Tunajifunza nini kwa CCM kutimiza miaka 33

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Hivi ni kweli malengo ya CCM ya 1977 na ya leo bado yale yale?

Makamu wa M/kiti wa CCM(Zanzibar) ambaye pia ni rais wa Zanzibar Ndugu Amani Karume jana akiwa Bagamoyo amefungua rasmi maadhimisho ya miaka 33 ya kuzaliwa kwa CCM amesema CCM ni imara na moja CCM ni kama mwalimu wa vyama vyote vya siasa.

Aidha amesema azma ya CCM ni kuendeleza mazuri yote ya TANU na ASP na kuyaacha mabaya pamoja naKuendelea kuimarisha uhuru wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha Mapinduzi ya ZanzibarKuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifaKuendelea kupanua na kuimarisha demokrasia ndani ya Chama chini ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya demokrasia Zanzibar.

Aidha CCM inaendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mfumo wa vyama vingi hauwi sababu ya chuki na msambaratiko wa umoja wa kitaifa, amani na mshikamano. Katika msimamo huo CCM imeweza kufikia MUAFAKA na CUF, hatua ambayo imetoa fursa kwa Zanzibar kurejesha hali ya amani, utulivu na mashirikiano, hivyo kuweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Lakini hakusita vile vile kuweka kijembe kuwa si lazima kila mtu awe kiongozi unaweza kutaka kuwa kiongozi na usichaguliwe nafikri alikwa akiwaeleza wale wanaonyemelea kiti cha urais Zanzibar baada ya yeye kumaliza kipindi chake cha pili hasa Ghalib Bilal aliyeuwania mara mbili na kuukosa

Akizunguza katika mkutano huo Katibu mkuu wa CCM Yusufu Makamba amerudia usemi wake kuwa wanaompinga rais Kikwete ni wehu kwa vile Kikwete ni zaidi ya chama na yuko tayari kupelekwa Mahakamani kwa kauli yake hiyo.

Naye makamu mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa akihutubia wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini Dodoma alimesema kuwa yeye ndiye aliyemuandaa Rais Jakaya Kikwete tangu akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa kijana mdogo na kuwa alikuwa mwanachama mwaminifu tangu wakati akiwa kijana mdogo , Msekwa alisema CCM kinawaandalia wasomi hao mazingira ya kuundiwa mkoa wao wa kichama.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).

Katika Mkutano Mkuu wa Pamoja wa TANU na ASP uliofanyika tarehe 22 Septemba, 1975 Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba Tanzania ni nchi yenye Chama kimoja;

Mwalimu alipendekeza kuunganishwa kwa TANU na ASP na kuundwa kwa chama kipya. Pendekezo hilo liliwasilishwa kwa wanachama wa TANU na ASP zaidi ya asilimia 90 ya wanachama walikubaliana na pendekezo la Mwalimu Nyerere. Tume ya watu 20 ilipewa jukumu la kutayarisha Katiba ya Chama kipya. Mwenyekiti wa Tume hiyo alikuwa Sheikh Thabit Kombo na Katibu wake alikuwa Ndugu Pius Msekwa.
Wajumbe wa Tume ya Watu 20 ya kuandaa Katiba ya CCM:-

Kutoka TANU:
1. Ndugu Peter A. Kisumo 2. Ndugu Pius Msekwa 3. Ndugu Daudi N. Mwakawago 4. Ndugu Kingunge Ngombale-Mwiru 5. Ndugu Jackson Kaaya 6. Ndugu Peter S.Siyovelwa
7. Ndugu Nicodemus M. Banduka 8. Ndugu Lawi N. Sijaona 9. Ndugu Beatrice P. hango
10. Ndugu Basheikh A. Mikidadi

Kutoka ASP:
1. Sheikh Thabiti Kombo 2. Ndugu Ali Mzee 3. Ndugu A.S. Natepe 4. Ndugu Seif Bakari 5. Ndugu Hamisi Hemed 6. Ndugu Rajab Kheri 7. Ndugu Asia Amour 8. Ndugu Hassan N. Moyo 9. Ndugu Juma Salum 10. Ndugu Hamdan Muhiddin

Tunajifunza nini kutokana na historia ya TANU na ASP na baadaye CCM
inayotimiza umri wa mtu mzima sasa?

Source: Magazeti ya Mwananchi Habari Leo Majira Tovuti mbalimbali na mimi
mwenyewe
 
CCM si chama kibaya. Ila viongozi wao wa miaka hii, si wabunifu. Wanafikiri chama kitaendelea kushika hatamu. Wanashindwa kudadisi; vi wapi vyama vilivytawala Kenya, Zambia, Malawi na Uganda.
 
Chukua Chako Mapema.Angalia watoto wa ;
1.Mwinyi
2.Mkapa
3.Msekwa
4.Malecela

Huwezi kuwalinganisha na watoto wa kawaida Tanzania hata siku moja.
Watatesa mpaka vijukuu vyao.
Ndio hawa wanasema Kidumu Cha Mapinduzi.
 
Tunajifunza kuiba. Kwani CCM ndio imejenga dhana ya mtu mwizi ndio mjanja. Ndio maana ukiangalia tabia za wabongo wengi zimekaa kiwiziwizi. Mtu anapewa kazi, kabla ya kuanza anajiuliza ati hii kazi ina madili gani?! Mwizi mtarajiwa! Wengi wa watz ipo hivyo sasa. Urithi wa CCM huo, na ndio somo la kujifunza.
 
Kuhusu kujifunza; hakuna kizuri cha kujifunza kwa sasa.
Vibaya ni:-
wizi, ufedhuli, uhuni, umalaya, ufisadi, kuoneana haya, kukosa huruma, ubinafsi, uongo, kukosa haya ktk mambo yoote ya kifedhuli, uonevu, udanganyifu na.................
 

Wanajamii; tarehe 31 Januari 2010 nilikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Viongozi wa CHADEMA Jimbo la Ubungo kuhusu Uendeshaji wa chama na maandalizi ya uchaguzi mkuu 2010.

Katika hotuba yangu ya ufunguzi nilieleza mambo ambayo ni kipaumbele katika kushamiri kwa chama cha siasa na kushinda kwa wagombea wake.

Pia Nikatoa mwito kwa wananchi kwamba uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa upande wa Dar es salaam, na kutangaza tarehe husika kwa upande wa Dar es salaam.

Kadhalika nilitoa changamoto kwamba katika mazingira ya leo ambapo chama kilichopo madarakani kinaendesha siasa za rushwa na vurugu kikitumia pia vyombo vya dola na watumishi wa umma ni muhimu kujipanga kuunganisha nguvu ya umma kukabiliana na hujuma ikiwemo kuzuia uwizi wa kura.

Kwa upande nilitoa angalizo kwa umma kuhususiana na maadhimisho ya miaka 33 ya CCM ambayo chama hicho kimeamua kuyafanya kwa wiki nzima. Ni vizuri watanzania wakaendelea kufunguka macho na kutambua unafiki huu wa CCM na viongozi wake ambao wameamua kutumia maadhimisho hayo kufanya propaganda za kurejesha imani kwa wananchi kwa kuwa mwaka huu ni kipindi ambacho tunaelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kuliko kufanya propaganda zinazohusisha matumizi ya anasa ikiwemo ya fedha za umma zaidi ya bilioni mbili (milioni zaidi ya 2000) ambazo chama hicho kinachukua kila mwezi kutoka serikali zizotokana na kodi yako na yangu badala ya kuendelea kufanya ubadhirifu wapeleke fedha hizo kuwahudumia watanzania wenzetu walioathirika na maafuriko huko Kilosa. Katika hotuba hiyo nimeeleza changamoto za msingi ambazo CCM imeshindwa kukabiliana nazo hususani katika Halmashauri ya Kinondoni kero ambazo zinawaondolea uhalali wa kusherehekea.

Nilitoa maoni yangu suala moja ambalo linaendelea kujadiliwa sasa kutokana na mkutano ulioitishwa na SUMATRA kupata maoni ya wadau kuhusu utoaji wa huduma ya usafiri mijini kwa kutumia makampuni na mashirika ambao kwa kiasi kikubwa ulijadili mradi wa mabasi yaendeyo kasi mkoani Dar es salaam (DART). Nilidokeza athari za mpango huo na kufananisha na yaliyotokea katika mchakato wa TRL.


Nilimalizia kwa kuwa changamoto washiriki kuwa Mafunzo yanapaswa kuwawezesha kwenda kwa umma kuwaeleza udhaifu wa uongozi ulioko madarakani na ufisadi uliokithiri lakini nikawataka wasiishie kukosoa tu bali muweze kueleza kwa kina sera mbadala za CHADEMA na kuondoa upotoshaji unaofanywa kuhusu sera hizo, na nikachambua kidogo kuhusu sera ya mfumo mpya wa utawala.

Hotuba kamili inapatikana hapa: http://mnyika.blogspot.com/2010/01/hotuba-yangu-jimboni-ubungo-nikifungua.html , sehemu ya maadhui ya hotuba hii imetoka katika vyombo mbalimbali vya habari tarehe 1 Februari 2010 lakini naamini maudhui yake yanaweza kuendelea kujadiliwa tuendeleze fikra mbadala za kuleta mabadiliko kuanzia ngazi ya chini.

Nawatakia mjadala mwema

JJ
 

Nilimalizia kwa kuwa changamoto washiriki kuwa Mafunzo yanapaswa kuwawezesha kwenda kwa umma kuwaeleza udhaifu wa uongozi ulioko madarakani na ufisadi uliokithiri lakini nikawataka wasiishie kukosoa tu bali muweze kueleza kwa kina sera mbadala za CHADEMA na kuondoa upotoshaji unaofanywa kuhusu sera hizo, na nikachambua kidogo kuhusu sera ya mfumo mpya wa utawala.

JJ
Mnyika, hao unaowatuma kwenda kwa Umma kueleza UFEDHULI wa Chama Cha Maulaji umewapa nyenzo gani kufikisha hicho unachokikusudia? Wana access na vyombo vya aina yoyote ili kuhubiri hayo?
Upinzani tuache blah blah...!
 
JJ

Ningetamani kukuandikia ujumbe huu kwa njia ya PM.
Ushauri wangu ni kuwa si lazima hotuba zako katika vikao vya ndani ya chama zitolewe kwenye jamvi.
Believe me, hii ndiyo sumu inayotaka kukiua chama chetu.
Wakati umefika, tukomae.
 
JJ

Ningetamani kukuandikia ujumbe huu kwa njia ya PM.
Ushauri wangu ni kuwa si lazima hotuba zako katika vikao vya ndani ya chama zitolewe kwenye jamvi.
Believe me, hii ndiyo sumu inayotaka kukiua chama chetu.
Wakati umefika, tukomae.


Baija

Asante kwa maoni yako.Hii ni hotuba ya wazi kwa umma, kwenye ufunguzi waandishi wa habari walikuwepo. Baada ya hapo mambo yote yalikuwa ni siri, ndio maana hatukutoa hadharani mada mbalimbali zilizotolewa, majadiliano yaliyofanyika wala maamuzi/maazimio yaliyofikiwa. Mara nyingi huwa tunatoa hotuba za ufunguzi ambazo hatuzileti jamvini, ni za siri.lakini unavyoona tumeleta, ujue ni zile za wazi

JJ
 
Mnyika, hao unaowatuma kwenda kwa Umma kueleza UFEDHULI wa Chama Cha Maulaji umewapa nyenzo gani kufikisha hicho unachokikusudia? Wana access na vyombo vya aina yoyote ili kuhubiri hayo?
Upinzani tuache blah blah...!

Chama sio cha Mnyika ndugu yangu, chama ni cha wanachama kama nilivyoelezea kwenye hotuba yangu. Wengine nasi tunachangia kama sehemu ya wanachama. Unazungumzia nyenzo za aina gani?

JJ
 
Mnyika, you will be better off ukienda kwenye majukwaa ya siasa mitaani na kumwaga 'sera' zako utakuwa umefanya kazi yenye manufaa sana. Nakusoma kila mara hapa lakini sijakuona wala kusikia umekuja kwenye mitaa na vitongoji vya Ubungo kufanya mkutano wa hadhara kuelimisha kama unavyofanya hapa. Huko mitaani ndiko waliko wengi wenye masikio ya kusikia!
 
CCM yazindua maadhimisho ya miaka 33

Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akitoa kadi kwa wanachama wapya katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 33 ya Chama cha Mapinduzi kitaifa mjini Bagamoyo.
Makada wakila kiapo cha utii katika Chama.
Pia alikuwepo...
Pia alirejea kiapo chake cha Utii katika chama.
3.JPG
Halaiki ikionesha vitu vyake.
wanachama wakiwa katika viwanja vya sherehe
Kiongozi wa TOT Pluys Capt. John Damian Komba (MB) akitumbuiza.

Kutoka kwa Mroki Mroki.
 
CCM si chama kibaya. Ila viongozi wao wa miaka hii, si wabunifu. Wanafikiri chama kitaendelea kushika hatamu. Wanashindwa kudadisi; vi wapi vyama vilivytawala Kenya, Zambia, Malawi na Uganda.


Ni kweli yale yaliyobainishwa na Baba wa taifa enzi za CCM yajenga nchi ya 1977 hayapo tena jamii imeachwa kama mtoto yatima hakuna wa kuisaidia hakuna wa kumkanya mwenzake wazee kama watoto na watoto kama wazee

Akina Butiku walijaribu kuona kama wataweza kuirudisha heshima ya CCM ya wakati ule lakini tumeshuhudia wakiitwa wahuni sijui nani muhuni kati ya wanaosema ukweli na wanaoona mambo ndani ya chama ni shwari lakini yetu macho siyo mbali tutaona kila mtu ndani ya CCM anajichukulia chake mapema.
 
Mnyika, you will be better off ukienda kwenye majukwaa ya siasa mitaani na kumwaga 'sera' zako utakuwa umefanya kazi yenye manufaa sana. Nakusoma kila mara hapa lakini sijakuona wala kusikia umekuja kwenye mitaa na vitongoji vya Ubungo kufanya mkutano wa hadhara kuelimisha kama unavyofanya hapa. Huko mitaani ndiko waliko wengi wenye masikio ya kusikia!

Boramaisha

Asante kwa maoni yako, mtaa gani katika kata gani? Maana Novemba na Disemba 2009 pamoja na Januari 2010 nimekuwa kwenye ziara katika mitaa kadhaa.

Ila nakubaliana nawe kwamba ni muhimu kuwalenga wananchi huko mitaani hususani wenye masikio ya kusikia.

JJ
 
Heshima Mbele!

Hakuna cha kujifunza zaidi ya ufisadi kama sio wizi. Nashangaa members humu ndani wanaosema CCM sio mbaya kama chama. Si chama kinajengwa na watu au wanachama? Nadhani hakuna chama kama hakuna wanachama (watu). Hivyo CCM ni wizi na unyama, hakuna zaidi ya hilo wanaJF.

Angalia Watanzania wanavyo geuka kuwa maskini wa kutupwa chini ya CCM, wanavyo dhulumiwa haki zao (Loliondo na kwingineko) na sasa pwani au fukwe za jiji la Dar es Salaam.

Cha kushangaza wapo waTanzania wameshaikubali hali hii na kujiona hawastahili kuwa na maisha bora zaidi ya bora maisha. Natamani WaTZ wote mungu atuue ili uje uzao mwingine ulio safi. Ambao utajali vizazi vyao kuliko ilivyo sasa. Fisadi wenye mwenye haki ndani ya CCM. Nilipokuwa TANU YOUTHLEAGUE, tulifundishwa mengi kuhusu usawa wa binaadamu na watanzania kwa ujumla wake. Nilikariri na kuelewa vyema imani hii. Leo hii ni binadamu wote ni sawa lakini wengine ni sawa zaidi. (All animals are equal but others are more equal. ref. animal farm).

Angalia watu ndani ya CCM wamelewa ufisadi hata wanayosema na kuwaahidi watanzania kila siku ni vichekesho. Eti mtu mwenye akili kweli anaweza kusemba ahadi alizotoa MH. zimetimizwa kwa asilimia 500? Jamani hata nchi kama Denmark ambayo ndiyo nchi yenye uchumi bora dunia haijafikia kiwango hicho. Hivi huu ni uwenda wazimu au wehu anaousema mzaa wa Mahezanguu a.k mzee wa kuropoka?

CCM NI UNYAMA.
 
Back
Top Bottom