Tunakumbuka nini Tuliosoma Igowole, Mdabulo, JJ Mungai au Malangali tukutane hapa

INTROVERT MAN

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
993
1,337
Aisee mkoa wa Iringa kielimu nao si haba kwa nyanda za juu kusini
Miaka hyo ilianzishwa Mufindi Education Trust (MET) ambayo ilikuwa chini ya marehemu Mbunge na Waziri wa zamani wa Elimu JJ Mungai

So hizo shule zilikuwa chini ya MET kabla ya kubadilishwa mfumo na serikali.

Me binafsi nmesoma Igowole Secondary School chini ya headmaster KAUTA
Nilikaa bwenini kule chini. Bweni la wavulana tulikuwa tunaliita seed farm na limejitenga mbali sana shule ni kama tunajitegemea vile.

Kipindi cha msimu wa mahindi mabichi aisee tukiwadhulumu sana wanakijiji full kuiba aisee

Walimu adimu naowakumbuka ni Kauta ,Msumule, Mwalimu Sanga (tukikuwa tunamuita disease kisa alivofika alianza na topic fulani ya bios ilikuwa inaitwa disease basi likawa lake).

Mwalimu Makombe yule mwenye skafu kama waziri fulani wa mambo ya ndani aliyetimuliwa. HUYU Mwalimu alikuwa na mwandiko mzuri sana ila sasa toka nafika ile shule hadi naondoka alikuwa anatumia perfume moja tu.Alikuwa anakaa igowe kule juu ila pombe lazima aende mhamati.

Madam Mlasu huyu alikuwa kakariri wanafunzi shule nzima coz alikuwa mhasibu kiasi kwamba ukikutana njiani ukimuuliza anaweza kukuambia kiasi unachodaiwa

Mwalimu Mlembe a.k.a soja katulisha sana stick kiasi kwamba ukiwa na kosa hata uwe nunda unakiri

Kuhusu msosi ilikuwa ni noma kama si mbishi waweza miss ukashiba kwa kupewa mapafu tu

Kuhusu maji ilikiwa changamoto ila kisima cha kwa "mchepenge" kiliokoa sana roho zetu .

Wakumbuka bifu kati ya igowole na malangali kipindi cha umiseta wakati wa kambi pale igowole.

Maisha ya pale yalikuwa simple na kikubwa uhuru full kuzurura mhamati kula vitairi kwa mama kayuki And so on.

Maisha ya bweni ;ukiwa mwizi na ikathibitika ma bro walikuwa wanaagiza madogo walete kuni aka fimbo. Baada ya prepo kikao then unafunikwa blanket na taa kuzimwa hapo ni kupigwa mpk udate.

Nakumbuka bifu kati ya waschana wa O level na Advanced kisa wavulana wa O level coz Advanced ilikuwa single sex tu.

Karibu na wewe utukumbushe lolote ulipokiwa unasoma hizi shule Wilayani Mufindi

-all is well-
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🙌🙌🙌🙌! Nikikumbuka sakata la Mdabulo
secondary naishiaga kucheka sana!...madent mkachoma shule...! Hatarious !..umenikumbusha mbali sana ingawa sijasoma hizo shule!
Wapi Cagrielo😃😃😃!
 
Jamani anayejua mwalimu Mhema(Magulu pande) alipo ...! Huyu kwao ni Mufindi lakini alikua anafundisha Mwembetogwa...!
 
Back
Top Bottom