Tunahitaji tume huru kwa tukio la dr ulimboka sio usanii wa kova!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji tume huru kwa tukio la dr ulimboka sio usanii wa kova!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eumb, Jul 14, 2012.

 1. eumb

  eumb Senior Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana baada ya kusikia taarifa za kukamatwa kwa jambazi eti aliyekwenda kutubu kwa Mch Gwajima kuwa ndiye mhusika wa kumteka na kumtesa Dr Ulimboka, niliamua kurudi JF nakutafuata ile thread iliyo na video clip ya Dr Ulimboka Ushuhuda wa Dr. Stephen Ulimboka - YouTube akijeleza jinsi tukio zima lilivyotokea. Nimesikiliza na naomba kila mtu asikilize tena kwa makini halafu tujiulize maswali. Kwa upande wangu nina haya yafuatayo;

  1. Dr ameeleza jinsi alivyokuwa anawasiliana mara kwa mara na mtu aliyefanikisha yeye kufika Leaders Club usiku ule. Tena anasema mawasiliano yao yalianza wakati wa mgomo wa kwanza, je kweli polisi wanaweza kutuambia mtu huyo kwa kujaribu kufuatilia kwenye mitandano ya mawasiliano hawajaweza kumpata? Kwa jinsi ilivyokuwa ni lazima yeye ndio aliunganisha watekaji.

  2. Dr anakumbuka watu waliomteka na hata wakati wa kumtesa hawakuwa kumi na mbili, tena walimuamisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, sasa hilo jambazi la Kenya limepata wapi figure ya 12?

  3. Dr anasema walipomtesa walikuwa wanamwambia unatusumbua sana wakati tulishasaini makubaliano, je makubaliano yapi? Unafikiri ni ya wagonjwa na madaktari? Hapa, je watanzania tuliwahi kufanya nao makubaliano? Hapa, makubaliano pekee ninayoyakumbuka ni kati ya Madaktari na serikali, correct me if i'm wrong!

  4. Haingii akili eti Jambazi linataja idadi ya waliokwenda kumteka na kumtesa lakini hawakumbuki kwa sura!! Jambazi mzoefu kutoka nje ya nchi aliyekodiwa kwa special task hawezi kuwakumbuka waliompa ajira? Kwa kazi kama hizo lazima kuna makubaliano fulani ya awali sometimes part payment na watu waliomuunganisha kuja kufanya kitendo kama hicho, kweli hata hao hawakumbuki?
   
 2. w

  why JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni hatari kwa nchi kuwa na jeshi la polisi lililoingia katika siasa,imefahamika vyombo vya habari kutangza kukamatwa kwa anayesadidkika kumteka Dr Ulimboka,ndugu zangu naomba muelewe sasa inchi imefikia pabaya,ukweli ni HUU.
  Aliyekamatwa ni mkenya amabaye ameandaliwa na serikali ili kufuta ukweli wa serikali kuhusika na kiteno hicho.alikamatwa kwenye kanisa linaloaminika kuwa ni la mtu wa usalama wa taifa akiwa hapo kwa lengo la kutubu dhambi zake hii ni njama kwani ni kanisa gani linalotoa siri za wadhambi.ameahidiwa kuondolewa nchini pindi upepo huu utakapopungua hasa watanzania kujadili swala hili ikizingatiwa wengi kuwa na hasira na serikali.Hatua iliyofikiwa na serikali ni mbaya kwani hadi sasa wamebadili mfuo wa kuhakiki wapigania haki hasa viongozi wa vyama vya siasa kutafutiwa mbinu nyingine ya kuhakiki wanaondolewa duniani,hii ni baada ya mbinu zao kugundulika hivi karibuni na viongozi hao kutoka hadharani na kutoa tahadhari dhidi ya usalama wa taifa.Napenda kutoa angalizo kwa vyama vya siasa pindi wanapofanya harakati zao vema wakachukua tahadhari ikizingatiwa kutafutwa na watu wasio wajua.
   
 3. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Go to hell Mr. Kova, I am not stupid as you think.
   
 4. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kova adhihirisha hili kwa kuleta inteligensia ya uongo mbele ya waandishi ya wahabari. inawezekanaje kwa mtuhumiwa kwenda kanisani kutubu kufanya kosa ambalo atakuwa matatani pili katika simu ya mkenya huyu anAyejidai ndiye aliyehusika na kumteka dr ulimboka kuna message nanukuu '' NIMESHAFIKA NAJARIBU KUWAZOEA'' inavyoonyesha dhahiri huyu mkenya feki wa TISS+polisi/kova. Alienda pale kwaajili ya kujikamatisha ili ionekane sio seriali imehusika na uteaji huu wa dr ulimboka. tatu naona sasa inteligensia zinaanza kutumia makanisa kufanikisha uozo wao kumtuma mtu kanisani akajisalimishe ili kuaminisha umma kwamba ni kweli kwa mtu ambaye ni proffessional kutesa watu hawezi kufanya kitu hiko. tatu kumbuka Dr ulimboka alipohojiwa alisema anamfahamu mmoja ni afisa wa polis. CHANGANYA AKILI ZAKO NA ZA KOVA usiamini uongo huu wa intelegensia za kitoto. USIDANGANYIKE HIKI NI KIZAZI KIPYA.
  NB: "kama wanataka intelegensia za kisasa wajaribu kunitafuta am professional kutengeneza"
   
 5. m

  muafaka Senior Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ingekuwa vema hata ukajifunza lugha ya kiswahili vizuri maana ni lugha ya Taifa.
   
 6. k

  kbhoke Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Serikali ya kisanii iko kazini!
   
 7. m

  mambomoto JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Inatia hasira sana kova anavyotufanya watz kama viazi hatunazo. Sakata la Dr. Uli anakuja na ngonjera kama za jana kuhusu mtekaji ni Mkenya. Wanamdanganya nani na kutaka kuharibu picha yote kwa taarifa za kitoto kama zile? Ukimwangalia hata alivyokuwa anaelezea utagundua tu hii ni picha imetengenezwa halafu kabla ya kukamilika ikapelekwa sokoni.
   
 8. r

  richone Senior Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  maumivu yangu yaliyo moyoni nimeamua kuwashirikisha wanaJF na hii inatokana na mambo yote mabovu ambayao yamekuwa yakifanywa na hawa askari wetu wakiongozwa na Mwemana na kova kama tarumbeta lao.
  naumia sana ninapomuona huyu mjinga Suleman Kova ambapo amekuwa akitudharau na kutuona sisi watanzania wote kuwa ni mambumbumbu hatujui chochote hatuoni, hatuelewi kiasi cha kuweza kutudanganya na kutufanya sisi ni was-nge kama yeye mimi nimeapa na mungu anisaidie siku nikikutana nae usokwa uso nitamshughulikia wacha wanisweke ndani mimi sina wasiwasi.
   
 9. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana, usihofu, subiri wajaribu huu ujinga wao mpya wanaotaka kuufanya dhidi ya Chadema, kudadadeki, yaani tutawazima kwa awamu kimyakimya, mpaka watashangaa, yaani leo huyu, kesho yule, mpaka wakiri makosa yao na wawataje wahusika wao wakubwa kabisa, wanaowatuma ili tusafishe hao wajinga kabisa tubaki na Tanzania yenye viongozi wa kweli, sio madictator
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  husiwe na wasi mkuu utakutana naye tu, c unajuwa ana makengeza!
   
 11. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yani hukuelewa? unahitaji kujifunza kiswahili.
   
 12. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Hata mimi.naskia huyo mkenya ataitaja chadema kuwa ndo walomtuma,halafu mwisho wa siku mkenya anaondoka na fungu kwa kufanikisha usanii..SERIKALI DHAAIF
   
 13. M

  Malova JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  SCRIPT hii ya KOVA kuhusu Dr. Ulimboka, move yake haichezeki. Ingekuwa Ulimboka hajaongea hata kidogo juu ya swala lililotokea ingeingia akilini juu ya alichoongea. Kama alikuwa anakwenda kutubu kwa Mchungaji, inakuwaje kutubu kwake kujulikane. Taratibu za mtu anapokwenda kutubu dhambi zake kwa mchungaji, mchungaji hatakiwi kutoa njee juu ya alichotubu kama ilivyo kwa madaktari unapotibiwa hatakiwi kutoa siri ya ugonjwa wa m2. Hii ni script iliyotengenezwa amabyo sis watz tunaona kabisa move yake haiwezi na wala haitaweza kuchezeka.
   
 14. s

  sambu JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Kwa wale mnaokumbuka hadithi ya wafanya biashara ya madini na RPC wa wakati huo hadithi zinafanana kabisa. Hawa jamaa hata kutunga uongo hawawezi hata kidogo. Yaani wanaigiza kudanganya watanzania.
   
 15. M

  Magesi JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kova ni janga la kitaifa
   
 16. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  naogopa kutoa maoni maana nitatukana!
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  shangaa na wewe?!!!! ni aibu kubwa sana!!!
   
 18. H

  Hydrobenga JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 1,124
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Naunga Mkono Hoja namba moja


  Hoja namba mbili ni kama ifuatavyo :- inawezekana waliopanga dili ni 12 lakini walioenda kumteka Dokta Uli wakawa chini ya 12.....fikiria vizuri kuhusu hili

  Hoja namba tatu ni kama ifuatavyo :- inawezekana waliomteka ni maajenti wa serikali au isiwe hivyo..maswali
  aliyoulizwa DKT uli wakati wa utesaji hayawezi kuwa ushahidi wa kuthibitisha ushiriki wa serikali....Hata wewe unaweza kumteka DKT uli kisha ukamuuliza hayo maswali kwa malengo tofauti...fikiria hili vizuri  Hoja namba 4 ni kama ifuatavyo:- Inaonyesha wazi mtoa hoja ni mgeni wa mbinu za kimafia na kihalifu.....inawezekana
  tena sana..kufanya uhalifu wa kutumwa na usijue nani alikutuma na malipo yako ukayapata kamili...Pia unaweza kabisa kufanya kazi na watu kisha usiwakumbuke.....

  Hitimisho:- Polisi wana uwezo mkubwa wa kuwakamata wahalifu wote...inategemea tu iwapo wanayo Dhamira hiyo au la

   
 19. Rasib

  Rasib JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani haidanganyi kabisa
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Watanzania tumezidi ukondoo, na bado wataendelea kutudharau mpaka watatutia vidole vya mattako.
   
Loading...