Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Tunajenga “Moral less, value less and ethical less political society”
Tanatengeneza viongozi na jamii ambayo kwayo hakuna jambo lolote ambalo ni baya wala zuri na hakuna jambo linalokubalika au kutokukubalika.
Kwa taifa tunalojenga, uzuri au ubaya wa jambo haupo kwenye jambo lenyewe bali kwenye ‘Nani ni mnufakika na nani ni muathirika kwa uangalia usoni”. Kanuni inaayotumika kuamua ni rahisi lakini hatari sana. Kanuni hiyo ni ‘lolote ninalofanya mimi au linalofanyika kwa maslahi yangu ni sahihi na linakubalika na lolote analofanya mwingine au linalofanyika kwa maslahi ya mwingine si sahihi na halikubaliki’.
Kwa hiyo kama taifa tunashindwa kusema vitu 1,2,3 ni tatizo na havikubaliki bila kujali mfanyaji ni nani na mwathirika ni nani, na vitu 1,2,3 vinakubalika bila kujali mfanyaji ni nani na mwathirika ni nani.
Hali hiyo hupelekea kitu ambacho mtu anakipinga kwa mtu A tukio A akitetee kwa mtu B kwenye tukio hilo hilo au linalofana. Na hili ni kama vile amma hatulioni, au tunaliona lakini kila mtu anapuuza kana kwamba halipo, au ni jambo la kawaida.Lakini katika uhalisia wake ni moja ya mzizi wa matatizo makuu yanayotukabili na kama tutaendelea kuchukulia tabia hii kama jambo la kawaida, madhara yake yatakuwa serious Zaidi.
Kwa mfano, umevamiwa na vibaka, unalaani na unataka wachomwe moto, baadae mwanao anavamia na kuiba kwa jirani, unasema acha kijana aibe, kwani jirani hakujua wizi upo, kwa nini hakuweka walinzi? Yaani hatuoni kama tatizo ni kile kinachofanywa bali tunafikiri tatizo ni nani kafanya na nani kafanyiwa.
Aidha, katika mazingira hayo bado tunaamini tutamaliza tatizo la msingi, tunasahau kwamba wakati mmoja anaona ni tatizo na anazuia mwingine anafikiri ni sahihi na anahimiza kutokana na upande aliopo kwa wakati husika. Ni sawa na mlango ambao wakati mmoja akifungua mwingine anafunga na nyote mnaamini ipo siku huo mlango utafunguka.