Tunahitaji wanasiasa wenye calibre ya Tundu Lissu, Godbless Lema na Zitto Kabwe

a4apple

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
927
1,131
Hakuna asiyejua kuwa Tanzania tunapitia kipindi cha majaribu ya uhuru wa maoni na kujieleza kuanzia mwaka 2015. Katika kipindi hiki kushtakiwa kwa kesi ya uchochezi na kesi za kumdhihaki yule asiyejaribiwa ni kufumba macho na kufumbua.

Wananchi na wanasiasa wengi wamekuwa waoga kutumia haki zao za msingi za kutoa maoni, hasa pale ambapo maoni yao yatapingana na mtazamo wa asiyejaribiwa. Lakini nashukuru hatujazimishwa wote, tunao bado wanasiasa vijana machachari Mhe. Lema, Lisu, na Zitto.

Hawa tunawategemea kututetea wananchi na kupinga vitisho dhidi ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.
 
Hakuna asiyejua kuwa Tanzania tunapitia kipindi cha majaribu ya uhuru wa maoni na kujieleza kuanzia mwaka 2015. Katika kipindi hiki kushtakiwa kwa kesi ya uchochezi na kesi za kumdhihaki yule asiyejaribiwa ni kufumba macho na kufumbua. Wananchi na wanasiasa wengi wamekuwa waoga kutumia haki zao za msingi za kutoa maoni, hasa pale ambapo maoni yao yatapingana na mtazamo wa asiyejaribiwa. Lakini nashukuru hatujazimishwa wote, tunao bado wanasiasa vijana machachari Mhe. Lema, Lisu, na Zitto. Hawa tunawategemea kututetea wananchi na kupinga vitisho dhidi ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.
Siamini kama wote tunapitia kipindi kigumu. Kipato changu kiko pale pale. mshahara wangu uko pale pale. Safari zangu ziko pale pale!

Kuna hii tabia ya kuamini yanayokupata na wengine yanawapata. Mtu anaanza kuandika haya eti watanzania tunapitia kipindi kigumu. kigumu kwa lipi? Mimi siyo mwanasiasa na sihitaji jukwaa kuzungumza sera za kazi yangu. Hao wanasiasa wakikerwa, wanashawishi nasi tuwe kama wao. I don't imbibe that idea! Kukamatwa na kuachiwa siyo ubora au ushujaa na hayo ndo yaliyotokea pale Zimbabwe kwa Morgan Tsvangilai, hata kuvunjwa mkono. Baadaye ikaonekana ni mtu bogus tu! Siyo kila anayeonewa ni shujaa.

Tujadili mambo na manufaa makubwa ya kitaifa, siyo haya ya binafsi. Ushujaa wao uko wapi wakati Bunge miaka yote linakula pesa za wananchi bila huruma tena hovyo tu! Sijaona yeyote kati ya hao akija juu kabisa kuzuia kujirundikia posho kama wanavyojionyesha kwa mambo yao binafsi.
 
Inawezekana wewe huna shida kuna Watanzania wengi wanatafuta haki zao zilizofungwa na watawala.

Leo unajiona haujaguswa siku ukiguswa ndipo utaelewa.

Kuna wanafunzi 8000 hawajapewa mikopo na wana risk ya kufukuzwa shule,ila sababu una kazi na mshahara huwezi kuwaona hawa.Kuna wahitimu ambao waliajiriwa wamefukuzwa ati wanahakiki wafanyakazi leo wako mitaani ila sababu unachosema hawa huwezi kuwaona.

Umefumbwa macho na akili ya ubinafsi.Kuna zaidi ya wewe wanao wahitaji akina Lema.

Na kesi ya Lema itaingua kwenye vitabu vya Mahakama kama kesi ya mfano kwa ajili ya watakaonyimwa dhamana kwa sababu zisizo za msingi.

Bado Lema amethubutu kumweleza Rais ukweli ambao wewe tumeshindwa kufanya pamoja na kuwa na kazi na kutembea utakako,umekosa u binadamu sababu umejivika umimi.
 
Hakuna asiyejua kuwa Tanzania tunapitia kipindi cha majaribu ya uhuru wa maoni na kujieleza kuanzia mwaka 2015. Katika kipindi hiki kushtakiwa kwa kesi ya uchochezi na kesi za kumdhihaki yule asiyejaribiwa ni kufumba macho na kufumbua. Wananchi na wanasiasa wengi wamekuwa waoga kutumia haki zao za msingi za kutoa maoni, hasa pale ambapo maoni yao yatapingana na mtazamo wa asiyejaribiwa. Lakini nashukuru hatujazimishwa wote, tunao bado wanasiasa vijana machachari Mhe. Lema, Lisu, na Zitto. Hawa tunawategemea kututetea wananchi na kupinga vitisho dhidi ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

kWA assesment yangu ya vyama vya upinzani WOTE HAO Wwatatu uliowataja ni wapiga kelele tu hela hawana wanataka kudandia pesa za wengine.Vyama vya upinzani vinahitaji wenye pesa sio wapiga kelele Kama Lisu,Lema na Zitto KABWE.Bila pesa upinzani hupenyi utabaki kupiga tu mayowe barabarani kama mwehu.Wenye pesa zao akina Mbowe,LOWASA ,NDESAMBURO ,MTEI wako kimya wakiangalia tu akina Tundu LISU,Lema na Zitto KABWE wakibwata mabarabarani wakidhani waweza kitwaa chama na kukikakilia juu wampindue mwenyekiti.Chama kina wenyewe wenye pesa zao.Hao wengine waendelee tu kupiga mayowe barabarani
 
Siamini kama wote tunapitia kipindi kigumu. Kipato changu kiko pale pale. mshahara wangu uko pale pale. Safari zangu ziko pale pale!

Kuna hii tabia ya kuamini yanayokupata na wengine yanawapata. Mtu anaanza kuandika haya eti watanzania tunapitia kipindi kigumu. kigumu kwa lipi? Mimi siyo mwanasiasa na sihitaji jukwaa kuzungumza sera za kazi yangu. Hao wanasiasa wakikerwa, wanashawishi nasi tuwe kama wao. I don't imbibe that idea! Kukamatwa na kuachiwa siyo ubora au ushujaa na hayo ndo yaliyotokea pale Zimbabwe kwa Morgan Tsvangilai, hata kuvunjwa mkono. Baadaye ikaonekana ni mtu bogus tu! Siyo kila anayeonewa ni shujaa.

Tujadili mambo na manufaa makubwa ya kitaifa, siyo haya ya binafsi. Ushujaa wao uko wapi wakati Bunge miaka yote linakula pesa za wananchi bila huruma tena hovyo tu! Sijaona yeyote kati ya hao akija juu kabisa kuzuia kujirundikia posho kama wanavyojionyesha kwa mambo yao binafsi.
Yawezekana kweli kipato chako kiko pale pale, lakini kg 1 ya unga wa mahindi (sembe) ni tsh 2000+ kwa sasa, lakini kipindi cha Kikwete kg 1 hiyo hiyo na ya bidhaa hiyo ilikuwa tsh 800-1000
 
Siamini kama wote tunapitia kipindi kigumu. Kipato changu kiko pale pale. mshahara wangu uko pale pale. Safari zangu ziko pale pale!

Kuna hii tabia ya kuamini yanayokupata na wengine yanawapata. Mtu anaanza kuandika haya eti watanzania tunapitia kipindi kigumu. kigumu kwa lipi? Mimi siyo mwanasiasa na sihitaji jukwaa kuzungumza sera za kazi yangu. Hao wanasiasa wakikerwa, wanashawishi nasi tuwe kama wao. I don't imbibe that idea! Kukamatwa na kuachiwa siyo ubora au ushujaa na hayo ndo yaliyotokea pale Zimbabwe kwa Morgan Tsvangilai, hata kuvunjwa mkono. Baadaye ikaonekana ni mtu bogus tu! Siyo kila anayeonewa ni shujaa.

Tujadili mambo na manufaa makubwa ya kitaifa, siyo haya ya binafsi. Ushujaa wao uko wapi wakati Bunge miaka yote linakula pesa za wananchi bila huruma tena hovyo tu! Sijaona yeyote kati ya hao akija juu kabisa kuzuia kujirundikia posho kama wanavyojionyesha kwa mambo yao binafsi.
Umetumia nguvu kubwa kujadili ubinafsi. Hapa hatujadili familia zetu bali mustakbali wa nchi na vizazi vyetu.
Mbona umechagua Zimbabwe bila kwenda South Africa na Myanmar?
 
kWA assesment yangu ya vyama vya upinzani WOTE HAO Wwatatu uliowataja ni wapiga kelele tu hela hawana wanataka kudandia pesa za wengine.Vyama vya upinzani vinahitaji wenye pesa sio wapiga kelele Kama Lisu,Lema na Zitto KABWE.Bila pesa upinzani hupenyi utabaki kupiga tu mayowe barabarani kama mwehu.Wenye pesa zao akina Mbowe,LOWASA ,NDESAMBURO ,MTEI wako kimya wakiangalia tu akina Tundu LISU,Lema na Zitto KABWE wakibwata mabarabarani wakidhani waweza kitwaa chama na kukikakilia juu wampindue mwenyekiti.Chama kina wenyewe wenye pesa zao.Hao wengine waendelee tu kupiga mayowe barabarani
Japo una Uhuru wa kuchangia lakini una mawazo na fikra za kipuuzi kweli kweli.
 
Siamini kama wote tunapitia kipindi kigumu. Kipato changu kiko pale pale. mshahara wangu uko pale pale. Safari zangu ziko pale pale!

Kuna hii tabia ya kuamini yanayokupata na wengine yanawapata. Mtu anaanza kuandika haya eti watanzania tunapitia kipindi kigumu. kigumu kwa lipi? Mimi siyo mwanasiasa na sihitaji jukwaa kuzungumza sera za kazi yangu. Hao wanasiasa wakikerwa, wanashawishi nasi tuwe kama wao. I don't imbibe that idea! Kukamatwa na kuachiwa siyo ubora au ushujaa na hayo ndo yaliyotokea pale Zimbabwe kwa Morgan Tsvangilai, hata kuvunjwa mkono. Baadaye ikaonekana ni mtu bogus tu! Siyo kila anayeonewa ni shujaa.

Tujadili mambo na manufaa makubwa ya kitaifa, siyo haya ya binafsi. Ushujaa wao uko wapi wakati Bunge miaka yote linakula pesa za wananchi bila huruma tena hovyo tu! Sijaona yeyote kati ya hao akija juu kabisa kuzuia kujirundikia posho kama wanavyojionyesha kwa mambo yao binafsi.

Maisha yako kutokubadilika haimaanishi mambo hayabadiliki, You don't see it coming! Labda kwa sababu hayajakufikia wewe, hata wengine tunaishi vilevile tu, tena kipato kimeongezeka, lakini hatuwezi kaa kimya kwa kua ni wazi kabisa tunaelekea pabaya, huu uhuru unavyopelekwa ovyo, na biashara za watu zinafungwa without warning, hata watengeneza viroba hawakujua ila leo limewafikia, wanaambiwa wafunge bila kupewa muda wowote kuclear inventory, huku walikua wamesign mikataba na wamepewa go~ahead na TBS. Hizo ni ajira zimekufa hapo.

Ni kama umekaa unaona mtoto anachezea wembe kuweka kwenye ulimi alafu kwa kua haujamkata unasema "mbona haujamkata?" you think kila kitu kitaenda sawa. Tunacheza na hatari sasa hivi, probability ni mbili, either tutapita kibishi na kuishia pazuri, au tutaishia pabaya zaidi wamuachie mwingine kuja kufix hizi mistakes baadaye kitu ambacho ni very costful. Investors watakua wamekimbia wote by then kwa hizi treatment za kijinga.
 
Japo una Uhuru wa kuchangia lakini una mawazo na fikra za kipuuzi kweli kweli.

Kwa mtizamo wangu kama UKAWA wanatafuta watu wawezao kupiga mayowe sana barabarani I HIGHLY RECOMMEND wawape Godbless lema,TUndu LISU ana ZITTO KABWE.hizo nafasi zinawafaa sana tena sana.Kwa hilo hawana mshindani.
 
Maisha yako kutokubadilika haimaanishi mambo hayabadiliki, You don't see it coming! Labda kwa sababu hayajakufikia wewe, hata wengine tunaishi vilevile tu, tena kipato kimeongezeka, lakini hatuwezi kaa kimya kwa kua ni wazi kabisa tunaelekea pabaya, huu uhuru unavyopelekwa ovyo, na biashara za watu zinafungwa without warning, hata watengeneza viroba hawakujua ila leo limewafikia, wanaambiwa wafunge bila kupewa muda wowote kuclear inventory, huku walikua wamesign mikataba na wamepewa go~ahead na TBS. Hizo ni ajira zimekufa hapo.

Ni kama umekaa unaona mtoto anachezea wembe kuweka kwenye ulimi alafu kwa kua haujamkata unasema "mbona haujamkata?" you think kila kitu kitaenda sawa. Tunacheza na hatari sasa hivi, probability ni mbili, either tutapita kibishi na kuishia pazuri, au tutaishia pabaya zaidi wamuachie mwingine kuja kufix hizi mistakes baadaye kitu ambacho ni very costful. Investors watakua wamekimbia wote by then kwa hizi treatment za kijinga.
Nadhani umeathilika kwa kiasi fulani. Unafikia hatua ya kutetea viroba eti tu kwa sababu wana nembo ya TBS! Aspirin ni dawa iliyotumika miaka mingapi ktk dunia hii, ikiokoa maisha ya watu? Ilipogundulika ina madhara kwa watoto, mbona ilizuiliwa natena kwa matangazo ili kuwaepusha watoto? Mionzi imetumika dunia nzima kutunza vyakula lakini, baadaye imezuiliwa ili kuwalinda walaji. leo hii unatetea viroba! Mtu anadai eti aelimishwe kabla ya kuzuia viroba.

Mambo ya hovyo na yasiyo sahihi, yakisharudiwa tena na tena baadhi yetu huyazoea na kudhani ni ukweli. Nani anathibitisha tunaelekea kubaya kuliko tulikokuwa? Eti tu watu hawafanyi mikutano. Hilo ni baya kuliko pesa ya katiba iliyoliwa kwa mabilioni? Kodi zisizolipwa kwa mabilioni, Posho za wabunge kwa mabilioni? Tundu Lisu hakuona mabilioni aliyoweka mifukoni miaka yote hiyo bila ulinganifu wa kazi yake?
 
Umetumia nguvu kubwa kujadili ubinafsi. Hapa hatujadili familia zetu bali mustakbali wa nchi na vizazi vyetu.
Mbona umechagua Zimbabwe bila kwenda South Africa na Myanmar?
Ninachokataa ni kujidai tumeona muelekeo wa nchi ni mbaya kuliko tulikotoka. Tulikotoka kuna nini cha kujifunza?
 
Back
Top Bottom