Tunahitaji siasa za kiutendaji na si utendaji wa kisiasa

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,326
4,146
iTanzania hii kila mtu hapa nchini ni mjuaji, kila mtu anajua, Kila mtu anakosoa, kila mtu ana muelekeo na nchi hii lakini mara zote hizi zimekuwa ni propaganda za mdomoni tu na wala hakuna utendaji wa aina yoyote juu ya changamoto ambazo hao wajuaji wanaziorodhesha.

Nataka nikiri wazi kwa wakati huu hakuna mwanasiasa anayeweza kubipimishana msuli na Rais Magufuli,hayupo. Wendi wao hujaribu tu kuangalia madhaifu ya Rais tu na kuacha kuambatana naye katika mazuri mengi ambayo anayasimamia katika nchi yetu ya Tanzania.

Pengine Rais Magufuli hana lugha tamu masikioni pa wengi, pengine hana muonekano mzuri we kisiasa, pengine anawaumiza sana sana wanasiasa wengi, pengine so mtendaji mzuri wa kisiasa ila ni mwanasiasa mzuri kiutendaji.

Ni kiongozi mwenye upeo na dira, hakuna mtu anayehitaji udhahiri katika mambo yake akampuuzia mtu kama Rais Magufuli, yeye hapindishi pindishi hali yoyote inayoikabili jamii katika kuitatua.

Hakika tunahitaji mtu Rais Magufuli. Sijawahi kuwa na mapenzi na CCM ila Rais Magufuli atakuwa mtu wa kwanza nianze kumpenda kwa hakika ndani ya CCM. Najua wana CCM wengi ni watu wa mkumbo hivyo ninafurahi wakati huu watakua kwenye mkumbo unaowatesa
 
Wmbu taja maendeleo matatu tu (3) ya mtu wa kawaida yaliyoletwa kwa miaka mitano iliyopita.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom