Tunajifunza nini toka Uganda kuhusu rushwa ya CHOGM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajifunza nini toka Uganda kuhusu rushwa ya CHOGM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIGENE, Oct 13, 2011.

 1. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Hivi majuzi aliyekuwa makamu wa rais wa Uganda Prof Gilbert Bukenya alifutiwa dhamana yake nakuswekwa rumande katika gereza kuu la Luzira.

  Baada yakujivua nyazifa zao jana leo hii mwanasheria na mwanasiasa maarufu swaiba wa Yoweri Museveni Sam Kutesa mbunge na waziri wa mambo ya nchi za nje tangu 2005 amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya makosa yanayohusiana na rushwa akiwa na waziri wa nchi wa kazi Mwesigwa Rukutane na Eng John Nasasira Kiongozi wa shughuri za serikali bungeni (Goverment chief whip)

  Wote wanatuhumiwa kwa ufisadi matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya UShs 14 millioni wakati wa kipindi cha mkutano wa Jumuhia ya Madola uliofanyika mwaka 2007 Kampala kwa kile kinachojulikana kama kashfa ya CHOGM

  Wanajamvi somo gani tunalipata toka kwa majirani zetu?
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Boshen hiyo. nilikuwa kampala wakati wa maandalizi ya huo mkutano. Museveni aliweka
  katika kila idara ya maandalizi watu wake wa karibu na family members wake na hata
  tenda zilitolewa kwa watu wanaomzunguka. waganda wote wanaelewa hilo.

  Kwa kifupi ni kwamba hizo sarakasi za Uganda hazina tofauti na za hapa nyumbani
  ambapo Majambazi wetu wote serikali inawafahamu ila inatufanyia usaniii wa kufungua
  kesi za kijinga jinga na kushitaki very irrelevant people ambao mwisho wa siku
  ni lazima watashinda kesi sababu ya kukosekana direct evidences.

  Na mwisho ni kwamba, hili na zao la safari ya Museni to Magogoni kimya kimya
  ambayo hakuna records za mazunguzo yao mpaka sasa.

  Uko Kampala watu wote walikuwa wanajua kwamba hiyo safari lazima itaibuka
  na mazingaombwe, wao walitegemea ingeibuka na mikakati hewa ya kujenga
  reli from tanga to anywhere in kampala lakini kumbe poor Tanzania imeingineer
  agenda ya kuwapumbaza Waganda kwenye Vita dhidi ya Ufisadi.
   
Loading...