Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Wote ni mashahidi kwa yanayotokea nchini Marekani hivi sasa kwa Bunge la nchi hiyo kuanza mchakato wa kumfungulia mashtaka Rais wa nchi hiyo kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Kwa kifupi katika kuelezea kuhusu sakata hilo ni kuwa inadaiwa kuwa Rais Trump alitumia vibaya madaraka yake kwa kumpigia simu kiongozi wa nchi ya Ukraine mwezi July mwaka huu, ili amchunguze kiongozi mwenzake Joe Baden, katika biashara zake anazofanya nchini huko, ili ibainike kama rushwa imetumika.
Madhumiuni yake makubwa yakiwa ni kumkomoa na kumdhalilisha mgombea huyo wa chama cha Democrats, ambaye ameonyesha kuwa atakuwa tishio kwake katika uchaguzi ujao wa Urais nchini Marekani.
Ndipo hapo ninapojiuliza kama nchi tunapata somo gani katika sakata hilo la kumchunguza Rais aliyeko madarakani, tena uchunguzi huo ukirushwa Live na vituo kadhaa vya lunimga nchini humo kikiwemo kituo maarufu kabisa duniani cha CNN?
Najaribu kujiuliza hivi Rais wetu, ameshavunja Katiba ya nchi yetu Mara ngapi?
Hivi alipopiga marufuku vyama vya siasa vya upinzani visifanye mikutano yoyote ya kisiasa hapa nchini hadi mwaka 2020, wakati yeye na chama chake cha CCM kila kukicha tunawaona nchi nzima wakizunguka na kufanya kampeni, je hajavunja Katiba ya nchi??
Tujiulize hivi hili sakata la uchaguzi wa serikali za mitaa jinsi ulivyovurugwa na hao wasimamizi wa uchaguzi, kwa kuwapendelea waziwazi wagombea wa chama tawala cha CCM na kuwaonea wagombea wa vyama vya upinzani, hivi kwa kufanya hivyo Rais wetu, hajavunja Katiba kweli?
Kama Rais kabla hajaingia madarakani anaapa kulinda na kuitii Katiba ya nchi ni kwanini basi yeye aachiwe aisigine Katiba ya nchi yetu atakavyo?
Je, Bunge letu halijayaona hayo?
Ni kwanini basi Bunge letu halianzishi mchakato wa "impeachment" kwa Rais wa nchi hii?
Naomba tuchangie kwa staha, mada hiyo muhimu sana kwa mustakabali wa Taifa letu, bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa.