Tunaipenda nchi yetu ndio maana yaliyotokea tena Afrika Kusini, tulishauri

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Tunaitwa sio wazalendo wa Taifa hili,sababu ya ukosoaji wetu na ushauri wetu kwa Serikali.

Baada ya ndege yetu kuachiwa Afrika ya kusini ,watu walifurahi tuu ,na kutoa maneno ya kejeli .wengine tulifurahi ila tulitaka suluhu ya kudumu .

Ndio maana tar 14/Septemba/2019 ,nilishauri haya kupitia gazeti la Tanzania,Daima.

Abdul Nondo,

Niliposema mh.Kabudi aliyekuwa waziri wa katiba na sheria sasa waziri wa mambo ya nje na
AG (Attorney General) kuwa wanapaswa kushtakiwa nilimaanisha na kama hawatachukua hatua
madhubuti ambazo nitazitaja hapo chini,wanapaswa kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi wa nchi
yetu,kwa kuchafua taswira ya nchi yetu kwa kufanya tuzidi kuwa taifa ambalo mali zetuz itawindwa kila kona ya dunia yetu.

Suala la kuachiwa ndege yetu huko Afrika ya kusini iliyozuiwa kwa agizo la mahakama tarehe2 1/August/2019 baada ya mfungua shauri hilo Bwana Hermanus Phillipus Steyn kupata agizo la
mahakama (Ex parte order) kuzuia ndege yetu ,suala hili linapaswa kuwa funzo kwetu na siok uishia kicheko , vifijo na kusifu bila kuwaza kesho nyingine juu ya usalama wa mali zetu kamat aifa .

Kwa wasio elewa wataishia kucheka, kufurahi na kusifu baada ya ndege kuachiwa bilak uwaza juu ya kesho ni wazi fikra zao ni tofauti kabisa na fikra za watu wengine kama sisia mbao tunaitwa sio wazalendo ila moyo wetu una farijika ndege yetu kuachiwa isipokuwa fikra
zetu zinawaza zaidi kesho baada ya leo juu ya usalama wa mali zetu ,taswira ya nchi yetuk imataifa na Imani ya wawekezaji katika taifa letu.

Bila kupepesa macho suala la kuachiwa ndege yetu iwe nafasi kwa viongozi wetu kuzidik uangalia namna bora zaidi ya kuendelea kulinda maslahi ya taifa letu kwa kufuata taratibu nan jia ambazo hazitaleta taswira mbaya kwa taifa letu na kwa kuhatarisha maslahi zaidi ya taifa
letu.

Tuelewe vyema kupitia suala hili la Bwana Steyn ,kukamatwa kwa ndege yetu haikuwa nam aana ndege yetu ndio ingechukuliwa,bali bwana Steyn alipewa ex parte injunction ya kuzuian dege yetu bila ya upande wetu kutokea au kuwepo(inter partes).Baada ya upande wetu( Tanzania) kujitokeza wakapeleka maombi ya kuondoa exparte injunction kuwa Arbitral award ambayo bwana,Steyn aliipata tarehe, 9/Julai/ 2010 na ambayo anataka ku -enforce haipo
kwasababu ilikufa tangu alivyoingia makubaliano ya malipo na Serikali(Deed of settlement)
tarehe 17/Julai /2012 na yakasajiliwa kama order of the court 18/Julai/2012 kwa kukubaliana
kulipa kutoka USD milion 36 hadi USD 30 .


Hivyo mahakama pamoja na mambo mengine ,jambo kubwa ilikuwa kwamba bwana Steyn
amefungua ku -enforce arbitral award ambayo tayari ilikufa tangu alipoingia makubaliano na serikali,hivyo sio arbitral award bali ni "Consent order" ambayo inataratibu yake na kwa
alivyofungua mahakama haiwezi ku-enforce kutokana na sheria ya kimataifa ya usuluhishi no.15
ya 2017 (International arbitration Act 15 of 2017).


Hoja yangu nikuendelea kusisitiza kuwa,kurudi kwa ndege yetu ni jambo kubwa na jema kama
taifa .Ila inapaswa kuwa fursa kwa viongozi wetu kuangalia namna ya ku-deal na haya mambo
ya kamata kamata ya mali zetu(ndege) kwa kupunguza ubabe na kuingia katika njia za
diplomasia zaidi,taarifa kuendelea kutolewa kuwa mali yetu imekamatwa,ndege yetu
imekamatwa haileti sura nzuri kwa taifa hata kimataifa.


Leo hii Bwana Steyn ameshindwa kwa hizo technicalities na erros (makosa ya kiufundi katika
sheria) ,ila madai yake hayajafutika bado yapo pale pale ambayo aliridhiana yeye na serikali yetu
tarehe 17/Julai/2012 (deed of settlement) na kusajiliwa mahakamani kuwa Order of the court tar
18/Julai/2012 .

Je,tunajua anajipanga namna gani ilikuzuia mali zetu zingine au ndege zetu hapo
baadaye? , Kama mtu alivyoshindwa tuu akakata rufaa hapo hapo tunajua anajipanga namna gani
kuibuka tena? .Maswali haya ni muhimu sana kuulizwa na raia yeyote mwenye mapenzi mema
kwa taifa hili.


Tarehe 10,Novemba 2018 ,bungeni Mh.Zitto alimuuliza aliyekuwa waziri wa katiba na sheria
Prof.Kabudi kutaka kujua idadi ya kesi za madai ambazo tumefunguliwa nje tangu Novemba
,2015.Prof.Kabudi alisema tangu Novemba 2015 idadi ya mashauri yaliyofunguliwa ni 13 katika
mahakama mbalimbali ,ikiwemo Permanent court of Arbitration (PCA),London court of
international (LCIA),International center for settlement of investment Disputes (ICSID) pia
UNICTRAL ila nyingi hazijatolewa maamuzi ambapo jumla ya madai hayo gharama ni sh.dola
za kimarekani 185,580,009 .76 (zaidi ya bilioni 400 za kitanzania).


Kuna kesi nyingine
tumefunguliwa na Mr.Ayoub Farid Saab huko ICSID ,tarehe 16/April /2019 ambaye ni
mwenyekiti FBME Bank chini ya Netherland .Shauri hili limefunguliwa ni baada ya Tanzania
kudhamiria kuvunja mkataba wa uwekezaji septemba 2018 ,unaoitwa (Agreement on
encouragement and Reciprocal Protection of investments) kati ya Tanzania na Netherlands.
Hivyo viongozi wetu wanapaswa kuwa makini sana ,wanapaswa watimize majukumu yao bila
kutumia ubabe wowote sababu sisi bado ni wanachama wa mahakama mbalimbali za
kimataifa,tumeridhia sheria na mikataba mingi ya kimataifa ,tukitumia ubabe na nguvu wao
wanaangalia sheria zinasemaje,wanatufungulia kesi huko nje,maamuzi yanatoka tuwalipe na riba
,tukigoma wanaomba agizo la mahakama wanazuia mali zetu ambazo kwa haraka haraka ni
ndege zetu tuu.


Limetokea Canada ,chupu chupu limetukosa kosa Afrika kusini.
Kuhusu hili la Bwana Steyn juu ya madai yake kwa serikali ,kwa unyenyekevu mkubwa nina
shauri serikali kuwa bwana.Steyn afunguliwe hiyo( PI , prohibited immigration/zuio la bwana
steyn kuingia nchini ) ili apate kuingia nchini na serikali ifanye mazungumzo naye juu ya
kufanya malipo yake kwa namna itakavyo weza,sababu bila hivyo hatujui anajipanga namna
gani ili aje azuie huko baadaye,haijalishi ni kwa miaka mingapi ijayo ,ilimradi ana documents za
makubaliano ya malipo kati yake na serikali (deed of settlement) hatosita kufanya hivyo hata
ikiwa ni huko huko nje hata ikiwa ni kwa miaka mitatu,mitano ,kumi au ishirini mbele litabaki
kuwa deni tena lenye riba zaidi.Hivyo jambo jema ni serikali kuangalia namna ambavyo
itamalizia kulipa hiyo fedha isiyozidi USD mil.10

Pili, hili zuio kwa Bwana Steyn kutokuingia nchini inaweza kupelekea picha mbaya kwa
wawekezaji wengine huko nje kutokuja Tanzania kuwekeza au waliopo kuwa na hofu kwamba
labda na wao wanaweza kuzuiwa kuingia nchini na kuacha mali zao ,tunazidi kutengeneza hofu
juu ya hofu kwa mambo ambayo serikali ikiamua kuatatua inaweza tena kwa diplomasia zaidi ili
kuongeza hamasa kwa wawekezaji na kusafisha sura au taswira ya taifa letu kuwa Tanzania ni
sehemu sahihi.

Kutokufanya hivyo viongozi wetu kwa makusudi watasababisha maslahi ya taifa
letu kudumaa kutokana na hofu ya wawekezaji kuwekeza bila hofu katika nchi yetu .
Tatu,nina shauri migogoro mingi ya madai ambayo tumefunguliwa katika mahakama za
usuluhishi huko PCA ,ICSID,UNICTRAL na LCIA ambayo gharama yake ni bilioni 400
),tuimalize migogoro hii kwa njia ya mazungumzo na diplomasia zaidi .


Kwani hatujui kwa tukio
hili la Afrika kusini hawa watu watajipanga kiasi gani mara nyingine dhidi ya mali zetu .
Tunaweza kupuuza,kwa kusema maneno ya "tupo huru " " uzalendo" "Vita ya kiuchumi" huku
hatimaye wanashinda kesi na wanaendelea kukamata mali zetu ,tujitahidi kuangalia namna ya
kupambana na kesi hizo kwa njia ya diplomasia zaidi kuliko ubabe ili kutoa ujumbe kwa
wawekezaji kimataifa kuwa Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji na pia kufanya mali zetu
(Ndege ) kufanya safari zake kwa uhuru zaidi na salama bila hofu ya kukamatwa.


Kama tukiendelea kutumia nguvu zaidi.
Hawa walio tufungulia hayo mashtaka 13 wataendelea kusambaza taarifa mbaya dhidi ya taifa
letu kuwa sio sehemu sahihi ya kuwekeza na pia watajipanga zaidi dhidi yetu.Tuepuke
haya,Tuepuke kauli za kusema tupo huru zaidi ya kufikiri kufanya tutakavyo wakati kuna
mahakama za kimataifa ambazo na uhuru wetu tunaweza kushtakiwa na kuadhibiwa ,pamoja na
uhuru wetu kuna sheria nyingi za kimataifa ambazo tumeziridhia na tukizivunja tunashtakiwa
hata kama sio mahakama za ndani hata za nje na tunaweza kushtakiwa.


Usijiite upo huru kufanya
jambo lolote kama kuna sheria za kimataifa na kikanda umeziridhia ,utaishia kujidanganya pasi
sababu yeyote ya msingi .Unaporidhia sheria fulani ya kikanda au kimataifa mamlaka au uhuru
fulani wa nchi(state Sovereignty) itakuwa imepungua .
Shukrani

Abdul Omary Nondo.
0659366125.
Septemba 14/2019.

2220408_IMG_20191124_124113_797.jpeg
 
Ushauri mzuri Ila kwa sababu hawataki kusikia ukweli hautazingatiwa Ila matatizo haya ya kamata kamata hayataisha na taswira ya nchi inazidi kuchafuliwa
 
Ukimwina mwenye hekima anampa ushauri mzuri mpumbavu huenda naye ameanza kupoteza hekima, Mpumbavu hashauriki, haelimiki
 
Back
Top Bottom