kwa mda mrefu jiji la Dar hukumbwa na mafuriko katika mto msimbazi yanayopelekea nyumba kadhaa kando kando ya mto msimbazi kuzingirwa na maji huku baadhi ya barabara kama magomeni eneo la jangwani kutopitika.
inashangaza kuona serikali inapanga kujenga daraja jangwani kama ndiyo suluhisho la jambo hili kwa kutatua shida ya usafiri tu na kutelekeza matatizo mengine.
Dar es salaam siyo ya wenye magari tu kusema waliojenga mabondeni shauri yao watafute pa kwenda bali tunahitaji kuondoa mafuriko mto msimbazi ikiwezekana kwa kuujengea mto msimbazi ili udongo usimomonyoke na kuziba mitaro na pia magugu na miti maji vinavyoota kuzuia maji kusafiri kwa kasi.
pia tunaweza kujenga mabwawa ya kutunza maji haya ili yasiganganie kukimbilia baharini kwa wakati mmoja.
tunahitaji kufikiri zaidi ya kuona magari yanayokwama na kuona nyumba zinazozingirwa na maji kama ni matatizo tuliyoyatengeneza wenyewe kwa kutokuwaelekeza hawa ni wapi sehemu sahihi ya kujenga kupitia mipango miji na hivyo ni wajibu wetu sote kutafuta suluhisho la mafuriko