Tunahoji ruzuku ya CHADEMA kuliwa na Mbowe, kwanini CCM hawatuelezi ruzuku yao Inaliwa na nani?

Kwa maana hiyo hakuna haja ya kuitoa CCM madarakani kama nyie mnaojiona ni mbadala wa CCM bado mnafanya madudu yaleyale ambayo tunayaona CCM. Ni ujinga kuona hampaswi kuhojiwa eti kisa CCM haihojiwi.
Hivi unawezaje kuhoji 250m lakini ukaufyata kuhoji 1.5 T zilizonyakuliwa na CCM kununulia wapinzani? Mbona kila siku mnaelezwa zinatumikaje? Lini hili genge la CCM lilitueleza namna linavyotumia ruzuku ya watanzania?
 
Wana Jf Tujiulize haya,

Chama kikubwa kama chama cha mapinduzi(CCM) kwa nini hawajawahi kutueleza ruzuku yao inatumikaje? Mbona kila siku wanahoji ruzuku ya CHADEMA lakini hawatupi matumizi ya ruzuku yao?

Kwa nini hatuhoji ufisadi unaofanywa na vigogo wa CCM wa matrioni na mali za umma ila tunashupaa kuhoji 250m za CHADEMA?

Kwa nini wataka kutuchagulia mwenyekiti wa kupambana naye?

Ni lini wanachama wa CCM waliwahi kukaa ktk ukumbi wowote ule hapa nchini na kumpigia kura mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) ili awaongoze kwa miaka 5?

Kwa nini ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) wanachama na viongozi hawataki kufanya uchaguzi wa mwenyekiti kila baada ya miaka 5 lakini wanashupaa na MBOWE ambaye hushinda uchaguzi halali wa kila baada ya miaka 5?

Majibu ya matumizi yaruzuku ya CHADEMA yamejibiwa Mara kwa Mara na CHADEMA.

*Tujikumbushe andiko LA Tundu lissu kuhusu ruzuku*

Kuhusu ruzuku. Kitu cha kwanza cha kuelewa ni kwamba ruzuku yetu haijawahi kutosheleza hata mahitaji ya kawaida ya uendeshaji chama.

Kila inapotokea kuna uchaguzi wa marudio au Uchaguzi Mkuu wowote ule, matumizi yamekuwa ni makubwa kuliko mapato yetu ya ruzuku na michango ya wabunge.

Tunapowapiga sana wabunge wetu, tuwe tunakumbuka pia kwamba nje ya ruzuku, wabunge wetu wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato ya chama hasa nyakati za Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio.

Kwa sababu ya upungufu huo wa mapato, hasa kila wakati wa Uchaguzi Mkuu, tumelazimika kukopa pesa kwa ajili ya kampeni kwa mapatano kwamba madeni hayo yatarudishwa baada ya Uchaguzi Mkuu.

Sasa ni vyema tujiulize, katika hali halisi ya Tanzania hii, ni akina nani hasa ambao wako, na wamekuwa, tayari kukikopesha chama??? Ni wachache sana, kwa sababu za wazi kabisa: hofu ya kunyanyaswa na mapolisi au uhamiaji au TRA.

Nimekuwa naingia kwenye vikao vya Kamati Kuu tangu mwaka 2004, na ninaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichokaa kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, ambacho hakikumwambia Mwenyekiti wetu atafute pesa za kampeni hata kwa kukopa, ili tuweze kununua vifaa vya kampeni au kulipia huduma zinazohitaji malipo.

Chopper, magari, pikipiki, bendera, mabango na kila aina ya vifaa vingine vya uchaguzi vinapopatikana kila Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, huwa hatuna utamaduni wa kuuliza au kujiuliza vifaa hivi vyote vitakuwa vimegharimu kiasi gani, na pesa hiyo itakuwa imetoka wapi.

Hata hivyo, kila baada ya Uchaguzi tunapoanza kulipa madeni ya waliotukopesha kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama, kunakuwa na kelele kubwa kwamba ruzuku ya chama inaliwa na viongozi wakuu, hasa Mwenyekiti. Na kila anayehama chama na kukimbilia CCM anarudia rudia tuhuma hizo mpaka watu wetu wanaanza na wao kuzirudia rudia.

Na lengo kubwa la mashambulizi haya, miaka yote, ni Freeman Aikaeli Mbowe, huyo huyo ambaye kila uchaguzi ukifika tunamwomba atutafutie pesa za kampeni.

MaCCM wanajua wanachokitaka kwenye kampeni hii ya kumchafua Mwenyekiti wetu. Wapambe wao, hasa wahamaji hawa, nao wanajua. Je, sisi wanachama wa CHADEMA tunaozirudia rudia tuhuma hizi tunajua hii ngoma tunayoicheza???

Naambiwa CAG naye amehoji juu ya matumizi ya ruzuku yetu. Ni kweli. Lakini ni kweli pia kwamba CAG amezungumzia pesa za ruzuku ambazo hatujawahi kuzipata tangu tuanze kupata ruzuku.

Na kwenye suala la ruzuku, maafisa wa Ofisi ya CAG wametuhumiwa kutoa taarifa yao bila kutupa sisi fursa ya kujibu 'audit queries' zao, kama inavyotakiwa na sheria na taratibu za ukaguzi wa mahesabu.

Tunapaswa hapa kukumbuka kwamba CAG na maafisa wake ni wateule wa Jiwe na/au watumishi wa serikali ambao, kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanashinikizwa sana kutafuta namna ya kuiumiza CHADEMA. Kwa hiyo, badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa jina la CAG, tunahitaji angalau kujihadhari na taarifa hizo kwa kuuliza maswali muhimu juu ya usahihi wake.

Kumalizia hoja hii ya ruzuku. Tumeijibu tangu ilipoanza kuibuliwa na marehemu Chacha Wangwe mwaka 2006/07. Tumeijibu wakati tunashughulikia 'Mkakati wa Mabadiliko' wa akina Zitto na Kitilla Mkumbo. Tumejieleza na kujieleza.

Lakini maCCM na wapambe wao wana malengo yao ya kutaka tuendelee kujadili ruzuku ya CHADEMA. Inawauma kwamba tangu mwaka 2005 tulipoanza kuonyesha aina mpya ya kampeni za kisiasa.

Tangu wakati huo, mafanikio yetu yamekuwa makubwa zaidi. Kutoka chama chenye wabunge 5 mwaka 2000 hadi chama kikuu cha upinzani chenye wabunge 72 mwaka 2015 ni mafanikio makubwa.

Ruzuku yetu imeongezeka pia, hata kama bado haikidhi mahitaji yetu yote. Wakati najiunga CHADEMA mwaka 2004, ruzuku yetu ilikuwa milioni 5.6 kwa mwezi. Leo ni takriban milioni 250 kwa mwezi.

Haya ni mafanikio makubwa. MaCCM wanajua hivyo lakini hawawezi kusema hivyo hadharani. Hawafurahishwi nayo. Ukitaka kujua wanatuonaje angalia mambo yote wanayotutendea. Mauaji, vipigo, vifungo vya kusingiziwa, ukiukaji wa haki za kisiasa, propaganda chafu, n.k.

Kuhusu kifo cha marehemu Chacha Zakayo Wangwe. Hii pia ni propaganda chafu iliyoanzishwa na maCCM. Ulizeni watu wetu wa Tarime kilichotokea mara baada ya kifo cha marehemu Chacha. Ghafla msiba ule ukawa wa akina Wassira na maCCM wenzao. Ukweli ni kwamba tuhuma hizi zilianzishwa na Wassira na genge lake wakati wa msiba huo. Vijana wa CCM walitolewa Bunda, Musoma na maeneo mengi nje ya Tarime na kuletwa kuja kumfanyia fujo Mwenyekiti wetu msibani. Ndugu zake Chacha, wale wale waliokuwa wakimbambikizia kesi ili afungwe wakati wa uhai wake, wakawa sasa ndio wenye uchungu naye akiwa amekufa. Hata hivyo, wananchi wa Tarime walielewa kilichokuwa kinaendelea. Ndio maana kwenye uchaguzi wa marudio baada ya kifo cha marehemu Chacha, tuliwapiga vibaya. Na ndio maana Tarime imeendelea kuwa ngome kubwa ya CHADEMA. Inatosha tu kujiuliza kama kweli tungekuwa tumemuua Chacha, haya maCCM kwa jinsi wanavyotuchukia wangetubakiza kwa hii miaka kumi??? Tunatakiwa kujielewa, tusije tukajikuta tunacheza ngoma ya maadui zetu wakubwa.

Nizungumzie swali langu la pili. Kwa miaka zaidi ya kumi sasa, CHADEMA ndio adui nambari moja wa maCCM. Dhambi yetu kubwa ni ile ile iliyokuwa dhambi kubwa ya NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 na 2000; na CUF kati ya 2000 na 2005.

Ni dhambi ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Ni dhambi ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye uchaguzi. Ni dhambi ya kupendwa na kuungwa mkono na wananchi.

Kwa sababu ya dhambi hiyo, ni lazima tushambuliwe na kuchafuliwa na kufanyiwa kila aina ya fujo na hila.

Tusipolielewa hilo ni rahisi sana kukatishwa tamaa na haya ya akina Waitara wa juzi, jana na wanaokuja mbeleni.

Ili tusibabaishwe na haya ya Magufuli na watu wake na hawa maYuda Iskariote, tukumbuke tu tulikotoka.

Tulikuwa na Amani Walid Kabourou kama Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Aliondoka na kujiunga na maCCM. Tulisonga mbele.

Tulikuwa na Zitto Zuberi Kabwe, Naibu Katibu Mkuu na Naibu KUB. Tulimwondoa na tukasonga mbele.

Tulikuwa na Mzee Saidi Arfi, Makamu Mwenyekiti na mrithi wa marehemu Chacha. Alitoroka na kujiunga nao, haikuwa mwisho wetu.

Tulikuwa na Dr. Wilbrod Peter Slaa, Katibu Mkuu na mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo. Alitukimbia katikati ya vita lakini hatuku-surrender. Tulisonga mbele.

Hawa wanaomkimbilia Jiwe, huyu anayetuogopa hadi kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa, wanatubabaishaje???

Mwisho, kwa yote ambayo nimeyasema hapa, sina maana sisi ni malaika tusiokuwa na doa lolote. Tuna mapungufu mengi ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kuyaondoa.

Mengine ni ya kujitakia; mengine ni ya kutakiwa na maadui zetu. Tupembue yapi ni ya kwetu wenyewe na yapi ni ya maCCM. Yote tuyatafutie dawa.Tujikumbushe andiko LA Tundu lissu kuhusu ruzuku:

Mengine ni ya kujitakia; mengine ni ya kutakiwa na maadui zetu. Tupembue yapi ni ya kwetu wenyewe na yapi ni ya maCCM. Yote tuyatafutie dawa.
Mkuu acha na haya mapumbavu yanayochangiwa na vipropaganda uchwara vya TISS ili watuaminishe CHADEMA ni mbaya kumbe ni uongo tu,kiukweli Mbowe ni chuma cha pua anawatesa sana serikali ya CCM ndo maana wanampiga sana vita mara kala ruzuku mara kakaa muda mrefu basi vijisababu tu vya kipumbavu yakwao yamewashinda na kugeukia yetu,alafu wanaompiga vita si wanaCHADEMA ni CCM!
 
mkuu kutohoji ruzuku za ccm hakuhalalishi kutohojiwa matumizi ya chadema. kwa mtzamo wangu vyama vyote vinakula ruzuku. sema chadema ndo chama kikuu cha upinzani....
Chama kikuu cha upinzani(chadema) kinaushawishi mkubwa.ndo maana ruzuku ya chama ni ndogo kama kingalikuwa na ruzuku ya kutosha wagombea wengi wengeweza kukamilisha kampeni ya uchaguzi kwa kuzunguka jimbo zima.mfano mzuri jimbo LA manyoni magharibi 2015 .mgombea wa chadema baadhi ya kata hakufanya mikutano ya kampeni .kati ya kata 9.akafanya kata 3.sababu ukosefu wa ruzuku.
 
Kwa maana hiyo hakuna haja ya kuitoa CCM madarakani kama nyie mnaojiona ni mbadala wa CCM bado mnafanya madudu yaleyale ambayo tunayaona CCM. Ni ujinga kuona hampaswi kuhojiwa eti kisa CCM haihojiwi.
Mkuu umesoma mpk mwisho au ni heading tu na kukomenti.
 
Pale unapohoji miambili ya mtoto aliyonunua pipi ya mkeo elfu 50 unaogopa kuhoji utanyimwa mchezo usiku... Shida sana
 
Mkuu wewe mchochezi, hivi kweli hujui kama mwenyekiti wa CCM ana kofia 2 hivyo anakinga kisheri?
 
Wana Jf Tujiulize haya,

Chama kikubwa kama chama cha mapinduzi(CCM) kwa nini hawajawahi kutueleza ruzuku yao inatumikaje? Mbona kila siku wanahoji ruzuku ya CHADEMA lakini hawatupi matumizi ya ruzuku yao?

Kwa nini hatuhoji ufisadi unaofanywa na vigogo wa CCM wa matrioni na mali za umma ila tunashupaa kuhoji 250m za CHADEMA?

Kwa nini wataka kutuchagulia mwenyekiti wa kupambana naye?

Ni lini wanachama wa CCM waliwahi kukaa ktk ukumbi wowote ule hapa nchini na kumpigia kura mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) ili awaongoze kwa miaka 5?

Kwa nini ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) wanachama na viongozi hawataki kufanya uchaguzi wa mwenyekiti kila baada ya miaka 5 lakini wanashupaa na MBOWE ambaye hushinda uchaguzi halali wa kila baada ya miaka 5?

Majibu ya matumizi yaruzuku ya CHADEMA yamejibiwa Mara kwa Mara na CHADEMA.

*Tujikumbushe andiko LA Tundu lissu kuhusu ruzuku*

Kuhusu ruzuku. Kitu cha kwanza cha kuelewa ni kwamba ruzuku yetu haijawahi kutosheleza hata mahitaji ya kawaida ya uendeshaji chama.

Kila inapotokea kuna uchaguzi wa marudio au Uchaguzi Mkuu wowote ule, matumizi yamekuwa ni makubwa kuliko mapato yetu ya ruzuku na michango ya wabunge.

Tunapowapiga sana wabunge wetu, tuwe tunakumbuka pia kwamba nje ya ruzuku, wabunge wetu wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato ya chama hasa nyakati za Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio.

Kwa sababu ya upungufu huo wa mapato, hasa kila wakati wa Uchaguzi Mkuu, tumelazimika kukopa pesa kwa ajili ya kampeni kwa mapatano kwamba madeni hayo yatarudishwa baada ya Uchaguzi Mkuu.

Sasa ni vyema tujiulize, katika hali halisi ya Tanzania hii, ni akina nani hasa ambao wako, na wamekuwa, tayari kukikopesha chama??? Ni wachache sana, kwa sababu za wazi kabisa: hofu ya kunyanyaswa na mapolisi au uhamiaji au TRA.

Nimekuwa naingia kwenye vikao vya Kamati Kuu tangu mwaka 2004, na ninaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichokaa kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, ambacho hakikumwambia Mwenyekiti wetu atafute pesa za kampeni hata kwa kukopa, ili tuweze kununua vifaa vya kampeni au kulipia huduma zinazohitaji malipo.

Chopper, magari, pikipiki, bendera, mabango na kila aina ya vifaa vingine vya uchaguzi vinapopatikana kila Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, huwa hatuna utamaduni wa kuuliza au kujiuliza vifaa hivi vyote vitakuwa vimegharimu kiasi gani, na pesa hiyo itakuwa imetoka wapi.

Hata hivyo, kila baada ya Uchaguzi tunapoanza kulipa madeni ya waliotukopesha kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama, kunakuwa na kelele kubwa kwamba ruzuku ya chama inaliwa na viongozi wakuu, hasa Mwenyekiti. Na kila anayehama chama na kukimbilia CCM anarudia rudia tuhuma hizo mpaka watu wetu wanaanza na wao kuzirudia rudia.

Na lengo kubwa la mashambulizi haya, miaka yote, ni Freeman Aikaeli Mbowe, huyo huyo ambaye kila uchaguzi ukifika tunamwomba atutafutie pesa za kampeni.

MaCCM wanajua wanachokitaka kwenye kampeni hii ya kumchafua Mwenyekiti wetu. Wapambe wao, hasa wahamaji hawa, nao wanajua. Je, sisi wanachama wa CHADEMA tunaozirudia rudia tuhuma hizi tunajua hii ngoma tunayoicheza???

Naambiwa CAG naye amehoji juu ya matumizi ya ruzuku yetu. Ni kweli. Lakini ni kweli pia kwamba CAG amezungumzia pesa za ruzuku ambazo hatujawahi kuzipata tangu tuanze kupata ruzuku.

Na kwenye suala la ruzuku, maafisa wa Ofisi ya CAG wametuhumiwa kutoa taarifa yao bila kutupa sisi fursa ya kujibu 'audit queries' zao, kama inavyotakiwa na sheria na taratibu za ukaguzi wa mahesabu.

Tunapaswa hapa kukumbuka kwamba CAG na maafisa wake ni wateule wa Jiwe na/au watumishi wa serikali ambao, kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanashinikizwa sana kutafuta namna ya kuiumiza CHADEMA. Kwa hiyo, badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa jina la CAG, tunahitaji angalau kujihadhari na taarifa hizo kwa kuuliza maswali muhimu juu ya usahihi wake.

Kumalizia hoja hii ya ruzuku. Tumeijibu tangu ilipoanza kuibuliwa na marehemu Chacha Wangwe mwaka 2006/07. Tumeijibu wakati tunashughulikia 'Mkakati wa Mabadiliko' wa akina Zitto na Kitilla Mkumbo. Tumejieleza na kujieleza.

Lakini maCCM na wapambe wao wana malengo yao ya kutaka tuendelee kujadili ruzuku ya CHADEMA. Inawauma kwamba tangu mwaka 2005 tulipoanza kuonyesha aina mpya ya kampeni za kisiasa.

Tangu wakati huo, mafanikio yetu yamekuwa makubwa zaidi. Kutoka chama chenye wabunge 5 mwaka 2000 hadi chama kikuu cha upinzani chenye wabunge 72 mwaka 2015 ni mafanikio makubwa.

Ruzuku yetu imeongezeka pia, hata kama bado haikidhi mahitaji yetu yote. Wakati najiunga CHADEMA mwaka 2004, ruzuku yetu ilikuwa milioni 5.6 kwa mwezi. Leo ni takriban milioni 250 kwa mwezi.

Haya ni mafanikio makubwa. MaCCM wanajua hivyo lakini hawawezi kusema hivyo hadharani. Hawafurahishwi nayo. Ukitaka kujua wanatuonaje angalia mambo yote wanayotutendea. Mauaji, vipigo, vifungo vya kusingiziwa, ukiukaji wa haki za kisiasa, propaganda chafu, n.k.

Kuhusu kifo cha marehemu Chacha Zakayo Wangwe. Hii pia ni propaganda chafu iliyoanzishwa na maCCM. Ulizeni watu wetu wa Tarime kilichotokea mara baada ya kifo cha marehemu Chacha. Ghafla msiba ule ukawa wa akina Wassira na maCCM wenzao. Ukweli ni kwamba tuhuma hizi zilianzishwa na Wassira na genge lake wakati wa msiba huo. Vijana wa CCM walitolewa Bunda, Musoma na maeneo mengi nje ya Tarime na kuletwa kuja kumfanyia fujo Mwenyekiti wetu msibani. Ndugu zake Chacha, wale wale waliokuwa wakimbambikizia kesi ili afungwe wakati wa uhai wake, wakawa sasa ndio wenye uchungu naye akiwa amekufa. Hata hivyo, wananchi wa Tarime walielewa kilichokuwa kinaendelea. Ndio maana kwenye uchaguzi wa marudio baada ya kifo cha marehemu Chacha, tuliwapiga vibaya. Na ndio maana Tarime imeendelea kuwa ngome kubwa ya CHADEMA. Inatosha tu kujiuliza kama kweli tungekuwa tumemuua Chacha, haya maCCM kwa jinsi wanavyotuchukia wangetubakiza kwa hii miaka kumi??? Tunatakiwa kujielewa, tusije tukajikuta tunacheza ngoma ya maadui zetu wakubwa.

Nizungumzie swali langu la pili. Kwa miaka zaidi ya kumi sasa, CHADEMA ndio adui nambari moja wa maCCM. Dhambi yetu kubwa ni ile ile iliyokuwa dhambi kubwa ya NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 na 2000; na CUF kati ya 2000 na 2005.

Ni dhambi ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Ni dhambi ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye uchaguzi. Ni dhambi ya kupendwa na kuungwa mkono na wananchi.

Kwa sababu ya dhambi hiyo, ni lazima tushambuliwe na kuchafuliwa na kufanyiwa kila aina ya fujo na hila.

Tusipolielewa hilo ni rahisi sana kukatishwa tamaa na haya ya akina Waitara wa juzi, jana na wanaokuja mbeleni.

Ili tusibabaishwe na haya ya Magufuli na watu wake na hawa maYuda Iskariote, tukumbuke tu tulikotoka.

Tulikuwa na Amani Walid Kabourou kama Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Aliondoka na kujiunga na maCCM. Tulisonga mbele.

Tulikuwa na Zitto Zuberi Kabwe, Naibu Katibu Mkuu na Naibu KUB. Tulimwondoa na tukasonga mbele.

Tulikuwa na Mzee Saidi Arfi, Makamu Mwenyekiti na mrithi wa marehemu Chacha. Alitoroka na kujiunga nao, haikuwa mwisho wetu.

Tulikuwa na Dr. Wilbrod Peter Slaa, Katibu Mkuu na mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo. Alitukimbia katikati ya vita lakini hatuku-surrender. Tulisonga mbele.

Hawa wanaomkimbilia Jiwe, huyu anayetuogopa hadi kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa, wanatubabaishaje???

Mwisho, kwa yote ambayo nimeyasema hapa, sina maana sisi ni malaika tusiokuwa na doa lolote. Tuna mapungufu mengi ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kuyaondoa.

Mengine ni ya kujitakia; mengine ni ya kutakiwa na maadui zetu. Tupembue yapi ni ya kwetu wenyewe na yapi ni ya maCCM. Yote tuyatafutie dawa.Tujikumbushe andiko LA Tundu lissu kuhusu ruzuku:

Kuhusu ruzuku. Kitu cha kwanza cha kuelewa ni kwamba ruzuku yetu haijawahi kutosheleza hata mahitaji ya kawaida ya uendeshaji chama.

Kila inapotokea kuna uchaguzi wa marudio au Uchaguzi Mkuu wowote ule, matumizi yamekuwa ni makubwa kuliko mapato yetu ya ruzuku na michango ya wabunge.

Tunapowapiga sana wabunge wetu, tuwe tunakumbuka pia kwamba nje ya ruzuku, wabunge wetu wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato ya chama hasa nyakati za Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio.

Kwa sababu ya upungufu huo wa mapato, hasa kila wakati wa Uchaguzi Mkuu, tumelazimika kukopa pesa kwa ajili ya kampeni kwa mapatano kwamba madeni hayo yatarudishwa baada ya Uchaguzi Mkuu.

Sasa ni vyema tujiulize, katika hali halisi ya Tanzania hii, ni akina nani hasa ambao wako, na wamekuwa, tayari kukikopesha chama??? Ni wachache sana, kwa sababu za wazi kabisa: hofu ya kunyanyaswa na mapolisi au uhamiaji au TRA.

Nimekuwa naingia kwenye vikao vya Kamati Kuu tangu mwaka 2004, na ninaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichokaa kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, ambacho hakikumwambia Mwenyekiti wetu atafute pesa za kampeni hata kwa kukopa, ili tuweze kununua vifaa vya kampeni au kulipia huduma zinazohitaji malipo.

Chopper, magari, pikipiki, bendera, mabango na kila aina ya vifaa vingine vya uchaguzi vinapopatikana kila Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, huwa hatuna utamaduni wa kuuliza au kujiuliza vifaa hivi vyote vitakuwa vimegharimu kiasi gani, na pesa hiyo itakuwa imetoka wapi.

Hata hivyo, kila baada ya Uchaguzi tunapoanza kulipa madeni ya waliotukopesha kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama, kunakuwa na kelele kubwa kwamba ruzuku ya chama inaliwa na viongozi wakuu, hasa Mwenyekiti. Na kila anayehama chama na kukimbilia CCM anarudia rudia tuhuma hizo mpaka watu wetu wanaanza na wao kuzirudia rudia.

Na lengo kubwa la mashambulizi haya, miaka yote, ni Freeman Aikaeli Mbowe, huyo huyo ambaye kila uchaguzi ukifika tunamwomba atutafutie pesa za kampeni.

MaCCM wanajua wanachokitaka kwenye kampeni hii ya kumchafua Mwenyekiti wetu. Wapambe wao, hasa wahamaji hawa, nao wanajua. Je, sisi wanachama wa CHADEMA tunaozirudia rudia tuhuma hizi tunajua hii ngoma tunayoicheza???

Naambiwa CAG naye amehoji juu ya matumizi ya ruzuku yetu. Ni kweli. Lakini ni kweli pia kwamba CAG amezungumzia pesa za ruzuku ambazo hatujawahi kuzipata tangu tuanze kupata ruzuku.

Na kwenye suala la ruzuku, maafisa wa Ofisi ya CAG wametuhumiwa kutoa taarifa yao bila kutupa sisi fursa ya kujibu 'audit queries' zao, kama inavyotakiwa na sheria na taratibu za ukaguzi wa mahesabu.

Tunapaswa hapa kukumbuka kwamba CAG na maafisa wake ni wateule wa Jiwe na/au watumishi wa serikali ambao, kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanashinikizwa sana kutafuta namna ya kuiumiza CHADEMA. Kwa hiyo, badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa jina la CAG, tunahitaji angalau kujihadhari na taarifa hizo kwa kuuliza maswali muhimu juu ya usahihi wake.

Kumalizia hoja hii ya ruzuku. Tumeijibu tangu ilipoanza kuibuliwa na marehemu Chacha Wangwe mwaka 2006/07. Tumeijibu wakati tunashughulikia 'Mkakati wa Mabadiliko' wa akina Zitto na Kitilla Mkumbo. Tumejieleza na kujieleza.

Lakini maCCM na wapambe wao wana malengo yao ya kutaka tuendelee kujadili ruzuku ya CHADEMA. Inawauma kwamba tangu mwaka 2005 tulipoanza kuonyesha aina mpya ya kampeni za kisiasa.

Tangu wakati huo, mafanikio yetu yamekuwa makubwa zaidi. Kutoka chama chenye wabunge 5 mwaka 2000 hadi chama kikuu cha upinzani chenye wabunge 72 mwaka 2015 ni mafanikio makubwa.

Ruzuku yetu imeongezeka pia, hata kama bado haikidhi mahitaji yetu yote. Wakati najiunga CHADEMA mwaka 2004, ruzuku yetu ilikuwa milioni 5.6 kwa mwezi. Leo ni takriban milioni 250 kwa mwezi.

Haya ni mafanikio makubwa. MaCCM wanajua hivyo lakini hawawezi kusema hivyo hadharani. Hawafurahishwi nayo. Ukitaka kujua wanatuonaje angalia mambo yote wanayotutendea. Mauaji, vipigo, vifungo vya kusingiziwa, ukiukaji wa haki za kisiasa, propaganda chafu, n.k.

Kuhusu kifo cha marehemu Chacha Zakayo Wangwe. Hii pia ni propaganda chafu iliyoanzishwa na maCCM. Ulizeni watu wetu wa Tarime kilichotokea mara baada ya kifo cha marehemu Chacha. Ghafla msiba ule ukawa wa akina Wassira na maCCM wenzao. Ukweli ni kwamba tuhuma hizi zilianzishwa na Wassira na genge lake wakati wa msiba huo. Vijana wa CCM walitolewa Bunda, Musoma na maeneo mengi nje ya Tarime na kuletwa kuja kumfanyia fujo Mwenyekiti wetu msibani. Ndugu zake Chacha, wale wale waliokuwa wakimbambikizia kesi ili afungwe wakati wa uhai wake, wakawa sasa ndio wenye uchungu naye akiwa amekufa. Hata hivyo, wananchi wa Tarime walielewa kilichokuwa kinaendelea. Ndio maana kwenye uchaguzi wa marudio baada ya kifo cha marehemu Chacha, tuliwapiga vibaya. Na ndio maana Tarime imeendelea kuwa ngome kubwa ya CHADEMA. Inatosha tu kujiuliza kama kweli tungekuwa tumemuua Chacha, haya maCCM kwa jinsi wanavyotuchukia wangetubakiza kwa hii miaka kumi??? Tunatakiwa kujielewa, tusije tukajikuta tunacheza ngoma ya maadui zetu wakubwa.

Nizungumzie swali langu la pili. Kwa miaka zaidi ya kumi sasa, CHADEMA ndio adui nambari moja wa maCCM. Dhambi yetu kubwa ni ile ile iliyokuwa dhambi kubwa ya NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 na 2000; na CUF kati ya 2000 na 2005.

Ni dhambi ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Ni dhambi ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye uchaguzi. Ni dhambi ya kupendwa na kuungwa mkono na wananchi.

Kwa sababu ya dhambi hiyo, ni lazima tushambuliwe na kuchafuliwa na kufanyiwa kila aina ya fujo na hila.

Tusipolielewa hilo ni rahisi sana kukatishwa tamaa na haya ya akina Waitara wa juzi, jana na wanaokuja mbeleni.

Ili tusibabaishwe na haya ya Magufuli na watu wake na hawa maYuda Iskariote, tukumbuke tu tulikotoka.

Tulikuwa na Amani Walid Kabourou kama Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Aliondoka na kujiunga na maCCM. Tulisonga mbele.

Tulikuwa na Zitto Zuberi Kabwe, Naibu Katibu Mkuu na Naibu KUB. Tulimwondoa na tukasonga mbele.

Tulikuwa na Mzee Saidi Arfi, Makamu Mwenyekiti na mrithi wa marehemu Chacha. Alitoroka na kujiunga nao, haikuwa mwisho wetu.

Tulikuwa na Dr. Wilbrod Peter Slaa, Katibu Mkuu na mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo. Alitukimbia katikati ya vita lakini hatuku-surrender. Tulisonga mbele.

Hawa wanaomkimbilia Jiwe, huyu anayetuogopa hadi kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa, wanatubabaishaje???

Mwisho, kwa yote ambayo nimeyasema hapa, sina maana sisi ni malaika tusiokuwa na doa lolote. Tuna mapungufu mengi ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kuyaondoa.

Mengine ni ya kujitakia; mengine ni ya wa na maadui zetu. Tupembue yapi ni ya kwetu wenyewe na yapi ni ya maCCM. Yote tuyatafutie dawa.

Hivi kweli urefu wote huu wa gazet ni Kwa ajili ya kwenda kinyume nyuma.
 
Back
Top Bottom