kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,305
- 12,600
TBC ni chombo umma wa watanzania kinachoendeshwa kwa Kodi za watanzania wote. Ninamshukuru waziri mwenye dhamana ya michezo, waziri wa habari na mawasiliano na Mkurugenzi wa TBC kwa kuwafikiria matajiri wao (walipa Kodi) kuwaletea matangazo ya moja kwa moja kutoka Qatar, ahsanteni sana kwa kuwaza jambo hili. Labda shukrani nyingi zaidi ziende kwa Rais Dr. Samia kwa kuruhusu hili lifanyike kwa kutumia Kodi za wananchi, umeupiga mwingi kwakweli.
Lakini shughuli nzima ilikuwa na mapungufu yafuatayo.
1. Kukosekana kwa baadhi ya mechi. TBC haikuonyesha mechi zote, kama vile ilikuwa inatufanyia hisani TU watanzania kwa kutuchagulia mechi ipi tuangalie na ipi tusiangalie.
2. Kuchanganya channel ya matangazo ya taifa na michezo pamoja. Tulitegemea TBC ingekuwa na channel ya sports ili kuepuka kuchanganya matukio ya kitaifa na serikali na michezo.
3. Wachambuzi wa mpira hawakuwa na ubora. Wanaborongaboronga TU wakati hii ndiyo TV ambayo ingetakiwa na Quality wachambuzi.
4. Watangazaji wa mpira. Hawakuwa na mvuto zaidi ya kujua kiarabu TU. Hawavutii kuwasikiliza, unatamani waache kusimulia ili tuangalie TU wenyewe.
Ushauri: Sisi ndio wenye TBC, hivyo matangazo ya mpira lazima yawe ALL or NONE, sio vuguvugu kama vile. Bora muache kabisa ili watu wajioange kuliko vile. Chukueni wachambuzi ikiwezekana kutoka media nyingine binafsi. Kulikuwa na ugumu gani kutumia channel ya TBC2 au nyingine kwa michezo TU?
Ahsante ni TBC