Tunakupongeza Askofu Shao kwa uzalendo wako, Padri Mapunda, Dr Slaa kuweni na huruma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunakupongeza Askofu Shao kwa uzalendo wako, Padri Mapunda, Dr Slaa kuweni na huruma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Jul 8, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Kwa Watanzania wanaotakia mema nchi yetu wanampongeza Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Dr Martin Shao, kwa uzalendo wake alipowasihi madaktari waliogoma katika hospitali mbali mbali nchini ikiwemo hospitali ya KCMC kureja kazini huku wakiendelea na madai yao serikalini.

  Wananchi wengi wamefedheheswa na kauli za Padri Babtiste Mapunda na Dr Slaa, kuunga mkono mgomo wa madaktari...Padri na Dr Slaa, waelezeni Watanzania kwa maoni yenu mgomo unamkomoa nani? Na kumuumiza nani? Je ni kweli migomo ya aina hii inawafikia walengwa na kuwaonjesha maumivu yatokanayo na mgomo?

  Dr Slaa, tembelea muhimbili na kakae pale mapokezi walau kwa saa mbili tu ili uone mwenyewe wagonjwa wanavyoteseka na wengine wanavyokufa kwa kukosa huduma halafu uwaambie Watanzania mgomo uendelee hadi lini ama ujirudie mara ngapi ili kuwashikisha adabu hao unaodhani ndio wakosaji na wasiotaka kutoa stahiki ya madaktari..

  Tunashindwa kuamini Dr Slaa na Padri Mapunda, wameshindwa kuwahurumia Watanzania wanaoteseka na huku wengine wakifa baada ya kukosa huduma ya kitabibu, miongoni wanaougua ni wanachama wa Chadema sasa watu hao wakifa si anapoteza wananchama.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Dr Slaa na Padri Mapunda ndio mwajiri wa Madaktari? Au ugomvi uliopo ni kati ya madaktari na Dr Slaa & Padri Mapunda? Mbona mzee Massnja hajasema chochote na hujamtaja? Hii obsession na Dr Slaa itaisha lini?
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kwani msitu umekatwa miti? wakamateni mkawafanyie ya Dr. Uli maana kiwango chenu cha kufikiri kimefika ukomo kiasi cha kudhani (kipuuzi) kuwa kutesa na kuuwa ndiyo suluhu ya kushindwa kwa serikasli yenu.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Dry as dust! mwambie JKilaza ayashughulikie madai ya madaktari.
   
 5. h

  hans79 JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Rudi mirembe ,mtu sio mtawala anawezaje kuwaamuru wafanyakazi wagome ? Inaleta taabu juu ya uelewa wako .Katangaze radio ya kuwa Dr Slaa ndiye kiongozi wa nchi hii.
   
 6. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  padri slaa mzee wa kushadadia mambo yule ili apate covarage kwenye magazeti
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nasikia mke/demu wako wa UDOM anapenda kuliwa 0713 sana !
   
 8. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Naomba Ritz unijibu What is Dr Slaa in all this mess? Prime minister?
   
 9. t

  tubadilike-sasa JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 677
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Huu ni upuuzi. Tangu mgomo ulivyoanza wamekufa watu wangapi? Unazo data? Au unafikiri kwa kutumia ma....... yako? Huduma za dharurua si zilikuwa zinaendelea? Acha siasa kwenye mambo ya msingi.
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Dada unajiaibishaje?
  Kichwa unacho lakini hukitumii!!!
   
 11. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  We una akili ya maiti'
  slaa anahusikaje kwenye mgomo?
  Acha kuwa na akili ya maiti! Unataka kutuaminisha kwamba slaa anahusika?. Wewe ni mwehu?
   
 12. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  WAKIRUDI KAZINI BILA MAHITAJI YAO KUTEKELEZWA NI HATARI ZAIDI KWA WAGONJWA MAANA,wao walikuwa wanahitaji vifaa vya kzi na madawa hospitalini, sasa kama hivyo hakuna hata wakirudi kazi watafanyaje?huoni kama watu wataendelea kufa tu?
   
 13. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kawaabie mashekh watatue suala la mgomo kwani maaskofu na mapadri tumewasikia. Influence yao ni nini kwenye issues za maana kama hili zaidi ya kulilia posho ya serikali wanaposhughulikia ndoa?
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Dr. Martin Shayo ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa hospitali ya KCMC. Ulitegemea angetangaza mgomo?
   
 15. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ritz,

  Acha uzumbukuku au kuwa Zuzu. Dr.Shao anahangaikia hospital ya KCMC ya kanisa Madaktari warudi ili afanyie biashara period, Nani kakuambia ana huruma na wagonjwa . Ile hospital ya good Samaritan ilikuwa miaka ya sabini Kabla Nyerere hajaichukua ikadidimia mpaka ikafanywa uchafu. Sasa hivi ni Chuo Kikuu cha Tiba sawa na Mhumbili chini ya Kanisa inafufuliliwa kwa kasi huku CCM wanaifanya Lugalo military hospital kuwa ya Ruffaa how come?

  We need a Regulator for Universities , Schools,Hospitals halafu tukuasanye kodi acheni Uzuzu.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Waungwana wengi tulijarajia kwamba Padri Mapunda angetumia mimbari ya dini yaani jukwaa la Altare kuwasihi madakatari wawahurumie wagonjwa na kutafakari athari za mgomo kwa raia wema wanaohitaji huduma yao na ambao hawahusiki na makosa ya mwajiri wao... Lakini kinyume chake Padri akiwa altareni anatamka bila woga kwamba anaunga mkono mgomo wa madaktari, na pia anaiambia Serikali ijiandae kuondoka madarakani.
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mungi,

  Dr Martin Shao anasema madaktari wanapaswa kuzingatia wito wao kwa maana ya maisha kwanza, huku maslahi yao yatatuliwe kwa njia ya mazungumzo sio mgomo.
   
 18. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,800
  Likes Received: 17,886
  Trophy Points: 280
  Acha kuweweseka, changia Dr.Slaa atinge Ikulu 2015 ili haya mambo yapungue na then kuwa historia kabisa, pofu hili ungelitumia kumuomba J.Kikwete awe na huruma na wale anaowapeleka Mabwepande kuwa-ulimboka.
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kwani hujasikia kauli ya Slaa kuhusu mgogoro wa madaktari kuna thread humu JF itafute.
   
 20. B

  Baky New Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kurudi kwa madaktari kazini bila ya maelewano ya kweli na muajiri wake ni kazi bure. Sikuzote mtu hafanyikazi kwa lazima, ukimlazimisha akafanya kazi kwa woga, basi hiyo kazi haitakuwa naufanisi. Utapata mgomo baridi ambao ni mbaya zaidi. Angalia sekta nyingine kama Ualimu, Kilimo,Maji, Mahakama n.k hawagomi moja kwa moja huduma zake zikoje!
   
Loading...