Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi - haya mauzauza yanayofanywa na Serikali ya sasa sio halali

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,944
3,820
Serikali iliyopo ipo hapo kwa kuwekwa tuseme kimabavu bila ya kutoana jasho, japo kuna waliopata vilema na waliouliwa ili Chama cha CCM kisimike serikali yake, ambayo ndio imejipa madaraka ya kuongoza wasiotaka kuongozwa na wao.

Natija ni kila linalofanywa na serikali hii halikubaliki kwa roho safi, maneno na sononosonono kwa wananchi haziishi,na lawama ni kuwa Serikali haina radhi za wananchi inayowaongoza, hata Rais Mrithi Mzanzibari mkaazi Mama Samia Suluhu Hasani afanye nini, bado dukuduku la uchaguzi uliowaweka madarakani na laana yake lipo palepale, na kwa vile waTz wengi ni waumini wa Dini basi dini hazikubaliani na zulma ya aina yeyote ile.

Tuseme tu serikali iliyopo madarakani imelaniwa na inaendelea kulaaniwa na wale waliodhulumiwa haki yao ya kupiga kura na laana inawaandama maana kila wanapofumuana wanajiona bado wapo palepale wameondowa wasioona wameweka wasiosikia.

Serikali inaendeshwa kienjeji zaidi bila ya kuzingatia au kufuata katiba ya nchi, watu wanafukuzana makazini bila ya kufuata utaratibu, alimuradi kila kiongozi ili aonekane anafanya kazi basi ni kumfukuza mtu au watu kazini, wandugu hio ni laana na ndio iliyopo mabegani mwa serikali ya CCM.

Siku hizi wamekuja na style ya kushona na kufumua, CCM wote waliopo madarakani ndani ya serikali ni sawa na tambara bovi lililooza ,sasa pana kushona na kufumua hapo? Maana hata kuweka viraka ni shida.

Wekeni Tume huru muwawache wananchi wajikanyage wenyewe, sio mnajijazia kura feki ili kuweza kuingia serikalini na kuchomeka mirija na kujijengea himaya na netiwaki za kujilimbikizia mali ni aibu na, hatutofika mbali sana nchi itajaa matabaka ya walionacho na wasionacho.

CCM mmeiua na mnaendelea kuiua Tanzania kwa kufeli kufanya uchaguzi huru uliowazi na wa haki. CCM ina wananchama wengi lakini viongozi waliomdarakani ndio wameingia woga na wanachokifanya ni kutaka netiwaki zao zibaki.
 
CCM mpya ana kazi kubwa sana kupenya au kutoboa. Bila ya uchaguzi wa haki na huru hata CCM wapya tuna kazi kubwa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom