Tunajua juzi tu Rwanda iliadhimisha miaka 25 ya mauaji ya Kimbari

Nadhani atakuwepo maana hata majuzi marekani imesema ile $5mil kwa atakayefanikishwa kukamatwa kwa kabuga iko pale pale.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kumbe anasakwa hadi na USA basi kazi anayo?

Hivi na yeye yupo na drc na fdlr au yupo pengine?

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Yule atakua ana sponsor show maana mpunga anao mrefu tu,kama majengo anayomiliki huko Kenya tu yana thamani zaidi ya 1bil ya Kenya ingawa yalishataifishwa,kwa hela zetu za madafu ni more than 20b.

Atakua na FDLR yule,maana ni extremist si mchezo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu ni vizuri ujibu swali acha kuzunguka..... Narudia tena

Rwanda mlikuwa milion 6
Tutsi 14% na Hutu 84%

Vifo vinakadiriwa kufika million 1

Taasisi ya IBUKA inasema tutsi survivors ni laki 4

900,000 Tutsi - 400,000 Tutsi survivors= 500,000 Tutsi deaths

Sasa 1,000,000 Dead- 500,000 Tutsi dead= 500,000 Non-Tutsi Death

SWALI= Je ni kabila gani hili ambalo sio la watutsi ila wamekufa 500,000??

Ukijibu hili swali utakuwa umetusaidia wana JF wote.

Nijibu nini sasa bwana interahamwe,kwani kipindi kile wkt mnagawa ID huko kwenu Rwanda za kuonyesha huyu ni mhutu na huyu Mtutsi mkijiandaa na chinja chinja,Statistics zenu zilionyeshaje?

Pata ujumbe hapo chini.

Afisa wa zamani katika ngazi ya juu ya jeshi la Ufaransa, Jenerali Jean Varret, ametoa ushahidi mpya kuhusu msimamo wa Ufaransa wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani nchini Rwanda.

Mkuu huyo wa zamani wa ujumbe wa ushirikiano wa kijeshi wa Ufaransa nchini Rwanda amesema alipinga msaada wa Ufaransa kwa rais Habyarimana, bila mafanikio.

Kwa mujibu wa afisa huyo mwenye umri wa miaka 84, mkuu wa polisi ya Rwanda wakati huo, Kanali Pierre-Célestin Rwagafilita, alimwambia mnamo mwaka 1990 kwamba Watutsi walio wachache wanatakiwa "kuangamizwa".

Jenerali Jean Varret ametoa ushahidi huo kwa wenzetu wa redio France Inter na Médiapart. Ni karibu miaka 25 sasa baada ya mauaji hayo yaliyotokea nchini Rwanda, ambapo Jean Varret anaamua kuvunja ukimya na kusema yalityotokea huku akieleza jukumu la Ufaransa wakati wa maujai hayo.

Amerejelea hasa mazungumzo ya ana kwa ana kati yake na afisa wa polisi ya zamani ya Rwanda , Pierre-Célestin Rwagafilita: "Na hapo, aliniambia: 'Tunaongea ana kwa ana, sote hapa ni askari, tunapaswa kuweka mambo yote wazi.

Ninakuomba hizo silaha, kwa sababu nitashiriki na jeshi katika operesheni ya kuondoa njiani tatizo hilo'.

Niliposhangazwa na kauli hiyo, alisema: 'Tatizo hilo, ni rahisi sana. Ukweli ni kwamba Watutsi sio wengi, tutawaangamiza'. Alinambia wazi. "

Kwa upande wa Jenerali Varret, amesema mpango wa mauaji ya kimbari ulikuepo. Anasema pia kuwa alitoa taarifa hiyo kwa jeshi la Ufaransa, lakini viongozi hawakujibu: "Hakuna. Kwa sababu hawakutaka kuunga mkono mpango huo wa Habyarimana.

Kwa bahati mbaya, historia imethibitisha kwamba ilikuwa ni kosa, zaidi ya kosa, kwa sababu mauaji ya kimbari yalitokea bila hata hivyo kuzuia kabla hayajatokea wakati taarifa za mpango huo zilikuepo.

"Mwezi ujao, Rwanda inajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari. Rais wa Ufaransa amealikwa rasmi kwenye sherehe hizo. Elysee mpaka sasa, haijaweka wazi jibu lake. Emmanuel Macron alijibu tu kwamba Ufaransa itawakilishwa.

Source RFI

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nijibu nini sasa bwana interahamwe,kwani kipindi kile wkt mnagawa ID huko kwenu Rwanda za kuonyesha huyu ni mhutu na huyu Mtutsi mkijiandaa na chinja chinja,Statistics zenu zilionyeshaje?
ID zinaonyesha Tutsi mlikuwa 14% na hata UN report iliconfirm hilo so wabishie UN sio mimi;

Sasa ningependa ujibu je wale laki 5 waliokufa ambao sio watutsi walikuwa kabila gani?? Je siku yao huadhimishwa lini??

Naomba ujibu hoja tafadhali mipasho iweke pembeni
 
Mkuu mbona swali la zitoo Jr ni valid kabisa. Kama Ibuka wanasema idadi ya survivors ni laki nne na kwa mujibu wa report za Serikali waliokufa ni milioni moja, hao laki tano wengine ni kabila au jamii gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chief mimi nilianza discussion fresh kabisaa,yeye akajibu upuuzi sasa niko namjibu in accordance.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yule atakua ana sponsor show maana mpunga anao mrefu tu,kama majengo anayomiliki huko Kenya tu yana thamani zaidi ya 1bil ya Kenya ingawa yalishataifishwa,kwa hela zetu za madafu ni more than 20b.

Atakua na FDLR yule,maana ni extremist si mchezo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kawa kimya saana nadhani anasoma game au kaona now Rwanda pazito kaamua kuuchuna tu

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
ID zinaonyesha Tutsi mlikuwa 14% na hata UN report iliconfirm hilo so wabishie UN sio mimi;

Sasa ningependa ujibu je wale laki 5 waliokufa ambao sio watutsi walikuwa kabila gani?? Je siku yao huadhimishwa lini??

Naomba ujibu hoja tafadhali mipasho iweke pembeni

Hahahah nikubishie interahamwe ili nipate nini sasa?

Nikujibu wkt wewe ni bingwa wa kuharibu mjadala,ngoja mipasho ya namna mlivyokua mnaua iendelee hapo chini.

Huyo ni mbwa wenu mwingine aliyehukumiwa.

BAGOSORA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.

18.12.2008

Mahakama ya Umoja wa Mataifa leo imetoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa aliekuwa kanali wa jeshi la Rwanda Theoneste Bagosora baada kupatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya watu 800,000 nchini Rwanda mnamo mwaka 1994.

Mahakama maalumu ya kimataifa,ICTR ya mjini Arusha, Tanzania inayoshungulikia mauaji halaiki yaliyofanyika nchini Rwanda, ilimfungulia mashtaka Bagosora ya kuwa kiongozi wa vikosi vya jeshi na wa wanamgambo wa kihutu Interahamwe, waliowaangamiza watusi pamoja na wahutu waliokuwa na mtazamo wa ukadirifu.

Mahakama hiyo ilimtia hatiani Bagosora kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ,uhalifu dhidi ya ubinadamu na kwa kutenda uhalifu wa kivita.

Katika tamko la kumtia hatiani , Bagosora mwenye umri wa miaka 67, mahakama ya kimataifa ilisema kuwa kabla ya mauaji,Bagasora alisusia mazungumzo ya amani nchini Tanzania na kusema anarejea nyumbani " kutayarisha kihama".

Bagosora alikuwa mkurugenzi katika wizara ya ulinzi ya Rwanda wakati ndege ya aliekuwa rais wa nchi hiyo, Juvenal Habyarimana ilipotunguliwa.Kifo cha rais huyo ndicho kilichosababisha mauaji halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Mtu mwengine aliehukumiwa leo na mahakama ya kimataifa mjini Arsuha ni Protais Zigiranyirazo. Mfanyabiashara huyo ambae ni shemeji wa hayati Habyarimana amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwa mwanachama wa kundi la Akazu la watu waliokula njama za kuwaangamiza watusi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hana uwezo wa kujibu ndio maana kaishia mipasho tu.... Kaja hapa na data uchwara nimembana ajibu swali dogo tu la kutoa na kujumlisha ameanza mipasho tu.

Watutsi lazima waelewe dunia imebadilika huwezi danganya milele

Ni kweli dunia imebadilika sana sana ni muda wenu interahamwe mtoke huko msituni Kongo mnakobaka wakongo,mje muone ustaarabu wa duniani ukoje na muache kuteka magari/ma bus huko Kigoma na Kagera huko.

Ingawa ni ngumu nyinyi kuacha kusikia kiu ya damu maana mmezaliwa na hio kitu kwenye damu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hahahah nikubishie interahamwe ili nipate nini sasa?

Nikujibu wkt wewe ni bingwa wa kuharibu mjadala,ngoja mipasho ya namna mlivyokua mnaua iendelee hapo chini..

Sent from my iPhone using JamiiForums
Nilijua tu huna ubavu wa kujibu na hautowahi kuwa nao.... Kawadanganye illiterates wa huko kwenu sio sisi watanzania.

Mwanzoni nlidhani mtu makini kumbe mwana propaganda tu (Tutsi keyboard-extremist ) ndio maana umeacha kujibu facts unakimbilia mipasho.

Inyezi!!
 
Ni kweli dunia imebadilika sana sana ni muda wenu interahamwe mtoke huko msituni Kongo mnakobaka wakongo,mje muone ustaarabu wa duniani ukoje na muache kuteka magari/ma bus huko Kigoma na Kagera huko.

Ingawa ni ngumu nyinyi kuacha kusikia kiu ya damu maana mmezaliwa na hio kitu kwenye damu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Jibu hoja acha kulialia..... Kma huna hoja si uzime data ukalale sio lazima ucomment kitu usichokijua.

Shida yenu kila anayewapinga mnadhani ni mhutu.... Na hii shida itawatesa sana kwahiyo Katumba nyamwasa naye ni mhutu??

Kazi kwelikweli
 
Kawa kimya saana nadhani anasoma game au kaona now Rwanda pazito kaamua kuuchuna tu

Sent using my iPhone using jamiiforum app

Nadhani itakua hivyo boss,na umri pia umemtupa mkono kiaina hivi ana miaka 84 sasa.

Possibly anaomba amalize miaka yake duniani kabla hajakamatwa na mahakama au kama kawaida atakua ameshapata wakurithisha ideology zake za kuua kwa watoto wake au watu wengine so hata akifa mawazo yake yataendelea kuishi kwa watu wengine.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Jibu hoja acha kulialia..... Kma huna hoja si uzime data ukalale sio lazima ucomment kitu usichokijua.

Shida yenu kila anayewapinga mnadhani ni mhutu.... Na hii shida itawatesa sana kwahiyo Katumba nyamwasa naye ni mhutu??

Kazi kwelikweli

Ni kweli kabisa shida ya interahamwe kila wanayempinga wanajua ni mtusi.

Muache kulia lia nyie mnao ishi porini Kongo kama ngedere.

Hilo jina la 'katumba' Nyamwasa itakua ni jina uliombatiza mtoto wako.ila sijawahi kulisikia.

PATA UHONDP KAMILI.

UMEWAHI kujiuliza ni kwa namna gani makundi mbalimbali ya waasi huwa wanaishi wanapokuwa msituni wakiishi kusubiri kupindua serikali zilizo madarakani? Nimekuwa najiuliza swali hili kwa muda mrefu na majibu niliyapata nchini Rwanda hivi karibuni.

Nkomeje Jean Claude (36) mmoja wa waliokuwa waasi katika kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), alinipa sentensi moja tu (kwa Kiswahili chake chenye lafudhi ya Kicongo) iliyonipa majibu yote; "Mwenyewe yuko na bunduki halimagi (Mtu mwenye bunduki halimi)."

Kwa maelezo yake mwenyewe, bunduki ndiyo inakupa kila unachotaka. Ukisikia njaa unavamia kwa wananchi na kupora chakula chao. Ukihitaji nguo au viatu unavamia sokoni na bunduki yako na unateka vitu. Kila unachotaka unaweza kukipata kwa kutumia bunduki yako !

"Bunduki pia inakupa fursa ya kumnunulia zawadi mpenzi wako. " Kama akipita mwanamke amevaa vizuri na amependeza na nguo yake mpenzi wako alikuwa anaitaka kwa muda mrefu, unakwenda na kumvua yule mwanamke na kisha unampelekea zawadi mwanamke wako. Unatumia bunduki yako kupata kila unachotaka," anasema Nkomeje huku akitabasamu.

Nkomeje ni sehemu ya waliokuwa askari katika kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR ) ambao sasa wameamua kurejea nyumbani (Rwanda) kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako kundi hilo limeweka makazi yake ya kudumu.

FDLR ni kundi lililoundwa kutokana na mabaki ya waliokuwa askari katika Jeshi la Rwanda chini ya serikali ya hayati Rais Juvenal Habyarimana –wanaotumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 kabla ya mauaji hayo.

Mara baada ya majeshi ya Rwanda Patriotic Front (RPF) yaliyokuwa yakiongozwa na Jenerali Paul Kagame kutwaa madaraka, waasi hao walikimbilia nchini DRC ambako walitumia majina mbalimbali kabla ya jina la sasa la FDLR.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Rwanda, katika kipindi cha kati ya mwaka 1996 hadi mwaka huu, jumla ya askari 51,000 waliokuwa wakitumikia FDLR nchini DRC wamerejea kwao baada ya kukiri makosa waliyoyafanya na kukubali kujenga taifa jipya lisilo na ubaguzi.

"Baadhi ya waliokuwa waasi walijiunga na kundi hilo pasipo kujua nini haswa wanakipigania. Waliambiwa maneno ya uongo na kuyaamini. Ukiwauliza wanakwambia hawakujua chochote. Kazi yetu sasa ni kuwajenga kisaikolojia ili warejee uraiani na kuwa raia wema," anasema Frank Musonera, Mkuu wa kambi ya kuwapokea na kuwafundisha waasi hao wa zamani iliyopo wilayani Rubavu.

Nilifanikiwa kuhudhuria katika darasa la mafunzo ya waasi hao wa zamani na nilikuta wanafundishwa uzalendo, ujasiriamali na masuala mengine ya kujenga amani na mshikamano.

Waasi hao walikuwa wanaimba nyimbo za Kinyarwanda na mwenyeji wangu alinitafsiria kwamba nyingine zilikuwa zinahusu msamaha wanaoomba kwa Mungu na waliowakosea wakati walipokuwa wakiasi au wale walioua wakati wa mauaji ya kimbari.

"Nimeua watu wengi ingawa sikumbuki idadi. Unajua unapokuwa kwenye vita wewe unapiga tu risasi na hujui ya kwako imempiga nani na haikumpiga nani. Hata wakati ule tunakimbia kimbia kutoka Rwanda (mwaka 1995), nilikuwa naua tu mtu ninayekutana naye njiani na kumtilia mashaka. Lakini hayo yamepita na sasa niko tayari kujenga nchi yangu," anasema Nkomeje.

Kijana mwingine wa umri wa makamo, Ibrahim Bizihalimana, alinisisimsha kwa vile alinieleza namna alivyokimbia kutoka Rwanda na kujikuta yuko Kigoma, Tanzania.

Kwa maelezo yake, kuna wakati alikuja nchini ili asaidie kusafirisha madawa yaliyokuwa yakitumika kutibia waasi hao."Nilifurahia maisha ya Kigoma.

Pale tulikuwa na antena yetu (antenna kwa tafsiri yake inamaanisha mtawanyiko wa kundi kwa maana kwamba kama kuna masalia ya FDLR popote pale, wao wanaita kwa jina hilo). Niliishi vizuri na hakukuwa na shughuli za kijeshi. Ila tukitaka kusafirisha madawa tunayapokea na kuyasafirisha kupitia Ziwa Tanganyika," anasema kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Uso kwa uso na muuaji

Wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, mji mmoja kusini mwa Rwanda uitwao Murambi, ulijipatia sifa ya kipekee. Katika eneo ambalo ilijengwa Shule ya Ufundi, zaidi ya Watutsi na Wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani 45,000 waliuawa na kundi la Interahamwe lililokuwa likiungwa mkono na serikali ya Rwanda.

Mara baada ya ajali ya ndege iliyopoteza maisha ya Habyarimana mnamo Aprili 6 mwaka huo, Watutsi walianza kuhisi kwamba hatari inawasogelea maana propaganda za chuki kwamba wao ndiyo waliomuua rais huyo kutoka kabila la Wahutu, zilikuwa zimewajaza watu chuki.

Naambiwa wakaanza kukimbia majumbani mwao na kuelekea kwenye nyumba za ibada ili kuokoa maisha yao. Hata hivyo, viongozi wa serikali wa Wilaya ya Murambi waliwashauri kwamba ni vema wakakimbilia kwenye shule ya ufundi ya Murambi ambako ingekuwa rahisi kwao kupata huduma.

Inaelezwa takribani watu 60,000 walikuwa wamekwenda kujihifadhi kwenye shule hiyo. Ghafla, serikali ikakata huduma za maji na umeme. Wananchi wakaanza kushindwa kupika na kula. Wakadhoofika. Ilipofika Aprili 16, wananchi hao wakiwa wamedhoofu, Interahamwe wakavamia na kufanya mauaji hayo ya kutisha wakitumia bunduki, visu, mishale, mapanga, nyundo na marungu.

Nilipotembelea katika Makumbusho ya Murambi ambayo yamejengwa katika eneo hilo ambako zamani ilikuwapo shule, nilijionea jiografia ya mahali hapo. Japo na yenyewe ilikuwa iko juu kutoka usawa wa bahari, imezungukwa na vilima vingine pande zote. Ni wazi kwamba waliowashauri wananchi wakimbilie kule walikuwa wamewatafutia sehemu ambayo wangeweza kuwaona kwa urahisi na kuwazunguka pia.

Miili ya waliouawa, wengine walizikwa wakiwa hai, imehifadhiwa katika makumbusho hayo. Niliingia na kwenda kuiona na ingawa sasa yamebaki mafuvu na mifupa mitupu, harufu ya maiti bado inavuma na ilinichukua siku mbili kuacha kuihisi kwenye mikono na nguo niliyovaa. Ni kitu cha kusikitisha kuona maiti ya mtu anayezikwa akiwa hai, anakufa huku akiona kifo chake na mwili unapambana. Mifupa yake inaonyesha namna alivyokufa akiogopa kifo chake.

Nilipotoka nje ya makumbusho hayo, nakutana na Nyirimbuga Emmanuel (52), mmoja wa watu waliofanya mauaji hayo lakini sasa wamekiri makosa yao, wametumikia adhabu zao na sasa wanaishi katika jamii hizohizo walizoziletea maafa makubwa.

"Wakati wa mauaji yale nilikuwa nikiishi kwenye nyumba ile (ananionyesha nyumba moja iliyojengwa juu ya miongoni mwa vilima vinavyoizunguka shule ya Murambi). Wale waliokimbilia hapa nilikuwa nikiwaona kila siku wakiongezeka. Viongozi wetu wa serikali, redio na magazeti walikuwa wakitufundisha kwamba wakati wa kuwamaliza Watutsi umefika," anasema Nyirimbuga kwa Kinyarwanda ambacho nilitafsiriwa na mwenyeji wangu.

"Kwa kweli nakumbuka kuua watu kama saba hivi. Ila ninakumbuka zaidi watu watano kwa vile walikuwa ni watu niliowafahamu vizuri. Walikuwa ni jirani zangu na kuna mmoja wakati namuua aliniuliza kwanini unaniua? Wakati huo sikujali nafanya nini maana propaganda ya chuki ilikuwa imenijaa.

"Kuna mtoto nilimuua kwa kumpiga rungu. Kuna watu wazima niliwaua kwa kutumia panga. Nilitumia silaha za jadi maana zilikuwa zikigawiwa na viongozi wetu kwa kila aliyetaka. Sikuchagua nani wa kumuua, mradi nilijua huyo mtu ana sifa za Watutsi mimi nilikuwa naua tu.

"Mara tukasikia kwamba RPF wameshinda vita na sisi tulioua tunatafutwa sana ili nasi watuue. Nikaanza kukimbia. Huko njiani ukiona mtu anakuhisi au vipi unaua. Sasa sijui nao walikuwa wanakufa au wanapona lakini la msingi nilikuwa nadhuru.

"Kwanza nilikimbilia DRC kujiunga na waliokuwa waasi. Hata hivyo, baadaye nikabaini kwamba Wakongomani walikuwa hawatupendi sana na maisha yalikuwa magumu. Baadaye nikaenda kutafuta maisha Angola lakini askari wa kule hawakunipenda. Nikaondoka tena.

"Lakini, wakati ule wa mauaji nilikuwa na mke na watoto wanne na nilipoondoka sikujua wanaendeleaje. Hata hivyo, nilipokwenda ugenini na kuanza kutafakari kuhusu maisha yangu, nikaanza kuona dhambi niliyoitenda. Nikasema nitarudi nyumbani (Rwanda) nikatubu.

"Wakati ule kulikuwa na maneno mengi kuhusu sisi tulioua. Wenzangu ambao tulishiriki pamoja kuua walikuwa wakiniambia nisirudi nyumbani. Hata hivyo, kila nilipokimbia niliona kama nakimbia dhambi niliyoifanya. Nikasema afadhali nirudi nyumbani ili hata nikiuawa, nife nikiwa na amani moyoni.

"Ndipo nikarudi na kutubu makosa yangu. Sikuuawa. Nimeamua kusema yote haya ili niwe na amani moyoni mwangu. Kuna watoto zangu hawazungumzi nami. Mke wangu pia kanitoroka. Naishi mwenyewe tu lakini nina amani.

"Nikipita njiani watu wananionyeshea vidole kwamba Yule ndiyo muuaji aliyeua watoto wetu, ndugu na jamaa zetu. Lakini nimeamua kuishi hivyo. Hata hivyo, nahisi nina amani moyoni kuliko wale walioamua kukimbia maisha yao yote. Angalau mimi nitazikwa nyumbani kwangu nitakapokufa. Kuna wakati unatamani kufa ili yote haya yaishe lakini nina misheni kwenye maisha yangu na nitaitekeleza," anasema Nyirimbuga.

Shati alilovaa limechakaa. Suruali yake pia na viatu vyake vinaonyesha kwamba ni mtu anayeishi kwenye mazingira magumu. Hata uso wake umepoteza mng'aro na anaonekana mkubwa kuliko umri wake wa miaka 52. Lakini angalau Nyirimbuga atakufa akiwa na amani moyoni mwake. Nilimuaga nikimwita shujaa kwa maana anachokifanya ni kitu kigumu sana.

Ana kwa Ana na Bwana wa Vita

Kwa wafuatiliaji wa siasa za Afrika Magharibi, watakuwa wanafahamu kitu kuhusu vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyochakaza nchi za Sierra Leone na Liberia kwenye miaka ya 1999. Katika vita hiyo, maelfu ya watu waliuawa, kuporwa mali zao na kufanywa walemavu wa kudumu.

Kwa kiasi kikubwa, vita hiyo ilichochewa sana na biashara mbili kubwa; ya almasi na ya silaha. Kwamba wafanyabiashara wa silaha walikuwa wakiuza bidhaa hiyo kwa kubadilishana na almasi. Ni vita hiyo ndiyo ambayo ilikuja baadaye kutoa filamu ya Blood Diamonds na ile documentary maarufu ya War Don Don iliyotayarishwa na mwanamama Rebecca Richmann Cohen.

Nilipokwenda nchini Rwanda, nilifanikiwa kutembelea Gereza Kuu la Nyanza lililopo katika wilaya ya Nyanza. Lengo lilikuwa kuangalia namna tu wafungwa wa nchi hiyo wanavyoishi na kuendesha maisha yao.

Kwa bahati tu nikaambiwa kuna wafungwa kutoka Sierra Leone ambao wamo ndani ya gereza hilo. Nikaomba kwenda kuwasalimia na nilipofika, hamad !- Nikakutana na mtu ambaye nimemsoma kwenye vitabu na kumwona kwenye documentary. Anaitwa Issa Hassan Sesay.

Mwaka 2009, Sessay alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa Kuhusu Sierra Leone kwenda jela kwa muda wa miaka 52 kutokana na maovu aliyoyafanya wakati wa vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe. Sesay alikutwa na hatia ya makosa 16 kati ya 18 aliyotuhumiwa kuwa nayo. Baadhi ya makosa yake yalikuwa ni mauaji, ubakaji, kukata watu viungo vya mwili, utesaji, uporaji wa mali, uingizaji watoto jeshini na mambo mengine chungu nzima. Hakuna uovu wa kivita ambao hakushitakiwa kwayo.

Sesay ambaye ndiyo kwanza ana umri wa miaka 43 sasa, alipewa cheo cha Jenerali na kundi la waasi la United Revolutionary Front (RUF) wakati akiwa na umri wa miaka 30 tu. Nilimkuta kwenye chumba chake akiwa anasoma biblia. Amevaa tisheti yenye jezi kama za timu ya Arsenal ya England na mezani akiwa na picha za mchezaji Cristiano Ronaldo.

Nilimuuliza Issa Hassan Sesay, akanijibu mimi ndiye. Kwa sadfa tu (nikiazima neno la mwandishi nguli, Ahmed Rajab, kumaanisha neno coincidence-sadfa), wakati nakwenda Rwanda nilikuwa nasoma kitabu cha mwandishi wa Afrika Kusini, Andrew Feinstein kiitwacho The Shadow World: Inside the Global Arms Trade, ambacho kimeeleza mengi kuhusu Sierra Leone na hivyo picha nzima ya matukio ilikuwa kichwani kwangu.

Nilipojitambulisha kwake kama Mtanzania, Sesay alitabasamu na akaniambia anafahamu Tanzania ina chuo kizuri cha kijeshi ambapo baadhi ya maofisa wa kijeshi wa taifa lake walikuwa wakija kupata mafunzo.

"Mna chuo kizuri (Tanzania Military Academy-TMA). Askari waliokuwa wametoka kufundishwa Arusha walikuja kuwa askari wazuri sana. Mimi sikupitia lakini kwetu kule tunafahamu kwamba askari aliyepitia Tanzania ni mzuri," ananiambia.
Nilimuuliza kama anajutia alichokifanya wakati wa vita ile ya wenyewe kwa wenyewe na jibu lake lilikuwa fupi; "Its war, my friend…. You either Kill or be Killed." (Ni Vita, Rafiki Yangu, Ama unaua wewe au unauawa."

Miongoni mwa ukatili mkubwa kuwahi kufanywa katika vita ya Sierra Leone ilikuwa ni ile iliyoitwa Operation No Living Thing ambapo maelfu ya watu walikatwa mikono na miguu, kuuawa na kuchomewa mali zao.

Nilimuuliza Sesay nini ilikuwa dhamira ya ukatili wa namna ile; "Kile kinachoitwa Operation No Living Thing kilitengenezwa na vyombo vya habari vya Magharibi. Hakukuwa na operesheni kama hiyo na unajua wazungu wanapenda tu kutengeneza maneno ambayo wakati mwingine hayapo.

"Nakubali kwamba nimeua watu. Tena nimeua watu wengi sana. Sikuzaliwa ili niwe muuaji. Mfumo ulionikuza ndiyo ulionifanya baadaye niwe nilivyo. Kama mfumo ungekuwa mzuri au usingetengeneza mazingira haya, leo tungekuwa tunazungumza mengine," anasema.

Ushauri wowote kwa Watanzania? Sesay anaasa umakini wa hali ya juu kwenye kuangalia rasilimali za taifa. Kilichowaponza Sierra Leone, ananiambia bwana huyu wa vita ni utajiri wake wa almasi na kama Tanzania ina utajiri wowote ule, basi ijitazame.

Watoto hawa masikini

Ukienda nchini Rwanda na hatimaye ukafika jijini Kigali, nakushauri ukatetembelee Makumbusho ya Gisozi. Hapo ndiyo utaona ni kwa vipi mwanadamu anaweza kugeuka kuwa mnyama mkatili kuliko wanyama wenyewe.

Utaona sura ya mtoto mzuri wa kike, Fidele Ingabire aliyekuwa na umri wa miaka tisa lakini akauawa kwa kupigwa risasi ya kichwa na wauaji wakati wa mauaji ya kimbari. Kuna mwingine aliyekuwa na umri wa miaka nane tu, Chanelle Ruterana, ambaye alikatwakatwa mapanga hadi kufa.

Wapo watoto wengine wadogo zaidi kama Honore Gatera waliouawa kwa kupigwa marungu. Katika sehemu zote ambazo nilitembelea na kuona unyama wa wanadamu, hakuna nilipoumia kama Gisozi. Wakati mtu anapochochea vita au ubaguzi wa namna yoyote ile, ni vema kwanza akakumbuka watoto wake na madhila watakayoyapata.

Wakati nilipozungumza na Sesay alikuwa ametoka kula wali na nyama. Wakati nazungumza na Nyirimbuga alikuwa akinywa maji. Wanavyokula hao watu na wanavyokunywa ndivyo hivyohivyo ambavyo Watanzania wanavitumia.

Rwanda, Sierra Leone na kwingineko hawakupigana kwa sababu wako tofauti na sisi. Walipigana kwa sababu mfumo ulilea mazingira hatarishi. Kama alivyopata kuniambia Sesay, hakuzaliwa muuaji lakini mazingira yalimtengeza akawa alivyo sasa.
Tutazame kauli zetu. Tutazame matendo yetu. Tuangalie kalamu zetu. Isifike wakati tukaanza kuabudu bunduki na mapanga ili tusiende shambani kulima au maofisini kufanya kazi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Daaah nine yajua mengi aisee

Sent using Jamii Forums mobile app

Endelea kusoma na hii,uzidi kuyajua mengi mkuu.

Hahah interahamwe imeshakua inajiita 'sisi watanzania',hahah.

Tulia wewe member wa Akazu au umemisi mlivyokua mnakagua ID za watu mnawaweka pembeni then mnapiga rungu la kichwa/panga/shoka mchezo umeisha.

Interahamwe bwana,we rudi porini tu mjini huku hapakufai.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom