Tunaitaji wafanyakazi jasiri kama huyu asiye na nidhamu ya uwoga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaitaji wafanyakazi jasiri kama huyu asiye na nidhamu ya uwoga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,147
  Likes Received: 5,576
  Trophy Points: 280
  SHUTUMA DHIDI YANGU (AFRICAR KAGEMA) KUTOKA SALES TEAM

  Ni wajibu wetu sote kutambua kuwa biashara sio siasa na aihitaji mambo ya kisiasa badala yake inahitaji uwajibikaji na uzalendo kwa kila mmoja wetu kwa nafasi yake, kwa kutumia elimu yake na upeo wa uelewa wake kuhakikisha kampuni inayofanya biashara ya faida iweze kufanya hivyo kwa manufaa yetu sote.

  Kabla sijaeleza yaliyojiri siku ya jumamosi tarehe 26/09/09 kwenye mkutano wa wafanyakazi uliohusu kupunguza wafanyakazi, napenda kusema kuwa nimesikitishwa na nimefedheheshwa sana na majibu ya shutuma yaliyotolewa na sales team kujibu hoja ambazo sikuzitoa kwenye mkutano huo.

  Hoja zangu kwenye mkutano huo wa tarehe 26/09/09 zilizogawanyika katika mada mbili ambazo nilizitoa kwa maadishi ambayo nakala yake wanayo COWTU zilikuwa ni;
  i. Kutopunguza Wafanyakazi
  ii. Kupunguza Wafanyakazi

  Katika maelezo haya nitaijadili mada moja tu yaani Kutopunguza wafanyakazi ambayo sales Team wameijibu kama ifuatavyo;

  KUTOPUNGUZA WAFANYAKAZI

  1. MAPATO
  Mimi nilipingana na zoezi la kupunguza wafanyakazi kama kigezo cha kupunguza gharama za uendeshaji wa kampuni badala yake niliomba kampuni kufanya yafuatayo ili kuongeza mapato na kupunguza gharama za kampuni;

  a) Kuimarisha (Kuboresha) Vituo vyake vya Mauzo
  Nilitoa rai kwa kampuni kurekebisha vituo vyake vya mauzo ili kukabiliana na ushindani uliopo katika soko. Nikitolea mfano wa vituo vya ATC House na Interline sales counters ambavyo mazingira yake yanakuwa kana kwamba Air Tanzania haina ushindani wowote katika soko hivyo kwa mazingira yoyote yale wateja watakuja tu kununua tiketi.

  b) Kupunguza tiketi za bure yaani Liberty
  Nilishauri kampuni kupunguza kutoa tiketi za liberty kwa wafanyakazi na management na watu wengine kwani tiketi hizi ndizo chanzo cha kupungua kwa mapato kwa kampuni. Niliendelea kusisitiza kuwa liberty hazina control yoyote na watu wa Fedha (Finance) hivyo hakuna mtu anayejua kuwa kampuni inapoteza kiasi gani kwa siku, Mwezi au Mwaka kutokana na tiketi hizi. Nilitolea mfano kuwa tiketi hizi zinatolewa na watu wa record na Commercial bila kuwahusisha watu wa Finance hivyo kutojua hasara inayopatikana.

  c) Kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Air Tanzania na Travel Agents ndani na nje ya nchi.
  Nilikubushia kuweka uhusiano mzuri kati ya Air Tanzania na Travel Agents wa ndani na nje ya nchi kwani travel agents wanachukua nafasi kubwa katika mapato ya kampuni.

  Uhusiano wa Ndani.
  Nikielezea uhusiano wa ndani niliwakumbusha watu wa Commercial kuwa wanapaswa kutoa majibu yanayojitosheleza kwa travel agents kuhusu masuala yanayohusu uhasibu au BSP na kama wanaona hawana utaalam nayo wanapaswa kuniuliza ua kumuuliza mtu wa BSP kwa sasa AFRICAR ili wapate majibu sahihi badala ya kutoa shutuma kuwa mtu wa BSP ndiyo kikwazo cha matatizo yao.
  Nikielezea kuhusu matatizo yanayojitokeza mara kwa mara ya refunds wakati mwingine zinachelewa kutokana na utaratibu niliojiwekea kwamba lazima zichunguzwe na watu wa Help desk au Mama Kikowe na kuzifunga kwanza ndipo nizifanyie kazi. Vilevile ifahamike kuwa wakati mwingine tiketi hazionekani kwenye system kwa hiyo mimi (Africar) na watu wa help Desk inabidi kuomba msaada kutoka SITA, ATLANTA AU MERCATOR ili kujua status zake.

  Uhusiano wa nje.
  Niliikumbusha kampuni kuangalia upya soko la South Africa kwani mpaka sasa Travel Agents wanadai ZAR 1,269,618@ 168 = TZS 213,295,824 credit card refunds ambazo zitaisumbua sana kampuni ikianza safari zake huko. Kampuni itambue kuwa deni hili halijalipwa kwa muda mrefu tangu December 2008.

  d) Kulifanyia Matengenezo jingo la ATC House.
  Nilitoa wito kwa kampuni kulifanyia matengenezo jengo la ATC House ili lipangishwe kwa kutangaza tenda na makampuni makubwa tu ndio yapewe nafasi yatakayoweza kupanga floor nzima ili kuweza kupata pesa nyingi kwa mkupuo kuliko hizi pesa ndogo ndogo tunazopata kwa sasa.
  Nilipendekeza ukarabati ufanyike ili kubadilisha mabati juu ya paa ambayo yameoza na yanavuja hivyo kuleta usumbufu kwa wapangaji ikiwa ni pamoja na mabomba ya maji machafu.
  Vilevile nilipendekeza wafanyakazi wa ATC House wahamie Mezzanine Floor kama ilivyokuwa zamani na kupangisha ghorofa ya kwanza,pili na Tatu.

  e) Mikataba Mibovu
  Nilitoa ushauri kwa kuirekebisha mikataba yote mibovu na inayopunguza mapato ya kampuni kama vile mikataba ya Miss Tanzania ambayo ni dhahiri kuwa haiinufaishi Air Tanzania badala yake inawanufaisha hawa Miss Tanzania na wenzao. Ni ukweli usiopingika kuwa Miss Tanzania inaitangaza Air Tanzania wakati wa mchakato wa kumpata Miss Tanzania tu lakini baada ya hapo hawaisaidii kampuni hii, hivyo wanapanda ndege bure tu. Niliomba mikataba hiyo iwe ya kipindi Fulani tu hasa wakati wa mchakato.
  Vilevile mikataba ya Clouds FM ambayo nayo sio kila siku inaitangaza Air Tanzania, lakini wafanyakazi wake wanatumia liberty kila mara.
  Hivyo ni wajibu wa kampuni kuangalia upya mikataba kama hii ili kuinusuru kampuni na kuongeza mapato yake.

  f) Kuimarisha Kitengo cha mawasiliano.
  Nilitoa wito kwa kampuni kuimarisha kitengo hiki ili wateja wetu wapewe maelezo au taarifa mapema inapotokea mabadiliko yoyote katika ndege zetu. Nilitolea mfano wa abiria ambao walijikuta wanasafiri hadi Kigoma wakati wao walikuwa wanaenda Tabora kwenye mkutano. Nikitolea mfano kama huu hapa chini,
  Dear Rashida,

  First of all may I take this opportunity to apologize for the inconveniences caused to our valuable customers due to unexpected schedule change of our flight to TBO.

  Please convey our sincere apologies.

  ATTN: Africar kindly processes ACM as requested and please waive all charges.


  MBWETTE/TOLLYPROF (PNR# ZV6KGU, TKT# 197 3360837165)
  VARISANGA/MODESTPROF (PNR# N62L3A, TKT# 197 336083716
  MARGESON/DALOTTAPROF (PNR# N62L3A, TKT# 197 3360837167

  2. MATUMIZI
  Katika kipengele hiki niliiomba kampuni kupunguza matumizi katika mambo yafuatayo;
  a) Kupunguza Duty Travel zisizokuwa za lazima kwa wafanyakazi na management.
  b) Kupunguza matumizi mengine yoyote yasiyokuwa ya lazima ili kuinusuru kampuni na gharama zisizokuwa za lazima na kubana matumizi ikiwa ni pamoja na mikataba mibovu.  KUJIBU TUHUMA ZA SALES TEAM

  Kwanza ni matumaini yangu kuwa kwa wale waliokuwepo kwenye mkutano huu watakubaliana na mimi kuwa hayo maneno na lugha iliyotumika haikuwepo kwenye mkutano ule. Vilevile ukisoma kwa umakini sana utagundua kuwa hawa watu wanageneralize tuhuma zao na hawako specific kwa kila kauli wanayodai kama vile
  Quote ‘’Sales wamebweteka tu na hawafanyi kazi yoyote, hawana uhusiano mzuri na Ma-Ajenti wanao tuuza. Pia Sales hawajui wafanyalo wanaleta mkongamano na BSP/Agents, na kwamba tuje kwako utufundishe kazi. Hizi ni shutuma nzito na zinatia karaha, hasa kutoka kwa mtu kama wewe Afrika.’’

  Napenda kusema kuwa hizi kauli hazikutolewa na mtu yeyote kwenye mkutano huo. Hivyo huku ni kupotosha jamii ya ATCL hasa ambao hawakuhudhuria mkutano huo waelewe hivyo. Hizi ni hadithi za kutunga kwani hakuna binadamu mwenye akili timamu anaweza kutamka maneno haya.

  Quote ‘’Sisi tunaichukulia kuwa hukutoa shutuma hizi kwa nia njema ya kujenga, bali kama kawaida yako, lazima ukosoe ili uonekane unajua, hata ikibidi kuwadhalilisha viongozi wa juu sana kwako.’’

  Napenda kusema kuwa kwenye mkutano ule hapakuwa na kukosoa kwa mtindo huu unaoelezwa hapa juu kwenye quote na hakuna shutuma zozote zilizotolewa ingawaje kulikuwepo na kukumbusha wajibu wetu kama wafanyakazi na viongozi wetu. Mimi binafsi sijawahi kumdhalilisha kiongozi yeyote wa juu ndiyo maana Sales Team wameshindwa kutaja jina la huyo kiongozi hapa ili watu watafakali. Nina imani kuwa viongozi wa juu huwa tunashidana kwa nguvu za hoja zinazojenga kampuni hii na wala si kudhalilishana, wafanyakazi ni mashahidi kwa hili.

  Quote ‘’Wengi wao akiwemo Four Ways Mwanza. wamekutaja kwa jina kuwa u msumbufu, una majibu ya jeuri, na hujali mchango wao katika shirika.’’

  Napenda kusema kuwa ni dhambi mbele ya Mungu kumsingizia mtu bila makosa. Mimi siwezi nikaijibu 4ways majibu ya jeuri naomba mtajeni mtu (specific person) ambaye nilimjibu jeuri ili tumuulize.

  Quote ‘’Ushauri wetu wa bure kwako nikuwa, jiulize, je ni miaka mingapi uko kazini na je umewahi kuvumbua lipi jipya katika kuboresha sehemu yako ya kazi. Kama ulivyojigamba kuwa wewe unajua sana mambo ya Sales, sasa, ukipenda kuhamia Sales itabidi uende shirika jingine kwa vile kauli zako kwa wafanyakazi wenzio, abiria na maajenti hazito endana na majukumu ya kazi za Sales za Shirika la Ndege Tanzania..’’

  Kauli hii sales Team wanaitoa wakati mwafaka ili viongozi wangu wa juu wanichukie bila sababu za msingi. Wanaitoa kauli hii wakijua kilichopo mbele yetu na ikiwa ni kuwakumbusha tu viongozi wangu kuwa wasilisahau jina hii AFRICAR KAGEMA katika idadi ya wafanyakazi 125 wanaoodoka na kuwakumbuka wao katika ufalme wa kubaki. Napenda kuwahakikishia watu wa Sales Team kuwa mimi si mtu ninayetishika na zoezi la kupunguza wafanyakazi kwani uwezo wangu unahitajika kila kona ya nchi hii.

  MWISHO
  Nikiwa kama mwanajamii wa ATCL ni wajibu wangu kutoa ushauri wakati wowote na mahali popote panapofaa ili kuhakikisha kuwa kampuni yangu ATCL inasonga mbele kwa faida yangu na Watanzania wote na Taifa kwa ujumla.
  Hata hivyo natoa wito kwa watu wenye tabia ya kujenga chuki miongoni mwetu waache mara moja ili kuijenga ATCL na sio kujijenga wenyewe binafsi kwa maslahi yetu binafsi mbele ya jamii. Hata hivyo mimi binafsi nawaheshimu sana wafanyakazi wenzangu na nitaendelea kushirikiana nao bila kinyongo hadi mwisho wa ajira yangu.

  ‘’Mungu ibariki ATCL, Mungu ibariki Tanzania’’  Imeandaliwa na;

  AFRICAR TONONO KAGEMA

  KWELI SHULE NI SHULE HATA UFANYE KAZI MIAKA MIA(100) KAMA HUNA SHULE YA KUKUSAIDIA LAZIMA UBAKI KULUMBUNA
   
 2. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa jhinsi nilivyosoma naona huyu mwandishi ana pointi ila tu tatizo ni kwamba watu ni very conservative, hasa hawa walio kwenye mashirika ya uma, hawataki kuendesha kampuni kibiashara especially kwenye karne hii kama anavyowashauri huyu jamaa, ila tu wanang'ang'ania mfumo wa zamani ili mradi tu wasitoke kwenye ile comfort zone yao, namna hii lazima shirika life, kama wafanya kazi ndo wa type hii, full majungu,full chuki na utendaji zero. Kweli bwana wakikuzingua au kukumwaga we timua, na haya uliyoyaandika hapa yatakusaidia kupata kazi , kampuni zipo kibao tu kama una skills and na maarifa. all the best
   
 3. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama tatizo kubwa ni Mtaji, hivi Uongozi wa wizara na ATCL hauni kuna kila sababu ya kuuza hisa za ATCL kwenye DSE(Dar es Salaam Stock Exchange) Kama kampuni ya wazawa (NICOL) walivyo fanya wakati wa kununua hisa za NMB? Mhe. Dr. Shukuru Kawambwa kaza msuli Shirika lisikufie mikononi mwako!!!!!!! itakuwa ajabu kwa Waziri wa Miundo Mbinu Msomi kushinda wote katika historia ya Tanzania kufiwa na Shirika la Ndege ambalo ni National Carrier (Pride). Hebu onyesha nguvu ya Doctorate(Phd.).
   
 4. l

  lambie Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naombeni number ya simu ya huyo mwandishi nimpe kazi haraka....she is intelligent. ATCL majungu sana pale. hawana vision
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Hili ni shirika la umma au mali ya mtu? Naona hakuna nidhamu, haishangazi kuwa nidhamu toka juu hamna!
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hapa si pahala pa hii thread. Kwa kuibakiza hapa panaipunguzia makali. Ingepelekwa kwenya Habari na Hoja.

  Amandla....
   
 7. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli huyu jamaa kaonyesha ujasiri lakini wale wazee wanaozeekea madarakani hasa kwenye mashirika ya umma ni ukiritimba mtupu umewajaa.Lazima huyu ndugu atapigwa vita sana kwa kuwa ametoa ushauri wa kuwapunguzia maslahi yao. Sasa basi kama ana evidence ya mikataba mibovu aifumue iweze kufanyiwa kazi vinginevyo wanaweza kumng'oa kabla.Ndo maana ATCL haindelei kabisa. Shenzi sana hawa.
   
 8. C

  Chief JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  super!!
   
 9. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  inaonyesha ni namna gani shirika likipewa ni la umma linavyotafunwa,unakuta mfanyakzi wa atc pamoja na matatizo yoote hayo still wanatanua sna marurupu yoote,kudhamini miss tz, etc ni upuuzi, hiyo ni failure ya wanaoteuliwa,humo ndani wapo wazee wa miaka 100 what are they doing?what new do they have to the organisation?futa kzazi chote,weka mngt mpya, piga kazi!! au precision wanawaloga nini? watazania tuna matatizo sana mali ikishakuwa ya umma, no responsibility, shidaa si wingi wa wafanyakazi, ni poor running and mngt, kwanza kama mnaajiri watun wanaovuta modomo wateja hatutakuja kwenu! ful stop! even precision bado hamjaajiri customer oriented people, hili ni jambo muhimu, hawawezi nini? they dont work hard basi!!
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Watu kama huyu jamaa ndiyo wanatakiwa kupewa kazi ya kuongoza SHIRIKA. Halafu mwingine atakuja na kusema "sisi hatuna akili" kumbe si kweli. Njaa na UFISADI na UTINDIA akili wa Mizee iliyochoka kama Jogoo lilimaliza mapigano, ndiyo inakuwa mzizi wa fitina. Huku ikiwa na nguvu ya Rais au Waziri wa sehemu hiyo, itakaa pale wee hadi siku kampuni itakuwa IMEKUFA na kuzikwa. Hapo itasubiri ihamishwe sehemu nyingine.
  Mtu kama Mustafa Nyang'ganyi, hivi huyu atakumbuka kwa lipi hasa zuri alilifanyia TAIFA LA TANZANIA? Mkapa yeye tutamkumbuka kwa UFISADI na wizi wa ajabu ambao umelitia taifa pabaya. Mtu hizo hela zote utaenda nazo AHERA?
  Watoto wa JKN hadi kesho watasimama kila kona na kujisifia ushujaa wa baba yao. Hivi watoto wa Mkapa wanaweza kusimama sehemu na kujisema "sisi watoto wa Mkapa?" Watoto wa Lowassa, RA, na wengine ambao kwa sasa wako madarakani ila siku wakitoka nao aibu zao zitawekwa wazi? Huu ULAFI mwingine huu!!!!!
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,147
  Likes Received: 5,576
  Trophy Points: 280
  Kweli inaumiza kweli....watu wanapoendelea kulitafuna hili shirika embu niwape nilichosikia leo mpaka nimechoka

  bodi ya atcl imekuwa ikichukua million kumi kwa ajili ya vikao vya kujadili mafao ya watu...wakati wafanyakazi inasemekana mpaka leo hawajalipwa...
  Hawa bodi wamekuwa wakigawana million kumi kila kikao na inasemekana ni siku ya 5 bado wanaendelea ...kugawana jk r u serious na hii kampuni kweli
  kama unamua kuiua si uitangazie umma.......bogus watupiu watu wamejazwa kwenye position bila shule kisa kumjua mtu ama kutoa uc345i
   
Loading...