Tunahitaji voter's drive network nchi nzima now! Asasi za kijamii step up now!

George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
Ndugu wana JF,

Ni wakati muafaka kwa asasi zetu za kijamii kujitokeza hadharani na kuchukua jukumu la kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura, Sote tumekuwa mashahidi watanzania wengi wanapenda mabadiliko na wamechoka na ubabaishaji wa wanasiasa. Hivyo njia pekee ya kutimiza lengo la kufikia mabadiliko na ushindani wa kisiasa ni kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi wetu kupigania haki yao ya msingi ya kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Inakatisha tamaa sana kuona katika jimbo la Igunga watu wengi waliojiandikisha kupiga kura hawakupiga kura, hii inatokana na watanzania wengi kukata tamaa na mwenendo wa siasa zetu, hivyo tunahitaji new strategy ya kuwezesha wananchi wengi wanajitokeza kujiandikisha na kupiga kura. Na hapa tulipofikia ndipo asasi za kijamii zinapotakiwa kuchukua nafasi yake ya kuanzisha mtandao wa kijamii nchi nzima kuhakikisha every potential eligible voter is registered to vote.

Nimesikitishwa sana na wanaharakati wetu na asasi za kijamii zinapokuwa zinajitokeza kurusha lawama kuwa kuna vijana waliotimiza umri wa kupiga kura mwaka huu lakini hawata piga kura kwa kuwa hawakujiandikisha kana kwamba hilo ni swala jipya, Lazima wanaharakati wetu wawe na pre- emptive strategy za kuhakikisha kabla ya uchaguzi au voters register hajiwekwa hadharani na tume wana washitaki tume ya uchaguzi kwa kutumiwa kutaka kuwanyima baadhi ya wananchi haki yao ya kupiga kura.

Mathalani, katika jimbo la igunga kuna wapiga kura waliojiandikisha zaidi ya 170,000 lakini waliojitokeza kupiga kura hawafiki hata nusu ya waliojiandikisha, this is a shame to ourselves , something needs to be done urgently. Wanaharakati wanatakiwa ku challenge tume ya uchaguzi na kufanya vetting ya kujua kama je hao watu wote 170,000 ni ghost voters au ni real voters? na Je kwa nini hawajitokezi kupiga kura? Hili daftari la wapiga kura la tume ya uchaguzi linahitaji kuboreshwa kila mwezi na kila mara inapotakiwa.

Natoa wito kwa asasi za kijamiii kuanzisha Network nchi nzima kuhakikisha elimu ya kujiandikisha na kutumia nguvu ya wananchi kwenye voting booth ya kuchagua kiongozi na chama bora inatumika ipasavyo. Asasi za kijamii zinatakiwa kuwa pro-active na sio re-active, waache kutoa press realese kuwa kuna wapiga kura watakuwa desfranchised badala yake tuanze campaign na mpanga madhubuti wa kuanzisha NETWORK nchi nzima ya VOTER DRIVE, na tufungue kesi mahakamani ya kikatiba kuishitaki tume ya uchaguzi kwa kusababisha baadhi ya wananchi kukosa haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa kuwa VOTER REGISTER haikuboreshwa.

Wanasheria, needs to dare now! kuishitaki tume ya uchaguzi kwa kutumika ku desfranchise potential eligible voters.
 
Mkuu umenena hasa. Wahanga wa kushindwa kutumia haki ya kikatiba na kidemokrasia ni wananchi wenyewe na pendekezo lako la kufanya umiliki wa mchakato mzima uwe upande wa wananchi ni sasa kabisa. Hapana hakuna itikadi za kisiasa bali ni umma kudai haki yake ya msingi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom