Tunajiandaaje na Tanzania iliyo mfano na Zimbabwe ya sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajiandaaje na Tanzania iliyo mfano na Zimbabwe ya sasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by omarilyas, Jan 17, 2009.

 1. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni wazi kuwa kama hali ya kisiasa itaendelea kama ilivyo sasa huku watawala wakiendelea na imani potofu kuwa CCM ni Tanzania na Tanzania ni CCM, ipo siku nchi yetu itafika walipofikia makamarade wenzetu wa Zimbabwe kama sio kufikia hali mbaya zaidi ya wao. Kwa mtazamo wangu mazingira ya nchi yetu kisiasa, kijiografia, kiuchumi na zaidi kijamii ni "vulnurable" sana kwa machafuko makubwa kuzidi yanayotokea kiongoni mwa majirani zetu

  Wakati Tanzania tuna nafasi kubwa ya kuwa Taifa la mfano kwa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, vilevile tuna uwezekano mkubwa wa kuingia(kujiingiza) katika machafuko makubwa yasiyo na kifani katika bara letu. Wakati tuna kila aina ya misingi muhimu ya maendeleo, vilevile tuna mazingira yote ya kufanikisha machafuko yasiyo na kifani...


  Naamini itakuwa vizuri sana kama tutatumia nafasi ya "usalama na amani" ya sasa kufikiria kwa undani hatua za kuchukua pale tutakapofikia hali mbaya kama ilivyo kwa "wenzetu". Kwa kifupi ni muhimu kuanza kuwa na mikakati makini ya jinsi gani ya kuepusha Tanzania kufikia hali mbaya kama ilivyo kwa wenzetu wa Zimbabwe pale ambapo tabaka tawala ndani ya CCM litakapojiona kuwa limepoteza kabisa uhallali wa kutawala na lipo hatarini kuondolewa kidemokrasia na vyama vya upinzani. Ukweli ni kuwa ndani ya chama tayari kuna mikakati ya kukabiliana na hali ya kuondolewa madarakani lakini sidhani kama miongoni mwa asasi za kidola na kijamii mikakati hiyo ipo ama hata kama imeshafikiriwa. Ni wazi tuna nafasi kubwa ya kuepuka na yanayotokea mahala pengi barani Afrika kama tutathubutu kujiandaa kutoka sasa badala ya kusubiri tufike huko kwanza......

  Tusisubiri MAFISADI wakageuka Warlords ndipo tuanze kufikiria....tuthubutu kufikiria sasa jinsi gani tutajiepusha na yanayokuja...


  Nakaribisha maoni ndugu zangu watanzania...

  Tanzanianjema
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tusubiri mpaka walioko jeshini au wanajeshi wetu wengi waone kama wanaowalinda ni ngugu na jamaa zao ambao haki zao zimetekwa na wachache na viongozi au chama hiki cha CCM ambacho kipo madarakani kwa kwa karibu nusu karne kinawanufaisha wachache huku walio wengi wakiwamo wao wenye hati miliki ya kumiliki siasa wanadanganywa.
   
Loading...