Tunahitaji tume huru "NEC"

Makanda

Member
Oct 29, 2010
77
2
ndugu zangu wakati umefika watanzania tukaadamana kutaka tume huru ya uchanguzi iliyoundwa bila kushirikisha serkali iliyoko madarakani.tunahitaji mabadiriko ya katiba kuhusiana na mambo ya uchanguzi.
 
Najiuliza sijui tutaingiaje kwenye uchaguzi wa 2015 kama NEC itaendelea kuwa hii!
Has anyone else imagined this?
 
hilo ndilo la msingi hata hivyo ilipaswa KUDAIWA KABLA YA UCHAGUZI, lakini Viongozi wetu wanakubali kuingia kwenye UCHAGUZI bila tume HURU kwani hawajui matokeo yake?? Mbuzi umemnunua kwa bwana Mbaruku, aliyekwiba mbuzi huyo bwana Mbaruku,unapeleka mashtaka kwa bwana hakimu Mbaruku.....
KIFUATACHO SASA NAONA
KUTAKUWEPO MUAFAKA:sleep:
 
Jana nilitoa maoni yangu kuhusu h uzito wa hili suala kwenye thread aliyoanzisha bwana anayeitwa Rev. Kishoka lakini hiyo thread siioni. Ile thread ya Rev. Kishoka imekwenda wapi!!?? Katika mchango wangu kwenye hiyo thread nilishauri suala la mabadiliko ya katiba liwe priority kwa serikani yoyote inayoingia madarakani. Tushinikize jumuiya ya kimataifa kuishinikiza serikali mpya kuanza mchakato. Asasi zisizo za kiserikali zitumie matatizo tunayoyaona kwenye uchaguzi huu kushinikiza mabadiliko. Bila mabadiliko ya katiba siasa za vyama vingi Tanzania zitaendelea kuwa kiini macho.Ibadibi tuwe na tume huru ya uchaguzi, ofisi ya usajili wa vyama na mahakama. Mambo haya yanaweza kutupeleka kwenye mtafaruku, Kenya ni mfano mzuri
 
ndugu zangu wakati umefika watanzania tukaadamana kutaka tume huru ya uchanguzi iliyoundwa bila kushirikisha serkali iliyoko madarakani.tunahitaji mabadiriko ya katiba kuhusiana na mambo ya uchanguzi.

Wale Polisi waliowaua waandamanaji wa Pemba mwaka 2001 waliokuwa wakidai Tume Huru wameshakusanywa hapa Dar ili kufanyakazi yao kwa watakaoandamana kuomba Tume Huru Bara.

Usithubutu kufanya hivyo, unaweza ukauawa! Tume huru hakuna, iko tume ya CCM tu iliyowekwa na Mungu Mwenyezi.
 
(naona post ya awali haikuwa reader-friendly sababu ya font)
Jana nilitoa maoni yangu kuhusu h uzito wa hili suala kwenye thread aliyoanzisha bwana anayeitwa Rev. Kishoka lakini hiyo thread siioni. Ile thread ya Rev. Kishoka imekwenda wapi!!?? Katika mchango wangu kwenye hiyo thread nilishauri suala la mabadiliko ya katiba liwe priority kwa serikani yoyote inayoingia madarakani. Tushinikize jumuiya ya kimataifa kuishinikiza serikali mpya kuanza mchakato. Asasi zisizo za kiserikali zitumie matatizo tunayoyaona kwenye uchaguzi huu kushinikiza mabadiliko. Bila mabadiliko ya katiba siasa za vyama vingi Tanzania zitaendelea kuwa kiini macho.Ibadibi tuwe na tume huru ya uchaguzi, ofisi ya usajili wa vyama na mahakama. Mambo haya yanaweza kutupeleka kwenye mtafaruku, Kenya ni mfano mzuri
 
Hivi ni nani anaye wachagua hao watu wa tume! are they appointed by president!????:bowl::bowl::bowl: Mmmmh this will never work!
 
Nashangaa. These guys hav been travelling abroad since they took power. Why can't they learn? Nilikua namsikia kiravu na uyo profesa chaligha wanadanganya raia kua nchi zote tume ya uchaguzi inaendeshwa na serikali;iyo ni kweli,ila viongozi wa tume uwa ni wateuzi wa rais na washauri wake,ambao ni lazima waidhinishwe na bunge. Ina mana wanahojiwa na bunge,na bunge lina uwezo wa kuwakubali au kuwakataa. Kisha viongozi hao wanakua wanawajibika kwa bunge,ikimaanisha ni bunge pekee ndo linaweza kuwafukuza au kuwasimamisha kazi. Ila kwa Tanzania,the opposite is true. Kazi kwelikweli.
 
Unless kama tuna dfn tofauti ya democrasi otherwise it goes without saying that tume huru is a reflection of democrasia
 
Bila kuwa na wazalendo katika tume nchi hii itaendelea kuibiwa na kuwa ombaomba kwa kupitia neno Umaskini Huku wazungu wanakuja na kuwa matajiri ndani ya nchi maskini Sielewi kabisa Maisha haya.
 
Bila kuwa na wazalendo katika tume nchi hii itaendelea kuibiwa na kuwa ombaomba kwa kupitia neno Umaskini Huku wazungu wanakuja na kuwa matajiri ndani ya nchi maskini Sielewi kabisa Maisha haya.

Tume huru inajengwa kwenye katiba na sheria za uchaguzi na hivyo inabidi wanaharakati, wanasiasa na wote wanaoitakia serikali hii mema waanze kudai katiba mpya mara moja ili iweze kushughulikia suala uhuru wa Tume ya Uchaguzi, Msajili, Mahakama na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
 
Unayoyasema ukweli mtupu. Endapo tutaondoa woga ambao tumekuwa nao kama watanzania kwa visingizio vya kwamba Tanzania ni nchi ya amani. AMANI imekuwa ikitumika kutukandamiza na kutuacha katika dimbwi la umaskini. Huu ni wakati muafaka wa wa kuleta mabadiliko ya taasisi zote za Kiserikali ikiwemo TUME YA UCHAGUZI WA KIKWETE. Nguvu wa umma wa watanzania itumie mwanya wa uchaguzi huu uliosimamiwa vibaya na TUME YA UCHAGUZI WA KIKWETE. mabadiliko ni leo na si kesho.
 
I totally agree with u broda...... it's high time we demand for a change....Democracy itaanzia hapo
 
Hoja nzuri sana hii. Ili tuweze kupata tume huru ni kweli tutahitaji marekebisho ya katiba na ya sheria ya uchaguzi. Maswali mawili na yote yanatokana na ufahamu mzuri wa mambo katika nchi yetu:

1) "Je unadhani ni namna gani tume huru ya uchaguzi inaweza kuundwa, kufanya kazi kwa uhuru na pia kuhakikisha watendaji na watumishi wake hawafungamani na chombo au watu wowote wale?"

2) Je tume hii huru itapata wapi fedha za kujiendesha? Maana ukweli ni kwamba mlipaji ndiye mwenye sauti na ukisema utaitegemea serikali kuifadhili tume hii, tayari tutakuwa tumesharudia matatizo yanayoikabili sasa!
 
Hivi ni nani anaye wachagua hao watu wa tume! are they appointed by president!????:bowl::bowl::bowl: Mmmmh this will never work!

Ni Rais. kama ilivyo Chief Justice, etc. Hizi taasisi ni bora wajumbe wake watokane na councils au commissions huru zitakazoshirikisha wajumbe kutoka kila sekta na hasa vyamna vya siasa.
 
ndugu zangu wakati umefika watanzania tukaadamana kutaka tume huru ya uchanguzi iliyoundwa bila kushirikisha serkali iliyoko madarakani.tunahitaji mabadiriko ya katiba kuhusiana na mambo ya uchanguzi.

Tume iliyopo ni huru , ni uwoga wenu na dhana mlizojenga , jipangeni wekeni watu makini. TUME HAINA SHIDA NA 2015 ITAKUWA HII HIII, TUWAMALIZE TENA KAMA HII 2010.
 
Tanzania kuna Utulivu tuu si democrasia( Passive resistance) Hatutaki yanayoendelea lakini hatuwezi ongea lolote na haya ndo madhala ya ucommunist (the products of communist brain wash!)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom