Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Regia Regia Regia tafadhali sana!
Frankly speaking, kwa upande wangu hii haijanivutia hata kidogo. Hivi mpaka leo kuna mtanzania yeyote bila kujali ni mbunge au mwananchi wa kawaida asiyekuwa na cheo chochote, asiyejua kero za watanzania hadi inabidi awaulize ndiyo azielewe? Aisee Regia tumekutuma huko Bungeni tukiwa tuko siriazi, unataka kuanza kufanya nini? Kumbe umeingia Bungeni ukiwa hata kero za wattanzania huzijui? Kwa nini? Ungeniambia unakusanya mawazo ningekuelewa, mawazo yanakava vitu vingi kuliko kero. Kero ni too specific kiasi ambacho sitarajii mbunge kama wewe urudi kwetu kuja kutuuliza. Tafadhali tafadhali tafadhali
!

Duh mkuu yamekuwa hayo tena. Haka nako kaneno
 
Kuna mambo manne tu ambayo watanzania ni lazima yafanyike ili kuikomboa nchi yenu katika kuondoa kero na kuleta hali nzuri kiuchumi kwa wananchi wenu.
1. Kupata Katiba iliyo bora.
a. Katiba yenye kulinda maslahi ya taifa lenu na kujali maslahi ya wananchi kwanza.
b. Katiba yenye kulinda rasilimali za Taifa lenu na kuzimilikisha kwa wananchi
c. Katiba itakayowafanya viongozi wote waliochaguliwa na wananchi waweze kuwajibika kwa wananchi na sio vyama vya siasa.
d. Katiba itakayoangalia uwezekano mkubwa wa kuinua hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja mpaka kwa taifa zima kwa kifupi katiba yenye utashi wa kujenga uchumi wenu na kuondoa utegemezi.

2. Wananchi kupenda kuwajibika katika kulijenga taifa lenu. Hapa panahitajika zaidi kujenga msukumo na tarbia yya wananchi kulipenda kwa dhati taifa lenu na kuwa na kiu ya maendeleo . Kuchukia rushwa na ubinafsi na kupenda kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yenu

3. Viongozi kuacha kutumia afisi za umma na madaraka katika kujilimbikizia mali binafsi. Hapa panatakiwa kuweka sheria kali kulidhibiti hili


4. Taifa kuwa na mtazamo wa kiuchumi zaidi na sio siasa. Kila kitu kinachohusi maslahi ya taifa ni lazima kitazamwe kimapana zaidi katika angle ya kiuchumi na si kisiasa

Mkifanikiwa kurejesha hayo juu basi pasi na shaka mtaanza kusonga mbele.

Kila la kheir

Mifuko ya hifadhi ya jamii isiwe mapango ya wezi mahali ambapo pesa za uchaguzi zinachukuliwa wakati wenye mfuko (wafanyakazi) hawafaidiki kwa lolote. Pia itafutwe namna bora ya kuwanufaisha wafanyakazi kwa kulinganisha mifuko yenye kutoa mafao bora kwa wafanyakazi kabla na baada ya kustaafu tofauti na ilivyo sasa mfuko kama PPF ni wizi mtupu kwani fomula wanayotumia hata haieleweki na ni wizi mtupu suala hili liangaliwe kwa kina kwani wizi wa taasisi hii unawaumiza sana wafanyakazi wa Tanzania.
 
ni nia njema toka upinzani. Hapa tatizo si ajira tena maana imeshakuwa koras flani. Tunataka mje na suluhu ya vijana kujiajiri. Na hili lianzie vijijini zaidi maana huko ndo wanatoka wengi. Mjini ni uchuuzi tu. Vijana wanamaliza elimu zao na kubaki hapa mjini dar. Tungependa kuona popote panakalika bila kijana kuhisi kukosa kitu. Hili cdm mtaliweza? Mtalitekeleza vipi?
 
Dada regia naomba ufikishe kero hii;
Kwa nini wananchi tunatakiwa kulipia huduma kwenye office ya serikali za mtaa wakati kodi tunalipa.
mi nashangaa, mtu kupewa barua ya utambulisho inabidi kutoa 5000 Tsh really!!!!! inashangaza sana
 
Watumishi wa umma kupandishiwa mishahara lakini bado wanalipwa kwa rates za zamani (hawajarekebishiwa mishahara yao)

Hii ni moja kati ya kero nyingi ambazo zinawasibu watumishi wa umma.Hh kikao kijacho nitakuwepo Dodoma.Nitapenda nipate mawasiliano yako ili nikupatie baadhi ya vielelezo vya watumishi kadhaa ili mvipitie na kupata picha ya tatizo.
 
Kero nyingine ni hii vyama vyenye WABUNGE na kingine kina RAIS pia lakini vinachota mamilioni kama RUZUKU kila mwezi kutoka hazina yetu. Shule zetu hazina madarasa, madawati, maabara lakini tunagharamia SIASA kama mazuzu vile. Vyama hivi vina WANACHAMA kama makanisa na misikiti ilivyo na WAUMINI. Vijiendeshe.
 
Wazo ni zuri,
Tunataka kujua watu wale wanaoishi kando ya maeneo ya migodi huku nyumba zao zikiathirika kwa mitikisiko ya baruti kila siku (zinapata nyufa) na kuendelea kupasuka taratibu na kuzifanya nyumba kuanza kubomoka ama kuzeeka kabla ya muda wake mtawasaidia vipi endapo tutawaweka madarakani.
 
Kero yangu ni maji katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam hasahasa Manispaa ya Temeke.

Je ni lini serikali atafikisha maji ya bomba maeneo yote ya jiji na kwa nini serikali isisubsides watu wanaochimba visima na kuuwazia watu maji kwa bei ya juu ili kama wanauza maji basi yaendane na bei ya dawasco? Je serikali haioni kushindwa kufikisha maji kwa watu wake na kuacha watu wajiudumie wenyewe kuna siku kutakuja kutokea matatizo makubwa zaidi ya ukosefu wa maji siku za usoni na kujikuta serikali ikilazimika kuzima moto kwa jambo ambalo lingefanywa bila msukumo wowote?
 
Nataka serikali iulizwe hivi:

Kwa kuwa hakuna ajira kwa vijana na kwa kuwa wamachinga wengi wamekataa kwenda kufanyia biashara zao pale Machinga Complex:
  1. je serikali haioni ni hatari kwa wamachinga kuzagaa kila mahala na kufanya maeneo ya wapita nji kuwa ni masoko?
  2. Je serikali haioni kwamba ni hatari sasa kwani wamachinga wanauza silaha kama mapanga huko mabarabarani kama pale Ubungo mataa? Je Serikali ina mpango gani wa kuwaondoa hao machinga wauza mapenga mabarabarani kwa kuwa wanatishia maisha ya wapita njia?
 
Hongera sana kwa kazi nzuri ya ukombozi wa Taifa letu.Usiumize kichwa kubishana na hao wachache ambao malengo yao humu Jukwaani yanajulikana.Wenyewe wanataka kuonekana kuwa wanapingana na CDM.[/QUOTE]

Mwenzio ameelewa amejibu vizuri wewe unatoka huko unasema watu wanabishana! Uwe unasoma posts kwa furaha siyo unasoma ukiwa na msongo wa mawazo.
 
Asante sana dada!!
Mimi nawomba sana wabunge hasa wa CHADEMA!
Suala la madaktari na wataalamu wengine wa fani ya afya walio katika kazi kwa uangalizi(Internship) kwanza kabisa naomba mpate nafasi ya kumwambia waziri wa afya kwamba hawa si wanafunzi ni graduates na wapo katika Intrtniship na jamii yote ielewe hivyo na ndio wanao wahudumia watanzania katika hospitali nyingi nchini kwani watanzania wachache sana wanauwezo kwa kuhudumiwa na madaktari bingwa......Kwa hiyo wanastahili kuthaminiwa na kupew stahiki zao!! Na serikali iache kuingiza siasa katika mambo ya msingi!! Kwa hiyo naomba mkaikemee serikali kupitia wizara ya afya kitendo walichofanyiwa hawa wataalamu wetu si cha kiungwana na cha kinyama na serikali inapaswa kuomba radhi mara moja!! Kwani kwa kufanya hivyo inaweza kurudisha imani kwa kundi hili na taaluma ya utabibu nchini na iwe mwisho kushughulikia maswala yanayo husu maisha ya watu kisiasa!! Ikibidi waziri Kivuli wa afya Mh.Gervas anaweza kwenda na hoja binafsi yakutokua na imani na waziri wa afya kwa jinsi alivyolishughulikia suala hili kwani limesababisha usumbufu mkubwa na hata maisha ya watu kupotea!! Tuko tayari kumpatia ushirikiano ikiwa ni pamoja na takwimu na vielelezo vingine kufanikisha hilo!! TAFADHALI SANA NAOMBA DADA REGIA MTEMA MAMBO HAYA YAFIKE NA WATANZANIA WANASUBIRI KUSIKIA KUTOKA KWENU,MSIWANYIME HAKI HII MUHIMU YA UWAKILISHI!!
 
Kero nyingine ni hii vyama vyenye WABUNGE na kingine kina RAIS pia lakini vinachota mamilioni kama RUZUKU kila mwezi kutoka hazina yetu. Shule zetu hazina madarasa, madawati, maabara lakini tunagharamia SIASA kama mazuzu vile. Vyama hivi vina WANACHAMA kama makanisa na misikiti ilivyo na WAUMINI. Vijiendeshe.

Tuna heri sisi mbunge wetu,Wenje aligawa madawati 500,mengine yanakuja!
 
Lakini sisi pia tulio Arusha,tunajua kazi ya mbunge wetu Lema!Natamani nchi yote ingekuwa na wabunge wetu hawa!
 
Mnyika anastahili hiyo post kuliko Mimi..Unafikiri kuwa na sifa ya Uenezi ni kuanzisha sredi hapa JF?Uenezi ni zaidi ya hayo Mkuu...
swali kwa Mh.Mume wangu yeye alikuwa mbunge lakini alinikataza mimi kuwa Mbunge hasa kwa viti maalum,nilimuhoji lkn alikataa kunipa undani.lkn niligundua ni Wivu alionao baada ya kuishi sana Bungeni na kuona mengi. jee unatwambiaje dada kwa hili?[/QUOTE]

Kumbe umekuwa Mwanamke Siku hizi?Na hivyo vibinti vinavyopatia mimba madrasa inakuwaje?huyo mume wako ana wivu wa kijinga,anadhani ngono iko Bungeni tu?
 
Regia,

Bado naendelea...

[19] Sheria ya ajira kwa wageni itazamwe upya.Kampuni nyingi zinatoa ajira kwa wageni wasiokuwa na sifa na ujuzi wa kutosha.Kampuni za waIndi zimeajiri waIndi kibao toka India na Pakstani.Ukija Arusha kampuni za utalii zimeajiri wageni kibao kuanzia wapishi,driver,tour guide,wahasibu,procurement officer,operation officer na nk.

[A] Napendekeza sheria itaje wazi mgeni atapata ajira itakapothibitishwa ujuzi wake haupatikani Tanzania.

Napendekeza ada kwa wageni ipandishwe maradufu na itozwe kwa fedha za kigeni yaani U$ kuanzia 1,500 mpaka 10,000/ kwa mwezi ili kuwakatisha tamaa waajiri wanapenda kuajiri wageni badala ya kuajiri waTanzania.

[C] Napendekeza wageni wote waliopewa ajira hapa nchi ajira zao ziwezina renew kila baada ya mwaka mmoja.

[D] Napendekeza waajiri wakikutwa na kosa la kuajiri wageni watozwe faini kuanzia U$ 1,000,000/= kwa kila mgeni mmoja.

[E] Napendekeza uanze msako mkali kwenye kampuni zote ili kubaini kampuni zote zilizoajiri wageni.
 
Serikali isiwe na kigugumizi pale Bunge linaporidhia maamuzi..Jairo, Ngeleja, Luhanjo, Uda na akina Iddi Simba, Hivi haya yalijadiliwa tuu bungeni kisha wakapokea Laki 2 zao kila mmoja wakachapa mwendo..Hizi ni kero na Wananchi tunasikia.
Kesi ya Akina Mramba, Mahakama ni Watu Si Jengo.. Hizi kesi ingekuwa za kuku mambo yooote Hadharani, Miaka 10 Jela.Ila sasa hawa mapapa Keri zinapigwa miezi tuu kwani Mahakimu tunaishi nao mitaani hawajashuka mbinguni.KERO HIYO.

Sikio La kufa halisikii Dawa,, hivyo maadam ni la kufa inabidi lifarijiwe japo na Panadol....
 
Ntakushangaa sana kama wewe ulikuwa ulijui hilo.

Mimi ni Raia wa Oman, mzaliwa wa Kianga , Mwera, Zanzibar na nimesoma Tanzania Bara na nimewahi kufanya kazi Serikalini Muungano kwa miaka 8 .

Kumbuka Jf ni kwa wote. Soma rules zake utaligundua hilo. Na ndio maana najipambanua pasi na kujificha.

Sijui kama una la ziada.


Sasa wewe raia wa Oman, mambo ya serikali ya Tanzania unataka kuyadadisi kwa faida ya nani?
Ulishakimbia tuachie siye tuliobakia na kukomaa na serikali yetu japo maskini tukomae.Unachochangia kama "mgeni" hakina uzalendo hivyo kitatia shaka kama kina maslahi ya nchi.
 
Langu ni Moja tu ambalo linakata pande mbili:

Nendeni kaiulizeni kwanini Serikali haitekeleze mapendekezo ya Kamati Maalumu za Bunge hasa ktk haya mambo ya Kifisadi? Na kama Serikali haina majibu, na kama ikisema bado mambo yanashughurikiwa, pigeni kura ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu ili baraza zima livunjwe na liundwe upya.

Upande wa pili ni huu; Ikiwa kama mtashindwa hilo hapo juu, basi Bunge kama Bunge, litakuwa limeshindwa kuisimamia Serikali na hivyo kushindwa kufanya kazi yake muhimu ya kwanza ya kuisimamia Serikali kama muhimili huru, na kwa maana hiyo, peleke hoja ya Bunge kuvunjwa ili liundwe Bunge jipya linaloweza kusimamia Serikali.
 
Ngongo,
Mkuu una mapendekezo mazuri sana hasa kwenye eneo la ajira hadi nimetamani waziri wa kazi mama kabaka ndiye angekuwa amekuja kutafuta maoni ya wadau hapa, kwani baada ya hapa angekwenda moja kwa moja kutekeleza.

Hatahivyo nina matumaini makubwa na wabunge wa chama changu na shukrani za pekee kwa Regia kwa kutaka maoni yetu wanaJF. Naamini amepata changamoto nyingi zinazowakabili watanzania na wakizifanyia kazi vizuri kama ilivyo ada yao, tutanufaika sana wananchi.
 
Wakuu habari! Nimatumaini yangu kuwa tunaendelea vizuri na majukumu yetu ya kila Siku.

Nimeamua kuanzisha Uzi huu kwa lengo la kukuza ya kero,maoni,ushauri na chochote toka kwenu ili tuweze kuyasimamia ndani na nje ya Bunge.Kwa kutambua kuwa wanaJF wamesambaa kila mahali,maofisini,mashuleni,mitaani,majumbani na huko kote kuna kero mbalimbali zinazohitaji attention ya Serikali lakini mambo hayaendi na ungpenda kuona suala hilo linafanyiwa Kazi na hivyo unapendekeza Kambi ya Upinzani izibebe na kuzisimamia. Basi tafadhali toa kero,maoni,ushauri au hata mapendekezo yako hapa.

Tafadhali kero ziwe za kijamii na sio za mtu binafsi.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati kwa Ushirikiano wenu.

Wenu katika Ujenzi wa Taifa
Regia Mtema


Ahsante sana na nakupongeza kwa ubunifu huu. Kwenye msafara wa Mamba huwezi kuwakosa Kenge!!
Kero zangu kubwa ni:
1. Tuliamini katiba mpya itakuwa ni mkombozi kwa kipindi kilichobaki, tumesikitishwa na ubabe ktk maamuzi ya viongozi wetu, Mh. mtatusaidiaje kwa udogo wenu i.e idadi ili tupate kitu tulichokitarajia.
2. Tunashuhudia askari trafiki wakitusimamisha na kuamua ulipe faini au uwatoe hii sio haki na wakati mwingine sio kosa lako au ulihitaji msaada wa kuelekezwa tu. Serikali ibuni mfumo mpya wa ulipaji faini unaandikiwa kosa unalipia benki kwa kipindi atleast cha mwezi ili upate muda wa kujiandaa. Kwa leseni mpya ni rahisi kukutrace.
3. Kuna mikopo ya serikali kwa wafanyakazi wa umma iwekwe wazi kwenye internet ili tuijue na masharti yake na nani wanaamua kukupa mkopo na yawepo mazingira ya fair ground ktk utoaji wa mikopo hiyo.
Nacharge simu yangu nitarudi. Thanks
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom