Tunajifunza nini kwenye milipuko ya gongo la mboto? Gharama ya kuhifadhi amani ni kub | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajifunza nini kwenye milipuko ya gongo la mboto? Gharama ya kuhifadhi amani ni kub

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kim, Feb 18, 2011.

 1. Kim

  Kim Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2006
  Messages: 17
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  Wahenga wanasema: Kama hujui kufa, angalia kaburi. Ukiangalia hali ya maisha ya Dar es Salaam na hasa wakazi wa Gongo la Mboto na vitongoji vyake katika saa 24 zilizopita, unapata picha halisi ya gharama za uvunjifu wa amani na ama kutokuwa na amani kabisa katika jamii. Huu mstuko wa saa 24 zilizopita unatupatia picha halisi ya maisha wanayoishi wenzetu huko Somalia, Mashariki ya DRC, waliishi hivyo Rwanda, Burundi, Sierra Leone, Iraq, Afghanstan na maeneo mengine yenye vurugu na ambapo msamiati wa amani umekuwa hauna maana kwao.

  Kwa taarifa tu ni kwamba binafsi nimewahi kuwa muhanga wa kutokuwepo na amani hapa Tanzania hasa wakati ule wa vita ya 1978-9 nikiwa mdogo kabisa, nakumbuka kumwona mama amefunga kifurushi cha viguo vyetu pale nyumbani ambacho tulikiacha pale baada ya mtikisiko wa bomu kusababisha ufa kwenye jiko letu usiku tukiwa tunajiandaa kwa mlo wa usiku. Ninakumbuka kuwaona wakimbizi wengi wamehifadhiwa kwenye shule ya msingi Nyaishozi, jirani na nyumbani na mashule yote yalifungwa wakati huo. Lakini kama vile haitoshi wananchi waliikimbia mashine ya kuvuna ngano (combined harvester) ilipokuwa ikipita tokea mashamba ya ngano ya Kibale mpakani na Uganda wakidhania kuwa ni vifaru vya Uganda!

  Pia mimi niliponea kuwa muhanga wa vita ya Rwanda ya 1994 baada ya kutekwa na kundi la watu wanyarwanda Wahutu kwenye kambi ya wakimbizi Benaco, Ngara mnamo December 1994 baada ya watu hao kunituhumu kuwa nilikuwa miongoni mwa maaskari wa RPF waliovamia katika eneo lao ndani ya Rwanda wakati wa vurugu hizo, kwa bahati nzuri niliokolewa na askari wa usalama wa Tanzania waliokuwepo katika eneo lile lakini baada ya juhudi binafsi kujinasua kwenye mapanga na vijembe vikali hali iliyopelekea kukamatwa kwa baadhi yao. Mwezi mmoja baadaye,nikiwa nimeajiriwa katika shirika moja la kigeni kama msimamizi wa kituo cha kutoa msaada kwa wakimbizi, gari letu lilitegwa bomu la kutupwa kwa mkono (gruneti), siku hiyo niliacha kazi kirasmi kwenye shirika hilo kwa kuhofia usalama wangu. Yako mengi niliyoyashuhudia katika kipindi hicho ambayo kimsingi hapa si mahala pake ila nilitaka nijenge taswira halisi ya maisha bila kuwepo hali ya amani.

  Kwa hayo ya juzi jana na hali ilivyo leo, tunaona umuhimu wa kuitunza amani iliyokuwepo, na tukiruhusu siku moja iondoke, kuirudisha itakuwa ngumu sana. Nilikuwa nikiwatazama watanzania wenzangu kwenye runinga jana, wanavyohangaika, wamepoteza matumaini, wamepoteza mali, ndugu kwa maana ya familia, majirani na wapendwa wao, majeruhi kwa ujumla inatia uchungu sana hasa pale mtu anapokuwa mkimbizi ama muhanga wa matukio ya ndani ya nchi yake.

  Kwa ufupi haya ndiyo maisha ambayo wameishi wenzetu kwa miongo kadhaa baada ya amani kutoweka katika jamii yao. Ni picha ambayo hakuna mtanzania angependa aione katika uhalisia wake. Majeraha haya bado yanaonekana Kenya ambako amani liwahi kupotea tu katika muda mfuoi sana usiozidi wiki mbili baada ya matokeo tete ya uchaguzi.. bado wanauguza majeraha hadi leo!

  Lakini swali kubwa la msingi hapa ambalo tunajiuliza ni je, kuna dalili zozote ama viashiria vinavyoashiria kuwa kuna uwezekano wa kutufikisha hapa ambako tumefikishwa na mabomu ya Gongo la Mboto? Nina maana kuwa kuna jitihada zozote za makusudi zinazochukuliwa ili kuimarisha ustawi katika jamii yetu ya kitanzania kiasi kwamba wananchi hawawezi kupoteza imani na serikali yao? Maisha yanazidi kuwa Magumu, bei za bidhaa (consumables) zinapanda wakati mapato yanashuka, na uwezo wa kawaida wa wananchi kununua mahitaji na huduma unazidi kupungua; na umasikini unaongezeka kwa kasi kubwa.

  Kwa maoni yangu ni kwamba tayari picha ya kutokuwa na amani ambayo inaweza kufikiwa kama kutakuwepo na uwajibikaji mzuri wa kila mtu mahali pake na hasa wale waliokabidhiwa dhamana ya uongozi tayari inaonekana..ndiyo hii ya juzi jana na leo Dar es salaam. Hii inaweza kufikiwa wakati wowote pale tu ambapo wananchi watakuwa wamefikia mwisho wa uvumilivu wa kutokuwa na imani na serikali yao, japo hali hii haimaanishi kuwa ikitokea ndio ustawi unakuwepo, ndiyo inawezekana ustawi ukarejea lakini baada ya gharama kubwa ya maisha na mali (kama ilivyotokea Uganda miaka ya 1970 na 80) na ama isitokee kabisa kama ilivyo Somalia hivi sasa.

  Kwa hiyo kila mtu kwa nafasi yake mahala pake analo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa ustawi unakuwepo lakini pia misingi ya ustawi ijengwe kwa uwepo wa ukweli na uwazi katika masuala mbali mbali ya kijamii; matumizi sahihi na sawa (linganifu) ya raslimali zetu, kero za maisha ya jamii zishughulikiwe na zitatuliwe kwa wakati na kuepuka matendo yoyote ama mazingira yanayoweza kusababisha chuki kwa wananchi dhidi ya mifumo ya kiutawala iliyopo, kimsingi kuwepo na utawala bora, wa kisheria na kiuadilifu ambapo kila mtu anaweza kushiriki kwa vitendo ama mawazo bila kubugudhiwa; lakini pia wananchi wapewe majibu ya masuala mbali mbali pale yanapojitokeza.

  Naamini kuwa hali hii tumeishuhudia na zitafanyika juhudi za kimakusudi kuhakikisha kuwa hayajengeki mazingira yanayoweza kuhatarisha amani iliyopo na kututumbukiza katika picha hii ya juzi, jana na leo Dar es Salaam;na kwamba kila mmoja kwa nafasi yake na hasa zaidi kwa wale wenye dhamana ya kutuongoza wanafanya mambo sahihi kwa njia sahihi na wakati sahihi ili kurudisha imani ambayo kuna kila dalili kuwa inaweza kupotea kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.

  [​IMG]MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA[​IMG]
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  tunachoweza kujifunza ni kwamba tanzania ni mahali pekee uhai wa watu wake si wa muhimu labda wa mafisadi tu pia ni mahali pekee mambo ya hatari kama mabomu yanaifadhiwa kiholela pasipo tahadhari mana uhai si kitu cha thamani
   
 3. E

  Ebony Guest

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined:
  Messages: 0
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja...Maelezo yako ni mareeeeefu na yanachosha kabisa kusoma! La msingi kwa wewe kuelewa ni kwamba HAKUNA GHARAMA YOYOTE KATIKA KUILINDA AMANI! KINACHOTAKIWA NI KWA SERIKALI KUJALI NA KUBORESHA ULINZI NA USALAMA WA RAIA(KITU AMBACHO SERIKALI HII IMEDHIHIRISHA KUSHINDWA KUFANYA!) Mengine hapo ni tunzi binafsi, porojo na vitisho tu kwa wapenda maendeleo ya kweli!
  Either wewe ni mdini au mwanasiasa!
   
Loading...