Tunajadili Bajeti,Tunaizika EPA,Richmond: Lakini Je,Tunayajua haya?

Korosho

Senior Member
Nov 30, 2007
132
29
Tunajadili Bajeti: Lakini wanasiasa wanayajua haya?
Na Charles Kayoka
Mwananchi

WAKATI huu tunapoijadili bajeti sijui kama wanasiasa na watunga sera wetu wanalijua hili ninaloandika hii leo. Nilikuwa ziarani mkoani Rukwa hivi karibuni kwa ajili ya kujadiliana na waaandishi wa habari wenzangu kuhusu namna ya kuandika habari za kupunguza au kuondoa umasikini, kama sehemu ya jukumu la waandishi wa habari katika jamii, na katika kuisaidia serikali.

Moja ya kazi tuliyoifanya ni kujaribu kuainisha nani masikini, na nani sio masikini. Tuliamua kutembelea maeneo kadhaa ya mjini Sumbawanga kujaribu kubainisha nani ni masikini na nani siye. Tulichokikuta huko mtaani ni cha kutisha, na tunajiuliza, hivi tunapojadili bajeti na kusema kuwa bajeti hii ina nafuu, serikali na wananchi wenzetu wanajua hali halisi ya kiwango cha umasikini kinachowakabili waanchi huko vijijini?

Tulikutana na dada mmoja ambaye anaishi na mdogo wake katika familia ya mume na watoto wanne. Dada huyu anafanya biashara ya kuuza mafuta ya alizeti kwa mtaji mdogo sana wa Sh30,000. Faida yake ni Sh1500 kama atafanikiwa kuuza, na fedha hiyo itumike kulisha familia. Haitoshi, lakini si hilo tu, bali alitueleza kuwa mdogo wake ana akili sana shuleni na anahofu, narudia, anahofu kuwa atafaulu masomo yake ya shule ya msingi, na kama atafaulu atatakiwa kugharimia vifaa, matumizi, na kuchangia gharama za masomo.

Dada anasema kuwa hawezi na kama kuna kikombe anachoomba Mungu amuepushie asinywe ni kumlipia masomo mdogo wake. Fikiria, huku tunazungumzia kuwa watoto wetu na hasa watoto wa kike wananyimwa fursa ya kusoma kwa sababu ya mfumo dume, lakini kumbe umasikini unawafanya akina mama wenyewe washindwe kuwapeleka watoto wao shule na wanaogopa kusikia taarifa za watoto wenye akili sana.

Dada mwingine akatueleza kuwa anauza karanga za kuchemsha. Kipato anachopata hakimtoshi kabisa, kwa maelezo yake. Napoamuka asubuhi hana chakula cha kula zaidi ya kuchemsha karanga, kunywa chai kwa kitafunio hicho. Anasema yeye na watoto wake hushindia chakula hicho.

Hiyo ndiyo hali inayowakabili watoto wengi wilayani Sumbawanga. Kama kuna jeshi kubwa la watoto wa mtaani wanaouza karanga, kusukuma mikokoteni, kufanya kazi za harubu kwa ujira mdogo, basi Sumbawanga ni moja kati ya miji inayoongoza Tanzania, kwa mtazamo wangu. Watoto wanashindia maji na kula mlo mmoja kwa siku, wenyewe wanaita �kupiga picha za pasipoti.�

Maisha ya familia nyingi, kwa kadri tulivyowatembelea ni duni sana na hakuna uhakika wa kupata hata mlo mmoja kwa siku. Tulimtembelea mama mmoja ambaye mumewe ni fundi wa majiko ambayo huyauza kwa Sh4000, kama yakiuzika (mara nyingi huuza jiko moja kwa siku au akose kabisa).

Mama hutengeneza mazulia ya mlangoni ambayo nayo soko lake ni adimu. Mama huyu anasema hana ardhi ya kulima na maisha yake ni duni. Na kwa kumwangqtalia unaweza kuona jinsi utapia mlo ulivyomkabili na hata unamhurumia kwa kunyonywa na mtoto ambaye sidhai kama alikuwa anapata kitu chochote.

Kule nyumbani tulikutana na majirani ambao, kwa maelezo yao, ule mlo tuliowakuta wakijipatia, saa tisa mchana, ndio ulikuwa wa mwisho na hivyo walikuwa wanapiga picha ya pasipoti hadi kesho yake.

Kuna maelezo ya wakulima ambao kwa kushindwa kumudu gharama za maisha huwaomba mikopo ya fedha majirani wanaojiweza, wafanyakazi au wafanyabiashara, kuomba msaada wa fedha.

Madeni haya hawawezi kuyalipa kwa fedha na hivyo husubiriwa walime na wakati wa mavuno hulipa deni kwa mazao, na kujikuta wanabaki patupu aidha wafanyabiashara huwakopesha nguo, mbolea, na pembejeo zingine wakulima hawa masikini na kwa njia hiyo kuwalazimisha kulinunua shamba la mkulima kijanja kwani wakati wa mavuno mfanyabishara hulichukua shamba lote ili kufidia misaada na mikopo ya fedha waliyokuwa wakitoa kabla ya mavuno. Matokeo yake ni yaleyale, wakulima hubaki patupu mwisho wa msimu wa mavuno.

Serikali katika MKUKUTA wanasema, katika moja ya mkakati wa kuimairisha kilimo, watawahamasisha wafanyabiashara binafsi kununua mazao ya wakulima ili kupanua soko la mazao. Kama nilichoona kule Sumbawanga ndicho hicho cha wakulima kuahadiwa na wafanyabiashara, huo mkakati umefeli na tuanze upya.

Nadhani nilichokiona Rukwa ni kioo cha hali halisi ya maisha vijijini. Kuwa umasikini si tu kwamba umeshindwa kutafsiriwa na watunga sera bali pia mikakati ya kuutokomeza umasikini si tu kwamba haitoshi, bali haipo. Kama tulidhani mikopo ya wafanyabiashara ndogondogo, na SACCOS, au PRIDE au FINCA tulidhani inaweza kututoa kutoka umasikini basi hiyo ni ndoto kwani wengi wa wale tuliokutana nao walisema �nikikopa nitalipa nini?� Hana pato na wale wanaofanya biashara kipato chao hakitoshi hata kwa mlo mmoja, achilia hiyo ya siku nzima.

Bajeti hujadili fedha, vyanzo vya mapato na ahadi ya kuleta maendeleo; sisi wa huku mjini tunasema kuwa bajeti ni nafuu kwa vile mafuta na vitu vingine muhimu havikutozwa kodi, lakini huyu mwananchi wa Rukwa mateso yake hayatokani na kupandishwa au kutopandishwa kwa kodi katika mafuta na bidhaa muhimu, bali umasikini wake unatokana na kushindwa kwa sera na utekelezaji wake, kama sio usimamizi. Inatokana na watunga bajeti kushindwa kubeba sauti za wakulima masikini ili wajue nini watu hawa kinawasibu ili kutambua kuwa kama mikakati ni kutoa mikopo, basi haifai kama si kuwa haiwezekani; kama ni kupelekea pembejeo kupitia wafanyabiashara basi, imeshindwa. Wengi tunaujadili umasikini katika mitatazamo ya watu tunaoishi mjini, kukosa fedha za kununulia.

Ingawa kule kijijini sababu ya umaskini ni kukosa fedha, lakini hicho ni kigezo cha juu juu tu. Hicho ni kiashiria cha kushindwa kwa mfumo mzima wa kuwapatia nafuu ya maisha. Bajeti haisaidii chochote na kama tunafikiri inasaidia nadhani tunakosea sana.

Ni pendekezo langu kuwa mfumo mzima wa bajeti lazima ubadilike ili kuweza kuakisi mahitaji halisi ya wale walio pembezoni kwa mfumo badala ya kutunga bajeti kwa kufuatia mifumo (templates) ambayo haionyeshi ukweli halisi wa maisha ya wananchi na hasa masikini.

Huu si wakati wa kufuata mfumo mgando wa utungaji bajeti, nadhani tunatakiwa kujadili mfumo wa bajeti upya, wadau wote, kabla ya kuisubiri tu mwezi wa sita ikisomwa.
 
CHENGE, KARAMAGI, ROSTAM, MRAMBA, MKAPA, YONA NA JEETU PATEL MNAYASIKIA HAYO??????????????????????????????
 
Back
Top Bottom