Tunahitajika kuwavumilia zaidi wanawake kuliko tuwapendavyo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,203
157,370
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
 
Hayo ndiyo maisha ndani ya maisha, ni nafsi pekee yenye kujua.
 
Ndoa ina mengi sana usipokuwa mvumilivu unweza ukapagawa na kuchizika katikati ya safari
 
kwa sababu vijana wengi pia hawaoi hadi wazeeke mtaan hadi 35+ sasa mwanamke wa 35+ si ndo mnanuita mzee
 
Tatizo wanaharibiana.

Yaan wote wangekuwa na tabia hizi wangechukuliwa katika udhaifu wao mapema sana, ila kuna wanawake wana mlengo wa kulia yaan katika situation kama hiyo wanabaki wawili katika 60,kwamba ni kweli hawajawahi kutoa nje kabisa.

Unadhani kitakachofuata kwa mkeo ninini kama sio kumfukuza kama nzi???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom