Tunajifunza nini kutoka Rwanda?

Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
16
Makala hii imetoka RAIA MWEMA-28/11/2007 na imeandikwa na P-Karugendo. Ilikuwa ndefu lakini nimeweka kipande tu ambacho tunaweza kufanya comparison kati ya TZ na Rwanda.

Mambo mengi yalinishangaza Rwanda kinyume na nilivyotarajia. Kutoka mpakani hadi Kigali, sikuona askari mwenye bunduki. Ina maana kwa muda mfupi, wameweza kujenga amani na utulivu.

Lakini la kushanga zaidi ni uchumi wao. Pale mpakani nilipotoa shilingi 10,000 za Tanzania, nilipewa 3,500 za Rwanda. Ni wazi niliibiwa kidogo, lakini ukweli ni kwamba pesa ya Rwanda ina nguvu zaidi ya Tanzania. Wenyewe wanasema ni shilingi 10,000 kwa shilingi 5,000 za Rwanda – lakini kwa maisha ya kawaida ya mpakani ni 3,500 hadi 4,000.

Swali ambalo bila shaka linaweza kujibiwa na wanauchumi, ni inakuwa vipi, Rwanda, nchi iliyokuwa vitani, nchi ambayo haina rasilmali nyingi kama Tanzania, iwe na pesa yenye nguvu kuliko Tanzania?

Mfano, Mkoa wa Kagera, ni mkubwa zaidi ya Rwanda. Mkoa wa Kagera, una rasilmali nyingi, una ardhi ya kutosha, mazao mengi ya biashara yanastawi, una misitu, una madini, una ziwa lenye samaki wengi, una watu milioni mbili. Ukilinganisha watu wa Mkoa wa Kagera na rasilmali zilizopo, kila mtu angekuwa na maisha mazuri. Rwanda ina watu milioni tisa na rasilimali kidogo ukilinganisha na Kagera, lakini Rwanda imeendelea kwa mbali ukilinganisha na Mkoa wa Kagera.

Wanyarwanda, wanasema maendeleo yao yanatokana na rasilmali watu na uongozi bora. Ni kwamba Rais Paul Kagame na viongozi wenzake wana “vision” na mikakati ya kuendeleza taifa lao. Wana mipango mingi na wamefanya mengi, hapa ninataja yale tu niliyoelezwa kwa muda mfupi niliokaa Kigali: Mpango wa kufuta magari ya serikali, umepokewa na kukubaliwa na wengi. Leo hii kila Mnyarwanda, anatambua jinsi pesa nyingi za serikali zilivyokuwa zikipotea kwa kuyashughulikia na kuyatunza magari ya serikali.

Mpango wa kuwajibishana, umewavutia walio wengi. Hakuna kulindana katika serikali ya Rwanda, hakuna urafiki wala kulindana; anayeshindwa kuwajibika, anafukuzwa bila kujali cheo chake au mchango wake wakati wa vita ya ukombozi. Kinachotangulia na kujenga taifa, na wala si urafiki, undugu au chama. Mpango wa kuwasikiliza wananchi na kutambua kwamba serikali ipo kuwahudumia wao, umewavutia wengi. Nimeambiwa kwamba Rais Kagame, anapotembelea wilayani, viongozi wanakuwa matumbo joto, maana akijitokeza mwananchi akalalamika na malalamiko yakawa ni ya kweli, mkuu wa wilaya anaweza kupoteza kazi hapo hapo!

Mpango wa kujenga utaifa na kufukia tofauti za makabila , umepokewa kwa shangwe kubwa na wote. Ingawa ni vigumu kuangalia kwenye mioyo ya watu, yale yanayoonekana kwa nje yanaleta matumaini makubwa. Mpango wa kufuta uongozi wa mikoa, na kupeleka madaraka yote wilayani , umewavutia watu wengi na umepunguza gharama zilizokuwa zikitumika kufanya mambo yale yale kwenye ngazi ya mkoa na ngazi ya wilaya.

Mfano Mganga Mkuu wa Mkoa na Mganga Mkuu wa Wilaya. Watu hawa walikuwa na kazi zinazofanana, matumizi yalikuwa yakiongezeka bure. Hivyo kwa ngazi zote, ni kutoka wizarani na kwenda wilayani. Pesa nyingi zilizokuwa zikitumika kwa mishahara ya watumishi wa mikoa, zinatumika kwa mambo mengine, na mambo haya yanaonekana!

Mpango wa kujenga shule nzuri na vyuo vizuri, umewavutia Wanyarwanda wengi. Watoto wa Rais Kagame, wanasoma Kigali. Watoto wa viongozi na matajiri wanasoma Kigali. Hivyo wakiongea juu ya kujenga shule, watu wanawaamini.

Maendeleo ya Rwanda, yanaonekana kwa macho. Si lazima uwe mtaalam wa uchumi kutambua kwamba Rwanda, inapiga kasi ya kutisha ya maendeleo. Jiji linavyojengeka, barabara zilivyopangiliwa, usafi, huduma muhimu kama ubora wa hospitali, vijiji vilivyopangiliwa, ubora wa mashamba ni ishara tosha kuonyesha maendeleo ya nchi.

Serikali ya Rwanda inapambana na rushwa na inaelekea kufanikiwa. Juzi, walifukuzwa askari zaidi ya sitini, baada ya kubainika wamepokea rushwa, walikamatwa baada ya mama mmoja askari wa cheo cha juu kujibadilisha na kujifanya dereva wa lori la mkaa. Wana mbinu nyingi za kuwakamata wala rushwa.

Linaloshangaza zaidi ni uzalendo wa Wanyarwanda. Watu hawa wanalipenda taifa lao. Inaonekana wazi kwamba kila mmoja anafanya kazi kufa na kupona ili kulijenga taifa lake. Na wanaposema juu ya taifa lao, wanasema kwa majivuno.

Kuna rafiki yangu mmoja, aliyeniambia kamba ili Tanzania iendelee ni lazima Watanzania wabadilike, wawe na moyo wa uzalendo na walipende taifa lao. Huyu ni Mnyarwanda, aliyeishi Tanzania kwa miaka mingi. Bila shaka alikuwa na maana yake kusema hivyo.

Lengo la makala hii ni kutaka kutoa ujumbe kwa Watanzania kwamba tuna mengi ya kujifunza kutoka Rwanda. Ni nchi ndogo yenye mambo makubwa. Badala ya kusema uchumi wetu unapaa wakati shilingi 10,000 za Tanzania ni sawa na shilingi 3,500 za Rwanda; badala ya kuendelea kuyahudumia magari ya serikali wakati tunachangisha wananchi kujenga sekondari za kata; badala ya kuendelea kuwahudumia watumishi wa mikoa na wilaya, wakati hatujajenga hospitali za kutosha; badala ya kuendeleza urafiki na utamaduni wa kulindana wakati mambo yanakwenda vibaya serikalini, ni bora kukubali kwenda kujifunza kwa jirani zetu wa Rwanda.

Ninaamini Weusi tuna akili nzuri. Tatizo ni kwamba tunateleza na kuanguka, na wakati mwingine tukianguka, ni mwereka wa mende, tunashindwa kuamka na kuendelea na safari. Tanzania, tumeteleza na kuanguka, anayekataa, si mkweli!

Juzijuzi tuliwafukuza maelfu ya Wanyarwanda kutoka Karagwe. Watu hawa walikuwa wamelima mashamba makubwa na kuzalisha chakula kingi, walikuwa wafugaji. Kukaa kwao kwenye maeneo ya Bushangaro na kwingineko, kuliwafukuza wanyama. Walipoondoka, mashamba yao yamegeuka mapori na wanyama kama Tembo wameanza kusogea tena na kutishia maisha ya wakazi wa Karagwe.

Mbunge wa Karagwe Brandes Begumisa, alilalama bungeni, kwamba watu wake wa Karagwe, wanashambuliwa na wanyama pori. Hakumbuki kwamba hayo ni matokeo ya kuwafukuzwa Wanyarwanda. Tuliwafukuza bila kuangalia mbele, tuliwafukuza bila mipango inayoeleweka. Tungewaacha, wakalima, wakafuga, tukawatoza ushuru, ingechangia kiasi kikubwa maendeleo yetu. Tumewafukuza na sasa tunapiga kelele kwamba tunashambuliwa na wanyamapori.

Wakati umefika wa kujihoji na kutafuta tulipoteleza. Wakati umefika wa kujiuliza ni mawaziri wangapi ambao watoto wao wanasoma kwenye sekondari za kata; hakuna waziri asiyetoka kwenye kata; ni mawaziri wangapi ambao watoto wao wanasoma sekondari za Tanzania.

Wakati umefika wa kukubali kujifunza hata kama ni kutoka kwenye nchi ndogo kama Rwanda. Tusipokubali kujifunza, majuto ni mjukuu!
 
[COLOR="red" said:
Mpango wa kujenga shule nzuri na vyuo vizuri, umewavutia Wanyarwanda wengi. Watoto wa Rais Kagame, wanasoma Kigali.[/COLOR] Watoto wa viongozi na matajiri wanasoma Kigali. Hivyo wakiongea juu ya kujenga shule, watu wanawaamini.!

Juzi mtoto wa Karume--Fatma amejisifu kuwa kafunzwa sheria vizuri UK, je sheria inayofundishwa TZ haina lolote? ni watoto wangapi wa vigogo wanasoma shule za TZ hasa za kawaida?
 
Bank kuu ni chombo kinacho angalia na nguvu ya shiling. Central bank is obligated to control money circulation, which influance the strength or weakness of shilling.

Kitu kimoja kinacho tuumiza watanzania ni kungana kati ya bank kuu na serikali. Bank kuu si chombo huria ndani ya Tanzania, madhara yake ni viongizi wa kisiasa kutia mkono wao kwenye maamuzi ya kibank ambayo yana effect katika uchumi. Vitu kama kuprint pesa pasipo kujali supply ya pesa kwa wakati huo.

Bank kuu imefanya blanda nyingi sana ambazo zimetufikisha hapa tulipo. Ukubwa au udogo wa nchi haujalishi katika swala la nguvu ya fedha, kinachojalisha ni njia za kuendesha mfumo mzima wa mzunguko wa fedha.
swala hili linaitaji uchambuzi yakinifu, lakini hakuna mausiano kabisa ya ukubwa au udogo wa nchi.
 
Juzi mtoto wa Karume--Fatma amejisifu kuwa kafunzwa sheria vizuri UK, je sheria inayofundishwa TZ haina lolote? ni watoto wangapi wa vigogo wanasoma shule za TZ hasa za kawaida?

Do not hate the players, hate the game! Unafahamu ya kuwa hivi sasa University ya Kigali na hata consultants wa serikali ya Kagame wengi ni waBongo? Je unajua pia maprofesa wanaofundisha medicine wangapi wako nje ya nchi? Elimu Tanzania iko chini, na si watoto wa Karume tu, hata watoto wa middle class people wanakimbilia nje ya nchi kusoma. Tusijidanganye, wengi wanaJF tuko nje, na wengine wetu tumesoma nje na si lazima wote ni watoto wa vigogo.
Kinachotakiwa ni mipango madhubuti ya kuboresha elimu lakini tusiangalie eti mtoto wa nani kasoma wapi! Tuangalie ni hatua gani za maksudi zimechukuliwa ili kuboresha elimu.
 
Hapa issue ni kwamba viongozi wetu hawaoneshi uzalendo kwa taifa letu. Wao ndio wanakuwa wa kwanza kututosa.
Kama viongozi, wake zao, watoto na ndugu zao hata check up wanakwenda Kenya, South Africa, Ulaya au Marekani, Kuna haja gani ya kuboresha hospitali muhimbili? Unaweza kumwambia Balali kuhusu muhimbili akakuona unaakili?
Same applies to schools. Kama kungekuwa na sheria ya kuwafanya viongozi wetu wafanyiwe check up nyumbani, watibiwe nyumbani, na kama kungekuwa na sheria inayowabana wasomeshe watoto wao Tanzania basi no doubt kungekuwa na shule mbili au tatu zenye hadhi Tanzania. Huenda hata sisi kina kapuku tungenufaika. Sasa hivi tunadanganyana tu. Kinachosemwa ni kudanganya watanzania.
 
Do not hate the players, hate the game! Unafahamu ya kuwa hivi sasa University ya Kigali na hata consultants wa serikali ya Kagame wengi ni waBongo? Je unajua pia maprofesa wanaofundisha medicine wangapi wako nje ya nchi? Elimu Tanzania iko chini, na si watoto wa Karume tu, hata watoto wa middle class people wanakimbilia nje ya nchi kusoma. Tusijidanganye, wengi wanaJF tuko nje, na wengine wetu tumesoma nje na si lazima wote ni watoto wa vigogo.
Kinachotakiwa ni mipango madhubuti ya kuboresha elimu lakini tusiangalie eti mtoto wa nani kasoma wapi! Tuangalie ni hatua gani za maksudi zimechukuliwa ili kuboresha elimu.

Nafikiri we need to be more specific. Hivi unafikiri ni nani mwenye kuchukua hatua za makusudi kama sio viongozi kuwa mfano. Cha muhimu ni viongozi kuwa na vision ya kweli, unafikiri kama kiongozi akiugua anatibiwa nje, watu wengine hata kama wakitibiwa isivyo muhimbili yeye inamgusa moja kwa moja?. Juzi wakati KAPUYA kapelekwa India na yule mwenzake akafia muhimbili--uone difference?. Inabidi viongozi wafeel impact ya system kama vile mtoto wake akisoma shule isiyokuwa na walimu na akatoka kapa ndo atajua kuna umuhimu wa ku-invest kwenye elimu ya ndani.

Unasema elimu iko chini nani alaumiwe? nafikiri chanzo ni viongozi ambao sisi wananchi tumewachagua. Je maprof. kukimbilia nje ya nchi nani kawakimbiza? wameenda nje kutafuta nini ambacho akipatikani Tz?

So ukiweka viongozi nje nafikiri huwezi kupata suluhisho la matatizo yanayolikabili taifa la Tz. Ndo maana unamwona KAGAME watoto wake wanasoma KIGALI sababu shule zimeboreshwa.
 
..rwanda imefika hapo kwa kuwa ina wenyewe!

..wananchi wanajishughulisha na shughuli za maendeleo ili kuboresha maisha yao na kujenga taifa lao,na si kusudi wajirundikie mali bila mpangilio!

..wanajua kuwa nchi yao ni ndogo na inahitaji kujitegemea ili isionewe!

..wanajua kuwa hawana rasilimali nyingi kwahiyo zile chache zilizopo lazima wazitumie vizuri na kuzijenga zikue zaidi!

..tanzania is a sleeping giant!nchi isiyo na mwenyewe au yenye watu wachache wanajiona kuwa wao pekee ndio yao!

..tunalo shamba lenye rutuba,jembe na mbegu,lakini tumelala tunasubiri kula wakati hatujalima wala kupanda chochote!

..tumelewa vitu vingi!, we are living a fantasy!and staying poor!
 
Do not hate the players, hate the game! Unafahamu ya kuwa hivi sasa University ya Kigali na hata consultants wa serikali ya Kagame wengi ni waBongo? Je unajua pia maprofesa wanaofundisha medicine wangapi wako nje ya nchi? Elimu Tanzania iko chini, na si watoto wa Karume tu, hata watoto wa middle class people wanakimbilia nje ya nchi kusoma. Tusijidanganye, wengi wanaJF tuko nje, na wengine wetu tumesoma nje na si lazima wote ni watoto wa vigogo.
Kinachotakiwa ni mipango madhubuti ya kuboresha elimu lakini tusiangalie eti mtoto wa nani kasoma wapi! Tuangalie ni hatua gani za maksudi zimechukuliwa ili kuboresha elimu.

Una uhakika kuwa hao wabongo wanaofanya kazi nje hawajasomea Tanzania?
Kama elimu ya kibongo iko chini iweje wataalam wake wanatumika nchi za watu?

Hao tuseme Tanzania ina wataalam wazuri ndo maana wanakuwa lulu nchi zingine kuonyesha elimu yetu iko bomba!
 
semanao,

nashukuru kwa kuyaweka baadhi ya mambo mazuri ayafanyayo Rais Kagame kwa nchi yake.............kule ktk East African section hapa hapa JF nimemsifia Kagame.....kuna baadhi ya wanaJF wakauliza na kusema kuwa si kweli Rais Kagame anastahili sifa hizo...............anyway......siwezi kumlazimisha mtu kukubali ukweli kuwa Rais Kagame has a Vision kwa nchi yake na ana support kubwa ya wananchi wake.................nilikuwepo Rwanda 1999 - 2000, napia nilikuwepo tena 2003............huwezi kuamini the +ve difference ya maendeleo nilyoyaona................ufanisi kwa wafanyakazi serikalini, infrastructures, service industry yao, na project zinazoendelea...........inatia moyo....kweli nashauri tujifunze toka kwao.

Viongozi wabovu................wana-survive mpaka leo hii hapa Tanzania......ingekuwa kwa Rais Kagame sidhani kama with an inch hawa viongozi wange-survive
 
Yes Kagame ana mapungufu yake kama binadamu, wengine wanamwita mbabe. kwa nchi kama rwanda inahitaji mtu wa aina ya Kagame ili isonge mbele. kagame ana vision na akidhamiria jambo anahakikisha linafanyika. kuna members hapa ukiitaja rwanda kwamba inapaa hawataki kuamini. Kagame amewatumia watanzania kujenga nchi yake. nenda kigali institute of technology ndiyo utajua watanzania wanafanya nini pale. hatuna jinsi ila kuiga Rwanda hata kama ni nchi ndogo,hata kama ilikuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe twende huko tusione aibu.
 
Hawana mchezo hao,hata shirika lao la ndege sasa ni one of the best in Africa na linajiendesha bila ruzuku ya Serikali
 
Jamani Katika kufanya analyisis tunaweza kujua ni vipi Kagame ana uchungu wa nchi yake pamoja na wanyarwanda kwa ujumla ukilinganisha na Viongozi wetu wa juu kitaifa. Kagame hakuingia ikulu ya kigali kwa kutoa rushwa au ubabaishaji. He has to fight. anaujua uchungu wa porini. kwa hiyo kushinda vita ni sign kuwa wananchi walimuunga mkono. Na kwa kuwa ni mwadilifu then anahakikisha kile watu walichomwaga damu kukipigania kinapatikana nacho ni maisha bora kwa raia. He is a strict guy. Kwea Tanzania ninamfananisha na hayati Moringe. Kwa hiyo hata wale wazembe wamekoma sasa. Taifa linapiga hatua.

Kwa upande waelimu Tanznia sio kuwa elimu ni ya chini hilo si sahihi. Nilisoma Tanzania kuanzia vidudu( chekechea sexy language)- mpaka pale mlimani kabla sujaja huku ughaibuni Wot I foung I was far better than many of the indegneous students. Tatizo ni uongozi usiojali uwajibikaji, uongozi unaojali matumbo yao, uongozi wa ubabaishaji usion mwelekeo. Urafiki unatawla mno katika kuongoza ndiyo maana hatufiki kokote. There is no seriouness. TUOMBE MUNGU ATULETEE ANOTHER OF HAYATI MORINGE Character ili nchi iendeshwe kwa descipline. Hakuna descipline ya uongozi. ni kama GAME TU. UPOLE NAO UNATUUA!! HATUTAKI MAKUU, TUNA HURUMA MNO HATA KWA WAUAJI!! wot do you expect. tutawaona wakiendelea. Uganda museveni alianzia pale HALL five Mlimani vita Uganda je waganda tualingana nao pamoja na kuwakomboa toka kwa nduli? seriouness. sie wacha tu twe na Vasco da Gama avumbue dunia kwanza then atatulia kama alivyosema Rupia!! then atakuwa serious na kazi.
 
Maarifa.
Mungu akiwaletea viongozi kama moringe mnawapa kura mbile, sasa wacha awaletee kama JK ili muwape 80% ya kura. Rwanda ni nchi ndogo, easy kuyaona maendeleo. Hata kucalculate GDP per cap itakuwa kubwa.

Elimu ya Tanzania kuanzia one to six ipo tight, however to much theory. UDSM ni bomu kubwa tuu. Watanzania wengi wana vipaji vya kielimu sema system inawaangusha chini.
 
Ogah,Semanao,Saharavoice,koba,maarifa,mtanganyika,
Rwanda ni nchi ndogo sana. Labda tujiulize kwanini ZNZ haipigi hatua kama Rwanda au Mauritius na Seycheles.

Tukitaka kuwa fair tujilinganishe na Kenya au Ghana. Hao ndiyo saizi yetu.

Elimu ya Tanzania inahitaji vifaa, vitabu and lab equipment. Bila kusahau waalimu walioiva.

Wakati nipo shuleni serikali ilikuwa inatoa madaftari pamoja na text books kwa kila mwanafunzi. Maabara zilikuwa na vifaa vyote. Shule zilikuwa na store za kufuga panya, na mabwawa ya samaki na vyura.

Uchumi ulipoporomoka kila kitu kilipotea. Ilifikia kipindi wanafunzi 4 mna-share kitabu kimoja tena wakati wa kipindi. Serikali ilishindwa hata kuweka viti tukawa tunakalia matofali.
 
Angalieni watu wasione mlivyoandika na kulalamika saaana maana kuna watu hapa wanakataa kuwa maendeleo na umasikini havina uhusiano na uongozi.Mie nimesema tu.Tehehehe
 
Thanks for ur analysis. However sidhani ukubwa ama udogo wa nchi ni sababu. Ndiyo tukifuta kanuni za calculation za GDP it quite true idadi ya watu inaaffect wot GDP U get. Lakini kuna mambo mengine hata huhitaji calculation. Kwani ukubwa sio ndiyo ingekuwa faida maana tuna rasilimali kibao Kuanzia madini, watu wengi(Human capital= idadi + shule) kama ni kusoma I do think kuwa wapo tu wa kutosha maana ndiyo maana wengi hukimbilia nje kutafuta green pasture. Lakini kwa Tanzania mfumo mzima ni feki. It true true serious leaders katika kura watapata 2% kwa Tanzania kwani tumezoea mbwembwe. komba alianzaia NEC, ,Mbunge huenda akawa waziri wa madini. Hadija Kopa na TAARABU yuko NEC ya CCM kesho mbunge na nateuliwa kuwa waziri wa miundo mbinu! I think mnanielewa wot I mean Missallocation of resources including human. ndiyo maana there is Accountability na responsibility. Angalia Baraza la MAWAZIRI Mlima hata hawajui wot they are doing, they are not serious. they are not effective. We are in A viscious cirle. Viongozi ni maskini wakiingia mdarakani akilai yao ni kutafuta kwanza cha kati then Taifa. Hiyo si kwa viongozi wapigiwa kura tu hata maofisa wa serikali katika idara mbalimbali hawana usimamizi ulio bora kwani the whole system is corrupt and irresponsible. Ukimteua leo na hana usimamizi wa kutosha just a month kawa tajiri wa kutupa! 'Kila mtu anakula kazini kwake' hao ni proffessional waliosoma Tanzania na UGHAIBUNI NA WAKAIBUKA NA DISTINCTIONS za Nondos kama anavyoita rafiki yangu Michuzi. Lkini mazingira ni corrupt and irresponsible hivyo kila anaengia hata kama alikuwa msafi na mwadilifu annaguka. AKIKOMAA wanamuondosha ama kumbambika scandali. Sasa kazi where should we start? wanaotuongoza ni corupt wapiga kura nao huwachagua haohao. ni mpaka pale wapiga kura watakapog'mua janja ya nyani ndiyo hapo tu tutaanza piga hatua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom