Tunajifunza nini kutokana na mapungufu ya miaka 50 iliyopita? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajifunza nini kutokana na mapungufu ya miaka 50 iliyopita?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Dec 27, 2011.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Happy new year!mwaka 2011 unapita na mambo yake yote yanapita.Ni mwaka uliokamilisha idadi ya miaka hamsini ya uhuru wa nchi yetu toka mikononi mwa wakoloni.Tumekumbuka mengi kutokana na machungu waliyoyapata mababu zetu,tumejifunza mengi kutokana na yaliyopita lakini swali la kujiuliza tumevuna nini kutokana na yale yote yaliyopita ndani ya nusu karne?Wakati tunakabidhiwa nchi toka mikononi mwa wazungu tuliamini tunaweza,japokuwa hatukuwa na uzoefu wa kujitawala wenyewe na kufanya mambo yetu wenyewe bila kusimamiwa na watu weupe.Tuliamini umanamba umefika kikomo ikiwa kila Mtanganyika kuwa na haki sawa katika kuliletea taifa hili maendeleo.Tuliamini mfumo wa ujamaa na kujitegemea ndo suluhisho pekee la kuelekea kwenye mapinduzi ya kijani.Tuliuenzi mfumo huu kivitendo tukiamini wote tungefaidika na matunda ya uhuru.

  Mwalimu akiwa muumini mzuri wa ujamaa aliunda Azimio la Arusha miaka sita baada ya kupata uhuru.Azimio lilobeba maudhui mazito juu ya miiko ya uongozi na juu ya kugawana keki hii ya taifa bila kujali matabaka ndani ya jamii hii.Watanzania waliishi kijamaa wakiendesha shughuli za kijamaa.kwa kweli machungu ya kutumikishwa wazee wetu yalipotea kutoka ndani ya fikra mgando kuwa sisi waafrika ni watu wakutawaliwa na weupe.

  Nikiingia katika point ya msingi iliyonilazimu ni wakilishe thread hii,ni kutafakari kwa kina juu ya uzalendo wa taifa letu na mfumo dume ulioligubika taifa hili na kusahau usawa wetu uliohubiriwa na waasisi wa taifa hili bila kumung'unya maneno.Uzalendo uliopelekea kila mwananchi wa nchii kuamini rasilimali zote za taifa letu ni mali yetu sote.Kila mmoja aliamini ana haki ya kuwa kiongozi katika taifa hili ilimradi awe na akili timamu na akubalike na watu.Haki hii ya msingi imekwenda wapi ndani ya miaka hamsini baada ya uhuru?Tunajifunza nini wakati tunaukaribisha mwaka 2012,tunaingia tukiwa na malengo gani juu ya nchi yetu ili hali wengine ni wahanga wa siasa chafu zilizogubikwa na chuki na ulafi wa madaraka wakati uwezo wa kuongoza haupo!Inawezekanaje kuhubiri kuwa tunafuata mfumo wa ujamaa wakati vitendo ni vya kibepari?

  Uko wapi utaifa wetu ikiwa hatuweze hata kuhoji katiba tunayoitaka iweje katika karne hii ya sayansi na tekenolojia!Tunajifunia nini ndani ya mika hamsini ya uhuru wakati wananchi wake wengi waishio vijijini wanatumia mipira kama kandili kwa ajili y akupata mwanga.Tunakwenda wapi wakati taifa halina mipango ya muda mfupi na mrefu katika kuwaletea watu wake maendeleo?Sipendi kuamini kama tunasindikiza miaka kwa kuhesabu matundu ya choo wakati wenzetu wanafikiria kuwekeza kilimo kwenye sayari ya mars.Ulimbukeni huu wa madaraka na ubinafsi unatoka wapi wakati hatukuachiwa mikoba hiyo.Hazina kubwa ya fikra itaendelea mpaka lini kuzikwa ikiwa kizazi hiki kinachoongoza taifa hili kimefikia ukomo wake wa kufikiri?Ni lini basi tutaamkaa usingizini kutokana na ulevi wa madaraka kwa kujilimbikizia mali kwa kuplan sikukuu zisizo na tija wala mashiko.

  Hofu yangu kubwa kizazi kijacho kinaweza kufukua makaburi yetu na kutuwasha moto kutokana na kuupoteza uzalendo ndani ya nchi yetu.Hii ni hatari kwa taifa linalojiita kisiwa cha amani na utulivu wakati wananchi wake hawajui siku yao itaisha vipi.Tunaingia miaka mingine hamsini kwa style mpya ya kukandamiza haki ya kikatiba ibara ya 18 juu ya haki ya kutoa mawazo.Ni hatari sana kwa taifa lenye kauli mbiu mpya zisizo na tija wala mashiko.Taifa ambalo bado linaendesha umeme kwa nguvu za maji(HYDRO POWER) na kutegemea mvua za msimu wakati tuna vyanzo vingi vya maji.Ni lini basi ombwe hili la fikra litaondoka miongoni mwetu na kufanya maamuzi magumu kama Nabii Mussa alipoamua kujitoa mhanga kuwakomboa wana wa Israel mikononi mwa Fiaruni.Naamini ndugu zangu mtatoa mawazo mbadala zaidi nini cha kufanya ili kuweza kulikomboa taifa letu kivitendo zaidi kuliko maneno.naomaba kuwakilisha
   
Loading...