi sio kuwa ukiwa kijana sana ndio utashindwa kuwa balozi/waziri, kwani hao wazee wenye mauzoefu wengi wao wanaishia kutuibia na kulala tu maofisin kwa kutokuwa innovative. Tena hata kama ni Mbunge iwe ukishakuwa na zaid ya miaka 60 ichukuliwe kuwa umeshapoteza sifa ya kuwa Waziri.
 
sjamaliza...muleba ilikuja TASAF wakafyeka miti ya ekalyptus wilaya nzima eti inakunywa maji na kuzalisha acid,wazee waliokuwa wanategemea misitu kwa mbao na kuuza kuni wakafa kwa presha,waliobaki wakaendelea kudai mahakamani ila wameanza kuzeeka na kufa mmoja mmoja bila majibu...jamani taifa laenda wapi? pia meli ya muleba iliuzwa bila kuhusisha wananchi kwa nini? kwangu ni kero. Pia twende arusha,licha ya kuwa Geneva ya afrika,leo hii kijenge nzima haina lami,nenda sekei ,sakina,ngulelo koote siku za
 
Dada tunakushukuru sana kwa kutupa nafasi hii. mimi naomba uwasilishe kilio cha watu wasio na watu wa kuwasemea. hawa ni poli na maafisa wa usalama wa taifa. kwa kweli wanafanya kazi basi tu. mishahara yao ni midogo haiendani na hali ya maisha pia hasa wa usalama wa taifa ambao hata kukopa kwenye mabenki hawaruhusiwi. nani ndugu yangu wa damu ni shiida tupu amenipa hali halisi kwa kweli inasikitisha. mafuu waliopo dar. lakini ukweli ni kwamba usalama wa taifa ilikuwa zamani na wanataabika sana mishahara yao ni midogo hawana rushwa na kazi yao ni ngumu vitendea kazi wanatumia wakubwa tu dar huko mawilayani maafisa ni kutia aibu, ndio maana wengine wanajilewea tu. mkawasaidie hawa ndio washauri wa rais ndio maana unaona hatuendi. MSISAHAU HILI WADAU.
Kundi hili ulilolitaja acha liumie tu maana hawa ndo wanadiriki kucheza michezo michafu wakati wa uchaguzi. Usikute bila nyinyi leo tungekuwa tunaongelea mambo mazuri. Sasa kama hamlipwi vizuri inakuwaje huwa mnatusaliti wakati wa uchaguzi??????Nyie pigikeni ili 2015 tukiongea tuwe tunaongea lugha moja.
 
...ni kwani viwanja vya wazi vya city center kwa sasa vinajengwa?je ikitokea maafa wananchi wanaweza kukusanyika wapi? pia ni kwani jengo la Embassy hotel apo karibu na ohio limefungwa miaka nenda rudi kwa mgogoro usio na msingi wakati ni mali ya umma?je nikwanini govt inajenga chuo cha utalii hatua 8 toka chuo cha ifm wakati hata ifm haina hata madarasa ya kusomea?na chuo cha utalii kujengwa city centre kunaleta mantiki?kwa nini si sehemu za utalii?
 
..mimi hoja zangu zote zimejikita ktk MUUNGANO.

..kwanza, napendekeza wabunge mtusaidie ili Watanganyika tukienda Zanzibar tutumie PASSPORT, na Wazanzibar wakija Tanganyika waje na PASSPORT.

..pili,tungependa mapato ya serikali ya muungano yawekwe wazi. tunataka kujua kila upande unachangia kiasi gani ktk shughuli za muungano. zaidi tunataka tuujue formula ya mgawanyo wa mapato ya muungano na justification zake.

..tatu, suala la MAFUTA na GESI liondolewe haraka katika mambo ya muungano. hakuna haja ya kusubiri mjadala wa katiba mpya.

..nne, suala la VITAMBULISHO VYA TAIFA. kwa kuwa hatujui hatima ya muungano wetu kama utasalimika, basi hatua za tahadhari zichukuliwe ambapo VITAMBULISHO VYA WATANGANYIKA viwe tofauti na vile ya Wazanzibari.
 
School Fees! ADA za Private School ni za KINYONYAJI,kiundwe chombo cha kuzisimamia hizi private school kama EWURA.How come kila mtu anakimbilia kuanzisha shule? Yaani siku hizi biashara ya shule imekuwa kama biashara ya Mafuta?
 
Embassy hotel na Agip Motel tuliibua humu,wakaibukia magazetini eti soon panashughulikiwa,mpaka leo ni magofu! Dada Regia pointi hii pia!
 
Michezo imesahaulika! Majeshi yahamasishwe kuwekeza kwenye michezo lakini pia kila mkoa ufungue sport academy zaidi upande wa soka kwa vijana under 20 wawe sehemu ya Veta ili wapate ruzuku! madini haya Dada Regia!
 
nasisitiza shule zote za veta wafundishe Michezo na Muziki kama course inayojitegemea!! Hivi vyuo vya veta vimetapakaa nchi nzima!
 
Kero yangu mheshimiwa mbunge, ni nyinyi wabunge kujilipa posho nono nono ilhali watanzania walio wengi wanaendelea kusota na mishahara isiyokidhi mahitaji!- peleka swali hili bungeni, la ni lini seriakli itaandaa muswada wa sheria ili kuondoa posho za vikao vya wabunge, na vingine visivyo na tija?, maana mnalipwa mshahara ati!
 
Mapendekezo ya tucta yatafute hata hapa JF utayapata.

Na zaidi ya tucta, asasi mbalimbali zimekuwa zikiishauri serikali namna ya kuongeza makusanyo, nitakushangaa kama utakuwa hujawahi kuyaona.

Collection and allocation ni kukuonyesha kwamba hata sasa fedha zipo za kutosha kuwalipa. Nimekuuliza mbona nyongeza ya posho ya wabunge imepatikana? Mbona Jairo aliweza kukusanya zaidi ya milioni mia nne? Pesa zipo tena nyingi sana.

umeshafanya hesabu ya hela inayohitajika kwa mapendekezo unayoyatoa au unalalamika bila kujua gharama zake ni shillingi.it is always easy to say than to do..

nafikiri tutoe mapendekezo (lalamika) na source ya ku-finance ili iwe rahisi kupata solution; unajua waajiriwa ni walalamishi tu kumbe mwajiri anahangaika kutafuta sources za kupata pesa..
 
-takataka jamani miji na majiji yamegeuka madampo kila mahali ni takataka kwa mfano Dar maeneo ya mwenge kila barabara ina dampo pembeni yaani kero kwani yanasabibisha harufu kali, wadudu na vijidudu mbalimbali vinazaliana na kisaikolojia watu wanapata madhala kwa kuyaona hapo! mwe!

Nitarudi tena dada!
 
Hii ni moja ya njia ya mawasiliano. Au ndugu umezoea kusikiliza ya wakubwa peke yake? Badilika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom