Tunaipeleka wapi heshima ya Bunge kwa ushabiki huu wa maspika na wenyeviti wa Bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaipeleka wapi heshima ya Bunge kwa ushabiki huu wa maspika na wenyeviti wa Bunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by naggy, Jul 3, 2012.

 1. n

  naggy Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 15
  Nilisikitishwa sana na udhaifu wa M/kiti wa bunge wa kikao cha jana jioni jinsi alivyokuwa mshabiki wa vituko bungeni hadi kupelekea kushindwa kuongoza kikao. Leo hali hii imejitokeza tena kwa M/kiti wa leo mh. Jenister Muhagama. Tatizo langu kwa viongozi hawa ni wao kushabikia malumbano yasiyo ya kujenga ya wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala. Kimsingi, Spika au m/kiti hapaswi kuegamia upande wowote ki itikadi. Lakini hawa wameshindwa kulisimamia hilo na ndo maana siku hizi kila siku wanajitetea kwa waandishi wa habari kuwa wao wanatenda haki ili tu wasihukumiwe vibaya na umma wa watanzani. Najiuliza bila kupata majibu. Hivi huyu Mwigulu Nchemba (mb) anatumwa na chama? Kwa nini katika kuchangia kwake anakwenda kinyume na kanuni za bunge na spika anayekuwepo anamwachia? Kwa mfano katika kikao cha leo, hoja iliyoyoko mezani ni ofisi ya rais utumishi wa umma,utawala bora na maadili. Mbunge anapoinuka ni lazima achangie hotuba ya waziri ambayo ndo hoja yenyewe, sio kuchangia hoja ya mchangiaji mwingine. Sasa mbunge anapoinuka na kuchangia hoja ya upinzani ambayo ni ki mantiki ni sawa na mchango wa mbunge mwingine inawachanganya wasikilizaji. Mtoa maoni ya upinzani hana muda wa kujibu hoja za wabunge kwa sababu kanuni haziruhusu. Nchemba kwa tabia yake hiyo anawalazimisha wabunge wa upinzani wajibu hizo hoja anazoaitoa ili asipotoshe umma, na hapa ndiyo vurugu mechi huanza. Jenister Muhagama alipaswa kulizuia hili na kumuongoza mbunge ajikite kwenye hoja kama alivyokuja kumwelekeza mwishoni. Ameruhusu marumbano yasiyo na tija yaliyopoteza muda wa bunge. Kwa hali hii ni lazima kiti kilaumiwe. Maoni ya kambi ya upinzani yatajibiwa na waziri husika wakati wa majumuisho. Kama chama kinamuona Nchemba ni hodari wa kuzima hoja za wapinzani basi wamshauri rais ampe wizara awe rais. Watanzania tunahitaji malumbano ya hoja zenye kujenga sio hizo za kinanchemba ambazo zinatuchefua na kutufanya tusione maana ya kusikiliza majadiliano ya bunge.
   
 2. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  sikio la kufa.....
  Wewe unafikiri wanaelewa hayo,pamoja na matusi yote anayotoa wenzio ndio wanamchangia na hela kumpongeza.Upuuzi huu wanaoufanya watakuja kuujutia miaka miwili ijayo! Ajidhaniae amesimama.........
   
 3. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  CCM kama UKIMWI hakuna TIBA wala Kinga
   
 4. B

  Beethoven JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wenyeviti wa bunge,spika pamoja na naibu spika watabeba lawama kwa kushiriki kukiua chama chetu CCM.Wanafanya upendeleo usiojificha mpaka wapinzani na wananchi wanashtukia,tumieniakili kidogo maana huku mtaani tunapata wakati mgumu sana kukitetea chama.Hakukuwa na sababu hata kidogo kauli ya Manyanya kuwa waliomtesa Dr.ulimboka walikuwa CHADEMA kuachwa maana hata mitaani tunaulizwa mtu akitaka kwenda kufanya uhalifu anavaa uniform za kumtambulisha tujibu nini!!Kama kuna tume inachunguza si bora tujitahidi tuchakachue taarifa kuliko kutoa kauli tata?Wana CCm tunaelekea wapi?
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  bunge au kijiwe kilicho jaa wahuni..kama unaweza kutamka maneno kama unawashwa, unakiherehere, unatafuta umarufu hilo ni bunge sasa..
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ccm wanaporoja tu wanaachiwa upinzani ukifanya hivyo m/kiti anawaambia wanawashwa wakae chini
   
 7. cedrickngowi

  cedrickngowi Senior Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi bunge limekuwa kijiwe cha wabunge wa CCM,ni kejeli na fitna zisizoisha but wananchi tunashuhudia na tutaamua hatma yao by 2015.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tanzania Hakuna maspika labda tukodishe kutoka nje
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ushabiki wa vyama bungeni unakera sana!

  Matatizo haya yamesababishwa na Chadema wao hoja za maslahi ya Taifa zinaenda bungeni zinapata support ya wabunge wote (CCM & Chadema + Upinzani) mwisho wa siku wana Chadema wana hijack wana claim ushindi. Katika mazingira kama hayo lazima kuwe na resistance na sasa tunarudi kule kule ambapo hoja ya serikali itapitishwa tu kwa nguvu yeyote hata kama haitakuwa na mantiki.
   
 10. t

  tara Senior Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nadhni Irani inaweza kutusaidia kwa hilo......
   
 11. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  tusimulaumu Mbunge yeyote wa CCM aliyeko Bungeni tuwalaumu waliopiga kura kwa kuwachagua: na hii ni fundisho kwa watu wote waliajifanya kuwa mstari wa mbele kwenda kuwapigia kura wa-bunge hao wa CCM bila kuzingatia watu wanao wachagua ni wa aina gani.

  Kuwa na Wa-Bunge wa aina ya akina Nchemba na Wenyeviti wake bungeni ni Bora mhimili wa Bunge ukafutwa kabisa.
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Labda ccm waombe kwani ni Chama marafiki na Iran
   
 13. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli Bunge limepoteza mvuto. Majadiliano yanayoendelea na ambayo yanachukua muda mrefu hayana tija kwetu sisi wapiga kura. Muda mwingi wabunge wako kwenye malumbano yasiyochangia chochote kwenye maboresho ya bajeti. Nasikia uchungu!!! Nashindwa nitumie maneno gani ku-express uchungu wangu. Waheshimiwa Wabunge wetu, hivyo ndivyo mlivyotumwa na wapiga kura wenu? I doubt.
   
 14. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,531
  Trophy Points: 280
  Ila ninaomba kuulia hivi kuna haja ya Bunge hili la vituko kujiita Tukufu?Hivi kuna utukufu gani wakati limejaa pumba,matusi na vijembe?Bunge limejaa mafisadi ,wala rushwa na wauaji wanao jilimbikizi mali wao wenyewe tu.Hivi kweli kuna haja ya Bunge kujiita TUKUFU?
   
 15. mwanamke shujaa

  mwanamke shujaa Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mm naomba watanzania wote bila kujali itikadi ,rookie nchi mikononi mwa ccm kwa kuwatumia savings wake bila kujali maslahi ya nchi.
   
Loading...