Tunaitaka tanganyika yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaitaka tanganyika yetu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOUGLAS SALLU, Feb 10, 2011.

 1. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Jamani Zanzibar ni nchi kamili, ina serikali yake, bunge lake, bendera yake,wimbo wake wa taifa, ina vikosi vyake vya ulinzi na usalama(majeshi),kwa hiyo hii ni nchi kamili, swali langu ni kuwa kwanini watanganyika tunakuwa dhaifu kushindwa kurudisha utaifa wetu badala yake tunaona fahari kujiita watanzania wakati kimantiki hakuna nchi inayoitwa Tanzania kwani Zanzibar imeendelea kubaki kuwa taifa huru na hiki kinachoitwa Muungano ni usanii tu.Matokeo yake nchi ya kigeni inayoitwa Zanzibar imejipenyeza katika nchi yetu mpaka kuwa na wabunge kwenye nchi yetu tena wanakuwa na guvu kuliko sisi wenye nchi. Naomba wanasheria wasaidie kuhoji uhalali wa muungano huu feki.
   
Loading...