Tunajidanganya kwa kuamini kuwa ndoa ni tendo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajidanganya kwa kuamini kuwa ndoa ni tendo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jun 16, 2009.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Baadhi yetu tumelelewa na kukutana na mazingira yaliyotufundisha hivyo kwa hiyo ndivyo tunavyoamini. Tunaamini kwamba tunapooa au kuolewa tunafanya hivyo ili kushiriki tendo la ndoa kama dhana ya kwanza. Ni kitu gani kinachotokea basi pale ambapo haturidhiki na kuridhishwa kiunyumba na wake au waume zetu? Ni kwamba huwa tunadhani au kuamini kwamba hapo ndoa haina maana na hivyo huwajengea chuki wenzetu na pengine kutoka nje ya ndoa zetu tukidhani tutapata nafuu.

  Hebu tujiulize je ni kweli dhana ya ndoa ni kufanya mapenzi? Jibu ni siyo kweli hata kidogo. Hebu tujiulize tena baada ya kuoana na kuishi kwenye ndoa kwa muda fulani wake au waume zetu wakapata matatizo ya kimaradhi au ajali au mengine ambayo yatawafanya wasiweze kabisa kushiriki jambo hili tutafanyaje? Huenda jibu kwa wale wanaoamini kwamba ndoa maana yake ni kufanya mapenzi watasema kwamba watakwenda nje au kwa wanaume wataoa wake wengine. Huu ni ujinga mkubwa mno kwani tunaweza kufanya hivyo ikiwa ni wenzetu waliopata matatizo lakini kama ni sisi tutaona inavyoumiza.

  Tendo la ndoa katika ndoa ni muhimu na kwa kiasi cha kutosha husaidia pia kuimarisha uhusiano. Lakini pale kunapokuwa na tatizo kwenye suala hilo ndipo hapo upendo unapopimwa kama ni wa dhati, bandia, au upendo wa kimradi. Kama upendo wetu ni wa dhati tutajitahidi kuangalia mazingira ambayo huenda yatawafanya hao wenzetu wawe kama walivyo. Tunapojadili kwa upendo udhaifu fulani ni wazi tutawapa wengine nguvu ya kujikagua na kuzidisha upendo kwetu.

  Lakini tunapokuwa wakali na kulaumu au kuchukia na kulaani tutawafanya wenzetu wajione wanyonge na pia tutawafanya au kuwapa nafasi ya kuhalalisha kwamba huenda sisi tumetawaliwa sana na tamaa ya kimwili kuliko uwezo wa kufikiri kiasi kwamba linapotokea tatizo tunakuwa vichaa na hivyo uwezekano wa kutoka nje au kuvuruga ndoa ni mkubwa. tujifunze kufahamu na kukubali ukweli kwamba ndoa bora na imara hazifanywi hivyo na tendo la ndoa, bali hufanywa hivyo na wanandoa kusaidia kutatua kila tatizo linalotokea.

  Ni vizuri tukawa wazi kusema matatizo tunayohisi kwa wenzetu badala ya kuhisi tu na kudhani watayaona. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeshindwa jukumu letu la kupenda kwani tutakuwa tumejitazama wenyewe zaidi..
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Msingi wa ndoa ni upendo uliopo kati ya mwanaume na mwanamke. Na upendo ndiyo unaowaongoza watu kwenye kufunga ndoa (kujitoa kwa mwingine na kumpokea mwingine - matrimonial consent). Ni ukubaliano huu wa hiari wa watu wawili ndiyo unafanya ndoa iwe halali.

  Lakini ujue kwamba watu wa ndoa hawaishi kama mtu na dada yake au mtu na kaka yake. Hawa ni mume na mke! Kati ya majukumu na haki kubwa za wanandoa ni kufanya tendo la ndoa ambalo pamoja na kuwafurahisha wanandoa linalenga katika kushiriki kazi ya Mungu ya uumbaji (kuzaa na kulea watoto Mungu akiwajalia).

  Kumbe mtu akiwa ******* haruhusiwi kufunga ndoa iwe ya kiserikali au ya kidini. Hata ukiwa na upendo mkubwa wa aina gani kwa binti kama "mzee" hafanyi kazi huwezi kufunga ndoa ndugu. Kumbe upendo pekee hautoshi lazima pia uwe na uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Kwa nini? kwa sababu tendo hili ni la lazima katika ndoa. Hakuna mjadala. Tendo hili ndiyo alama ya juu kabisa ya upendo kati ya watu wa ndoa. Ndiyo maana limepewa heshima ya kuitwa "tendo la ndoa". Kwa watu wa ndoa ni tendo takatifu (sacred act)
   
Loading...