Tunahitaji Uhuru Wa Kujieleza, Uhuru Wa Maoni, Siyo Kumkamata Max!

Apr 23, 2012
76
71
.., najiuliza maswali hapa, kabla Max (mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa Jamii-forums) hajafikishwa kesho kizimbani.., kujibu tuhuma ambazo zinamkabili..., (kushindwa au kukataa kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake/watumiaji wa mtandao wa jamii forums)..,

Ok...., hivi inaweza kutokea hii kweli..,

MARK ZUCKERBERG (mmiliki wa mitandao ya Whatsapp na Facebook) au mmiliki wa Instagram, KEVIN SYSTROM, au mmiliki wa Telegram ndugu wawili, NIKOLAI and PAVEL DUROV, au EVAN SPIEGEL wa Snapchat.., wakatoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao yao ya kijamii?

HAPANA...,

Kila mtandao una terms na conditions na ili kujiunga inabidi mtumiaji ukubaliane nazo.., (vigezo na masharti)

hakuna sehemu imetajwa taarifa za mtumiaji zinaweza kutolewa Polisi/Serikali ikizihitaji..., (katika sehemu ya hizo terms and conditions wakati wa kujiunga na mtandao husika)

.., HAKUNA.

.., sheria ya makosa ya kimtandao (CyberCrime Act) ya mwaka (2015) sifikiri kama inaweza kuingilia 'huduma za úsiri' za watu/watumiaji wa Mitandao kiasi hicho..., unless kuwepo na uvunjifu mkubwa sana wa sheria za nchi (lakini siyo kumshurutisha, mtoa huduma (service provider) kutoa taarifa za wateja wake,

.., kama kuna mtandao wa kijamii ambao Ungelikuwa unaendekeza tabia hiyo ya kutoa taarifa za wateja wake kwenye vyombo vya dola.., wasingelikuwa na watumiaji tena.., (taarifa za mteja lazima zilindwe)

Kiundwe chombo chenye nguvu na utaalamu wa intelijensia kupitia Polisi katika kuchunguza haya mambo kivyao kama zilivyo intelejensia zingine za ulinzi duniani bila kulazimisha watu au taasisi au kampuni kuwarahisishia kazi katika pelelezi zao...,

Sheria yetu ya makosa ya kimtandao.., ni sheria dhaifu sana.., hauwezi kutunga sheria yenye kumtaka au kumlazimisha mtoa huduma (service provider) kutoa taarifa za wateja wake kwa lazima.., Ilitakiwa haki hiyo ipatikane kwa kuomba ridhaa ya mahakama.., watoa huduma (service providers) na jamhuri wakapambane kisheria ili kupata haki ya awali ya kutoa au kutokutoa taarifa za watumiaji wa mtandao husika.., lakini hii sheria ya sasa ina udhaifu mkubwa.., jamhuri ina upenyo mkubwa kuliko watumiaji na hata wamiliki wa Mitandao ya kijamii...,

Max siyo mara ya kwanza kukamatwa..., (kwa wanaomfahamu vyema).

Tunamtakia kila la heri huko rumande wapo Watanzania pia..., Katika hili la Max mnataka kufunga wengi. Jamii Forum imefanya kazi kubwa sana kwa Taifa letu...,
Kazi ya kutukuka na kuhitaji pongezi.

Nilitegemea utawala unaojipambanua kupambana na ufisadi kama awamu ya 5 iwape tano Jamii Forums na siyo kuwaghasi!

Jamii Forums ni sehemu ambayo watu wameweza kufichua maovu na kutoa taarifa muhimu bila kuwa na wasiwasi wa kulipiziwa kisasi kwa sababu nchi yetu haijawahi kuonyesha dhamira ya dhati ya kuwalinda wanaofichua maovu mbalimbali.

Watendaji Wakuu wa Serikali msiende kinyume na maono ya kiongozi mkuu wenu, ambaye anajipambanua hadharani kwamba anapinga ufisadi, basi, Jamii Forums ni moja kati ya majukwaa yanayosaidia mapambano hayo..,

., siyo vyema sana., kumlazimisha mmiliki wa Jamii Forums kutoa taarifa za watumiaji wa Jamii Forums.., anyways.., tusubiri hiyo kesho.., tutapata mengine ya kusema kuhusu haya masuala!

ni MAONI TU..,

Martin Maranja Masese (MMM)
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom