Tunajifunza nini juu ya hii habari ya Obama na rafiki yake wa Uganda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajifunza nini juu ya hii habari ya Obama na rafiki yake wa Uganda?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CPA, Sep 18, 2012.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 738
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Obama na rafiki yake wa Uganda

  18 Septemba 2012 15:03

  Kama kuna rais ambaye watu wengi Uganda wangetaka kukutana naye ni rais wa Marekani Barack Obama.
  Kijana Christopher Kule, mwenye umri wa miaka kumi na ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi wilayani Kasese, nchini Uganda, hajaachwa nyuma katika ndoto hiyo.
  Bila shaka wengi watasema yuko hatua nyingi mbele ya wale walio na ndoto ya kumuona Obama. Hii ni baada ya Kule kupokea majibu ya barua aliyomwandikia Rais Barack Obama kutoka kwa Obama mwenyewe.
  Kijana huyo anaamini kuwa baada ya kuandikiana barua na Rais Obama, kuna matumaini kwamba siku moja atakutana naye.
  Yote haya yanatokana na zoezi la kuandika barua ambalo Kule na wanafunzi wenzake walikuwa wanafanya darasani, baada ya kuagizwa na mwalimu wamwandikie barua mtu yeyote wakiomba msaada kwa jamii yao.
  Barua ya Kule bila shaka ilimtia hamasa mwalimu wake wa kigeni kutoka Marekani ambaye alikuwa anafunza shuleni humo kwa muda.
  Mwalimu huyo alisema kuwa nyanyake ni rafiki wa mmoja wa wasaidizi katika ikulu ya rais na kuahidi kuhakikisha kuwa ujumbe huo utamfikia rais Obama na bila shaka ahadi ikatimizwa , kwani barua ilimfikia rais Obama.
  Kule alisema kuwa katika barua yake, alimwomba Obama kusaidia Uganda kuangamiza uasi na kuhamasisha amani.
  Katika majibu yake kwa Kule, rais Obama alisema kuwa Marekani imejitolea kuangazia maswala kadhaa muhimu kote duniani kama haki za binadamu kwa sababu Marekani inapinga vikali ghasia na ukandamizaji dhidi ya watu wote. Pia alimtumia kijana huyo picha yake aliyokuwa ametia saini.
  Rais Obama alipata muda wa kumjibu kijana Kule. Je marais wa Afrika wana muda wa kuzungumza na wananchi wao na kutoa mfano wa Obama kwa Afrika? Nini maoni yako?

  Chanzo: bbcswahili.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  waafrika wanajibu wadada tu lol
   
 3. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,122
  Likes Received: 1,209
  Trophy Points: 280

  Ukitaka jibu lililo sahihi, tumia mifano hai ukianza na rais wetu. Huyu kijana (Kikwete) toka achukue hii nchi alitoa ahadi kibao kwa kila Mtanzania kuwa na maisha mazuri, walio wengi wetu tulichekelea mpaka tukasusa kula kwa ajili ya furaha ya ahadi hewa. Binafsi, nilimwandikia barua kulalamika juu ya kumuhamisha wizara Dr. Magufili toka Ujezi miaka ya nyuma kwani ujenzi ulisimama kwa kukosa mwangalizi ama usimamizi mzuri. Ilikuwa ni miaka minne iliyopita, mpaka leo hii sijata jibu. Unataka kuniambia inachuku miaka minne kumjibu mwananchi, kwa kazi gani anayoifanya zaidi ya kutalii? Isitoshe angeweza hata kunijibu kwenye ndege wakati akipumzika kucheza karata/bao na washikaji zake, ila hakutaka. Hapa Afrika, viongozi wanafikiri wao ndo Mungu hawatakiwi kukosolewa kwa lolote lile.
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,628
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  kikwete labda ile chopa ya raisi iharibike ndio atapata muda wa kujibu barua kama hizi.............
   
 5. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hata waafrika ukiwa na refa unasaidiwa, si unaona dogo amesaidiwa na nyanya yake ticha ambae ana rafiki msaidizi wa ikulu
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona wewe ndio ulipata majibu mazuri? Magufuli si alirudishwa Wizara ya Ujenzi baada ya Rais kuisoma barua yako na kukubaliana na maoni yako!
   
 7. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Yaani Kikwetee akujibu barua wewe? Hana muda huo bana. Ngoja nikupe mfano hai.

  Kuna mlemavu mmoja aliwahi kutoka Arusha kwenda kumtafuta rais wake amuelezee jinsi maosha yalivyo magumu.
  Basi jamaa akajiandaa na vinauli vya kuokoteza, hatimaye akafanikiwa kupata nauli ya kumfikisha Dar, na hatimaye akafanikiwa kufika Dar mpaka posta mpya akasukuma baiskeli yake hadi getini Ikulu. Akagonga, akiomba kuonana na rais wake.

  Baada ya mkuu kuambiwa kuna mlemavu anataka kuonana nae, ndipo alipotoa amri ambayo ilimfanya yule mlemavu ajute kuchukua uamuzi wa aina ile.

  Yaliyomkuta yule mlemavu ni kukamatwa, kula kichapo, kusekwa rumande na kufunguliwa kesi ya kusababisha/kuleta fujo Ikulu. Kilichomuokoa ni wanaharakati wachache ambao hawakukubaliana na upuuzi huo.

  Huyo ndio rais wetu na response kwa wale wanataka kuonana nae, Je atatoa wapi muda wa kukujibu barua yako?
   
 8. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,122
  Likes Received: 1,209
  Trophy Points: 280

  Ni kweli lakini Magufuli alirudishwa lini? Wizara ya ujenzi ilidorora vibaya sana baada ya yeye kuondolewa gafla. Suala hapa ni kujibu barua ambayo yeye he never did answer up to now.
   
 9. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,122
  Likes Received: 1,209
  Trophy Points: 280

  Yaani aliamuru kumpiga Kikwete, samahani Kiwete kisa alikwenda kumlalamikia juu ya ugumu wa maisha? Si ni yeye aliyetoa ahadi feki kuwa maisha bora kwa kil mtanzania sasa watu wakitaka kujua ukweli anawafukuza tena? Kweli rais tunaye.
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Obama alijibu barua iliyofikishwa kwake na mtu wa ikulu kama ilivyoelezwa hapo. Sasa kama jamaa alituma kwa njia y posta inakuwa ni vigumu kwa Rais kuipata. Huenda washauri wake waliipata wakamshauri.

  Lakini mbona nasikia JK alikuwa akijibu sms!
   
 11. l

  luckman JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Obama ni kiongozi kikwete na viongozi wengine wa afrika ni watawala¬
   
 12. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,116
  Likes Received: 6,598
  Trophy Points: 280
  hata wa kwetu anajali pia.


  [​IMG]
   
 13. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Huo usanii mara nyingi anaufanyaga mbele ya Camera ili aandikwe vizuri.
   
 14. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  ah wapi JK wala asingeipata hiyo barua ingechanwa na sekretari wake au maafisa usalama wake
  ule mtindo wa karani kusoma barua ya boss wake upo sana Tanzania hata kusoma email za boss wake
  akiona barua au email ambayo kwake haina maana hatampelekea boss wake.
   
 15. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  kwa hizi comment,nimegundua watz wengi pia awamjali rais wao
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  :biggrin1: ni kweli kabisaa...alafu wanavosema marekani wanasisitiza haki za binadamu na kupinga ukandamizaji..mbona hapa bongo hawafanyi lolote...au kwa vile wameahidiwa kupata mikataba ya gas na oil basi mengine wamefumba macho
   
 17. Githeri

  Githeri JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 820
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  CPA Kumbe wewe mkenya? Hiyo lafudhi... Mhh!...alikuja kufunza,....nyanyake! Au ndo BBC swahili ya Kenya
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kikwete kawaita yanga ikulu, kawaita na kuongea nao madaktari, kawaita bongo fleva kina juma nature , na juzi juzi kamuita diamond . Bado watu walimsema sana rais. Sasa sijui mnataka rais afanyaje???????
   
 19. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Wabongo kwa kushadadia mambo ya kipuuzi hamjambo, yaani mbona hilo halikuhitaji hata headlines waganda wanamatatizo lukuki lakini sio uasi kama ingekuwa Kivu au somalia sawa.

  Yaaani mtoto wa miaka 10 uganda aombe msaada wa kuondoa waasi ambao hawapo, Jose au Kony mbona kitambo yuko chaka kasepa. Mbona tunawashobokea sana wazungu jamani hata kwa mambo ya kipuuzi.
   
 20. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  hao wote aliowaita ni wanachama hai wa mabwepande..believe me
   
Loading...