Tunajifunza nini katika uchaguzi wa ccm wa spika wa bunge la kumi

Lalashe

Member
Nov 4, 2010
84
1
  1. Serikali ya CCM inajipanga kuongoza nchi kupitia Bunge
  2. Uteuzi wa Anna wawili na Kamba mmoja ni kutengeneza mazingira ya kuvunja nguvu za bunge na kufanya bunge na serikali kuwa kitu kimoja na kuongea lugha moja. MWISHO WA CHECKS AND BALANCES. Hii ina maana kwamba spika ajae hata ruhusu hoja zinazopeleka serikali kugaragazwa kama zile za RICHMOND NA EPA. Hivyo basi badala ya kuwa na mihimili mitatu ya serikali tunakuwa na mmoja. Kumbuka pia Mahakama ni sehemu ya executive branch-utakataa-je swala la mgombea binafsi the executive walikataa na mahakama nao wakalipiga chini-UTAWALA BORA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO CHALIII
  3. CCM wana uwakilishi mkubwa Bungeni hivyo basi kwa kura zao na spika wao watazima mambo mengi yasipite. Akina Mwakyembe, Sendeka na wengineo wakivimba na kuungana na wapinzani kuihukumu serikali wataitwa kwenye party caucus halafu mambo yanatulizwa na kuwekwa kapuni kama walivyolifanya Swala la UCHOMAJI WA KAYA ZA WAFUGAJI LOLIONDO BAADA YA TUME YA NDUGAI NA PARTY CAUCUS KUKAA UMEWAHI KULISIKIA SWALA HILO TENA, SUBIRI UTASHANGAZWA NA MENGI
  4. Raisi na baraza lake la mawaziri wanaweza kuondolewa madarakani na BUNGE sasa ukimweka spika ambaye haambiliki anaweza kuanzisha MOTION ambayo itapelekea kumwaga JK la baraza lake la mafisadi. Hata kama ni wewe sidhani kama utamweka spika wa aina hiyo kuliongoza Bunge ambalo kuna uwezekano mkubwa kwamba wamekuchoka na wakatumia nafasi hiyo kukumwaga baada ya kupata madaraka kwa kuiba kura. OGOPA mambo yanayoendelea ndani circles za mafisadi, wakuu wana wakati mgumu.
  5. Kingine wanachokwepa kwa uchaguzi huu ni raisi na baraza lake la mafisadi watakapo zidiwa hawataki kufikia hatua ya kuvunja bunge unajua kwanini-HAKUNA KITU CCM WANAOGOPA WAKATI HUU KAMA UCHAGUZI MKUU-Hivyo basi ni lazima wawekeze nguvu ya kunyamazisha bunge ili wasifikie mahali pa kulivunja. Wasiwasi wangu kwa bunge hili la kumi ni JE Anna wawili na kamba mmoja wataweza kweli kuwazuia WAGUMU KAMA AKINA LISU NA WENGINE kulipelekesha Bunge mpaka ikafikia hatua likavunjwa. Usishangae bunge hili likashindwa kuishi miaka mitano.
  6. CCM wakifanikiwa kwa hili la SPIKA, changamoto hazijawaishia bado kuna hili la WAZIRI MKUU AMBAYE NI MKUU WA SERIKALI BUNGENI-Wakiweka tu mtu anayelia lia ovyo wamekwisha. Wanajamii mnamwona nani atakayeweza kuliuganisha BUNGE na SERIKALI halafu mambo yakaenda shwari. IKO kazi kama mnaweza wasaidieni kuwapa mikakati japo haitawasaidia. Maji yakisha mwagika hayazoleki-CCM Finished.
 
Back
Top Bottom