Tunaipenda CHADEMA, ila Vijana wenzangu kuna mambo mengine tujitafakari kidogo

Bashiru alizindua data centre ya ccm kwa ajili ya uchaguzi,mkakisifia chama!Leo inakuwa nongwa upinzani wakifanya hivyo?
 
Habari wana JF, poleni kwa majukumu.

Leo ningependa kuzungumzia jambo ambalo kwa hakika limeniweka njia panda. Tunajua uchaguzi na mambo yote kuhusu uchaguzi kwa sasa yapo moto kwa kuwa tunaelekea mwishoni(zimebaki wiki 3).

Kuna mambo yameanza kujitokeza kwa kasi kwenye wiki hii ambapo tumesikia na wengine wameona kambi za wagombea Lema na Heche kuvamiwa.

Hili lilitarajiwa kutokea kwa kuwa watu ambao mpo nao kwenye hizo shughuli ndio watoa taarifa zote za kinachoendelea. Pia ku-recruit watu kwa ajili ya tallying centres sio jambo jepesi, ilipaswa mrecruit wapo ambao kweli wana uchungu na mapenzi na nyie.

Shida sasa wanaipata hao vijana na hakutakuwa na msaada wowote kutoka kwenu zaidi tu ya ku-tweet leo na kesho alafu ndio iwe imetoka hiyo.

Tunakumbuka 2015, Lowassa pia alikuwa na hao vijana kwa ajili ya kujumlisha matokeo ya CHADEMA, lakini mwisho wa siku wale vijana wote wakaishia mikononi mwa polisi na hadi leo hii bado wapo ndani, cha kushangaza waliokuwa wanamfanyia hiyo kazi kahama chama na sasa anasema chagua Magufuli.

Hakuna msaada wowote wanaopata wala hata kuzungumziwa tena hakuna, kwa kifupi wamesahaulika.

Hivyo ninawaomba vijana wenzangu ambao mnaipenda sana CHADEMA, sio kila kazi mnatakiwa kukubali kufanya, kuna kazi zingine ni za hatari na mwisho wa siku inakuwa hasara kwako binafsi.

Wanasiasa wakishapata madaraka au kukosa huwa hawakumbuki tena(hizi ndio hulka za wanasiasa karibu wote).

Hivyo chagueni kazi za kufanya, sio leo anakuja mtu kwa kuwa tu unamkubali anakupa kazi ambayo inaenda kukuweka matatizoni kwa sababu tu anakuambia eti unapigania ukombozi. Ukombozi ambao yeye na familia yake wanaishi vizuri wanalipwa mamillion ya pesa, wewe unaishia jela.

Poleni kwa wote yaliowakuta siku ya jana, pole sana dada yangu wa pale Arusha. Mkiwa humo ndani najua nafsi zenu zitajutia kwa kukubali kufanya kazi ambayo nyie hamkuwa na maslahi nayo.
Fake ID from Lumumba

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana unayoyasema yakawa kweli kabisa.
Ila Kama vijana woote throughout the history wangekua na mawazo Kama yako.

Nadhani hata Uhuru wa Tanganyika au wa huko Zanzibar ungekua hauja patikana mpaka leo hii.
 
Habari wana JF, poleni kwa majukumu.

Leo ningependa kuzungumzia jambo ambalo kwa hakika limeniweka njia panda. Tunajua uchaguzi na mambo yote kuhusu uchaguzi kwa sasa yapo moto kwa kuwa tunaelekea mwishoni(zimebaki wiki 3).

Kuna mambo yameanza kujitokeza kwa kasi kwenye wiki hii ambapo tumesikia na wengine wameona kambi za wagombea Lema na Heche kuvamiwa.

Hili lilitarajiwa kutokea kwa kuwa watu ambao mpo nao kwenye hizo shughuli ndio watoa taarifa zote za kinachoendelea. Pia ku-recruit watu kwa ajili ya tallying centres sio jambo jepesi, ilipaswa mrecruit wapo ambao kweli wana uchungu na mapenzi na nyie.

Shida sasa wanaipata hao vijana na hakutakuwa na msaada wowote kutoka kwenu zaidi tu ya ku-tweet leo na kesho alafu ndio iwe imetoka hiyo.

Tunakumbuka 2015, Lowassa pia alikuwa na hao vijana kwa ajili ya kujumlisha matokeo ya CHADEMA, lakini mwisho wa siku wale vijana wote wakaishia mikononi mwa polisi na hadi leo hii bado wapo ndani, cha kushangaza waliokuwa wanamfanyia hiyo kazi kahama chama na sasa anasema chagua Magufuli.

Hakuna msaada wowote wanaopata wala hata kuzungumziwa tena hakuna, kwa kifupi wamesahaulika.

Hivyo ninawaomba vijana wenzangu ambao mnaipenda sana CHADEMA, sio kila kazi mnatakiwa kukubali kufanya, kuna kazi zingine ni za hatari na mwisho wa siku inakuwa hasara kwako binafsi.

Wanasiasa wakishapata madaraka au kukosa huwa hawakumbuki tena(hizi ndio hulka za wanasiasa karibu wote).

Hivyo chagueni kazi za kufanya, sio leo anakuja mtu kwa kuwa tu unamkubali anakupa kazi ambayo inaenda kukuweka matatizoni kwa sababu tu anakuambia eti unapigania ukombozi. Ukombozi ambao yeye na familia yake wanaishi vizuri wanalipwa mamillion ya pesa, wewe unaishia jela.

Poleni kwa wote yaliowakuta siku ya jana, pole sana dada yangu wa pale Arusha. Mkiwa humo ndani najua nafsi zenu zitajutia kwa kukubali kufanya kazi ambayo nyie hamkuwa na maslahi nayo.
Lisu anawafanya maccm, mapolisi, tume na wadhalimu wote wajue hawajui chochote. Ni spana mdomoni, spana zaidi katika matendo. Spana! Spana! Spana. LISSU katupa msamiati mpya pale Kiluvya. Amemaliza hotuba kwa kusema "It's late, but it's okey. Tuko tayari kuingia magogoni.
 
Ni yeye Tundu Lissu 2020. Vijana tuko nyuma yako!!
Yaani mabumunda ya uvccm ya humu yote niliyapiga pini, nikifungua tu uzi najua huyu bumunda la polepole wala sio kamanda.

Mabumunda kazi yao kubwa ni kufokolewa.
 
Hivyo ninawaomba vijana wenzangu ambao mnaipenda sana CHADEMA, sio kila kazi mnatakiwa kukubali kufanya, kuna kazi zingine ni za hatari na mwisho wa siku inakuwa hasara kwako binafsi
Naiona hii post kama best thread kwa msimu huu
 
Back
Top Bottom