Tunakumiss Kamoga, clouds 360

MANILABHONA

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
462
348
Ni ukweli usiopingika kwa wale wapenzi wa kipindi cha clouds 360 kwa muda sasa toka H Kamoga ateuliwe na magu kuwa mkurugenzi Mbulu, hajapatikana mbadala wake, kamoga alikuwa msikivu ana-argue kwa hoja, alikuwa anaongea kwa point, maneno machache yaliyojaa pointi.

Leo kuna mtu kaongezeka pale anaitwa H. Ngoma anaboa sijawahi ona, anaongea maneno mengi sana- pointi moja, kiukweli anapoteza muda mwingi sana wa kufanya mambo mengine ya msingi.

H.Ngoma amenifanya nipoteze mapenzi kwa kipindi hiki nilichokipenda sana. Sijui kama anajitambua kuwa anaongea sana halafu content ni kidogo mno. Naushauri uongozi wa CLOUDS MEDIA lifanyieni utafiti na mrekebishe vinginevyo mtapunguza wapenzi na matangazo ya biashara.

Kumbukeni enzi za Kamoga namna viongozi walivyokuwa wakiwapigia simu kuwapongeza.

Kumbukaa anayekukosoa anakujenga, Nikikaa kimya sikisaidii kipindi kipenzzi changu
 
Back
Top Bottom