Tunakumbushia na kufuatilia: Je, kuna mikakati gani ya uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Oktoba 2020?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Watanzania wenzangu hili swali si kwa ajili ya wanasiasa au wanaharakati pekee - ni swali linalopaswa kuelekezwa kwetu sote Watanzania tunaotamani demokrasia, haki na utawala bora virejee na kutamalaki katika jamii yetu.

Tusitegemee hata siku moja eti walio madarakani watakubali kirahisi uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, it's only natural.

Which means inahitaji watu wengine walio nje ya madaraka ndiyo waweke msukumo mkubwa katika hili. Hata kama wadau wa maendeleo wa nchi yetu wanaunga mkono uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, si wao wanaoweza kulianzisha - wao wanaweza tu kuwa chachu katika msukumo ambao wahusika (yaani sisi) watauanzisha wenyewe.

Natambua kipaumbele kwa sasa ni mapambano dhidi ya janga la korona, lakini hii haituzuii in the meantime kuwa na mikakati thabiti itakayopelekea uundwaji wa NEC huru.

Je, kuna mikakati yoyote? Imefikia wapi? Ni nini matarajio? Kama hakuna mikakati yoyote, uzi huu ni kwa ajili ya kutukumbukusha (wake up call) kuwa tunalo hili jukumu mbele yetu.

Wabilah Tawfiq
Bwana Yesu Asifiwe
Tumsifu Yesu Kristo

cc: Zitto, John Mnyika
 
Tume huru ya Uchaguzi

Hilo jina la taasisi linajitosheleza

Tunahitaji uhuru gani tena
 
Mikakati tulionayo sisi wana Chadema Asilia, Chadema Wakuja na Chadema Wafia Mbowe ni kuji-Lockdown hadi Uchaguzi Mkuu umalizike sababu Haķuna Tume Huru ya Uchaguzi.
 
M-mbabe,
Tume iliyopo na huru na ndio maana kuna wabunge wa upinzanj zaidi ya mia Bungeni. Au kuwa huru mpaka wapinzani washinde urais?
 
Back
Top Bottom