JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Salamu wanabodi!
Umasikini ni jambo baya sawsawa kabisa na kuwa mjinga. Tunaishi kwa matumaini kuwa labda kesho maisha yatakuwa mazuri! Dalili zinaonesha kuwa umasikini unazidi kuongezeka katika nyanja zote lakini bado makumi kwa maelfu ya watanzania wanaamini wamempata mtu wa kuwavusha kwenda Nchi yenye neema. Tunakula samaki kwa picha! Kwanini tumekuwa wajinga hivi?
Tumepoteza mwelekeo kabisa! Mwaka wa fedha 2016/2017 bajeti ya serikali ilikuwa Tshs Trilioni 29, bado miezi miwili tu mwaka wa fedha uishe, mpaka sasa serikali imeweza kukusanya shs trilioni 15 tu ! Trilioni 14 bado! Tulipanga bajeti kubwa sana hivyo ya nini?
Tulio wakabidhi Nchi wako busy kukomoa wapinzani na kulipa visasi kwa mahasimu wao.Halmashauri zipo hoi karibu kila eneo lakini wajinga mitaani wanaamini maendeleo yatakuja tu! Wanakula samaki kwa picha.
Tulio waamini wanahangaika na akina Kimei kwakuwa alisema ukweli kuwa uchumi umeyumba, sasa bila kujali mikataba waliyo ingia na serikali anaagiza fedora zote zipitie NMB tu kwasababu CRDB kwa maana ya Kimei walimuudhi kwa kusema ukweli.
Ushauri wangu ni kwamba serikali iachane na mambo yasiyo na tija, badala yake ijielekeze kujenga uchumi kwa kushirikiana na sekta binafsi. Watathimini kwanini walipanga bajeti isiyo tekelezeka? Warudishe vyanzo vya mapato vya halmashauri ili ziwaletee wananchi maendeleo.
Kukiri mapungufu siyo udhaifu! Rais hawezi kufanya kila kitu yeye mwenyewe. Ni lazima awaamini wasaidizi wake. Aheshimu uwepo wa Bunge na Mahakama. Aheshimu utawala wa sheria. Aishi kwa ahadi zake. Tunataka maendeleo siyo mbwembwe.