Tunahitaji sheria ya kudhibiti Safari za rais,Tumeongea sana humu javini, sasa ni vitendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji sheria ya kudhibiti Safari za rais,Tumeongea sana humu javini, sasa ni vitendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NtakuwaSikuchukui, Feb 23, 2012.

 1. NtakuwaSikuchukui

  NtakuwaSikuchukui Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuongea jamani tumesema sana juu ya safari za rais huyu,ni kweli safari nyingi ni wazi ni kukwepa majukumu yake ya kushughulikia kero za watanzani, kwa kuogopa kugombana nao waliomweka madarakani.Safari nyingi zisizo na msingi ni upotevu mkubwa wa kodi za watanzania,inafika mahali ndege inachukuliwa kama boda boda,umelala umeamka unasema unaomba ufikishwe maramoja Uk au Marekani wakati tangu ameingia madarakani amezidi kuwaweka kwenye umaskini mkubwa watanzania hadi sasa navyo ongea hali ni mbaya ya uchumi.

  Sina mengi ila ni waombe wana JF na hasa sana wale wabunge na viongozi wengine kuna haja ya kuwa na sheria itakayosimamia safari zote za rais au waziri wa mambo ya nje ili kuokoa upotevu usio wa lazima wa kodi za watanzania.Sheria hiyo ibainishe:
  • Safari za msingi kwa viongozi kupanda ndege kulingana na vigezo mbalimbali vitakavyowekwa kama vile hali ya uchumi,matatizo ya ndani ya nchi yanaitaji utatuzi wa haraka n.k
  • Idadi maalumu ya watu watakaopata zali kupanda ndege kulingana na majukumu yao husika kwa taifa,ambayo itazingatia hali halisi ya uchumi na mambo mengine.Hapa sio kuwapa watu zawadi ya kupanda ndege kiolelaolela kama ilivyo sasa hata kama hausiki.
  • Rais hanabudi kugeuza haraka sana tena sana pale matatizo yanapotokea nchini na hakuna mtu wa kutatua ila yeye rais.mfano mgomo wa madaktari,rais alikuwa bubu na kuchelewa kutatua tatizo ilo.
  • TUENDELEZE MENGINE HAPA.............
  Sheria ni mwisho ya yote pasipo sheria mambo yatakwenda kiolelaolela na kuleta hasara kwa Taifa
  MNAONAJE WANA JF?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sasa tunaye rais kilaza ambaye anafikiria kuonekana kwenye majukwaa ya kimataifa ndiko kunakotuwekea chakula mezani what do you expect. Next time tuhakikishe tunachagua mtu makini. Hakuna sababu za kuweka sheria.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  There is a need for presidential trip to be moderated somehow, planned and ad hoc as well

  He is too much sasa, can you imagine?
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hatuhitaji sheria kama hiyo.
  Tunahitaji kuchagua mtu mwenye uwezo wa kushika madaraka ya Urais na mwenye upeo wa kuongoza nchi na ndoto za kulikomboa Taifa kutoka katika lindi la umasikini.
  Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 6 sasa pale Ikulu tuna Gharasha lenye umbo la JMK.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Sasa si Mngojee wakati wa Uchaguzi? mumchague Rais mnayemtaka? Unaweza kumuhukumu Hakim akiwa yupo kazini kwake Mahakamani?
   
 6. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu hukumsomaga mtu mmoja hapa jamvini anaitwa "Hutaki Unaacha"
  ana masilizi yake kwenye barua anazomwandikia JK!
  Huko juu kwa wafuma mfumo hamna kitu kama hicho eti chaguo la wananchi, mabadiliko hayaletwi na sanduku la kura!
  Hivyo kama pia hamna uwezekano wa kuingiza sheria za kujitetea japo hata kidogo basi tuendelee kulala tu sababu hatutaamini kitakachotokea 2015.
   
 7. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ziwe zinaidhinishwa na bunge
   
 8. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ingekuwa nchi yetu iko Afrika Magharibi ambako wenzetu wana wanajeshi walioamka huyu JK angekuwa kishapinduliwa
   
 9. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  mlimchagua wenyewe hakuanza leo kuzuzura ktk hawamu ya pili.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  I agree with you Jasusi that our country needs a leader who thinks using his head and nothing else!!
   
 11. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sheria hiyo nchi hii haitakuja kutokea. Nafasi hiyo ni ya ulaji, si unaona wenzako wanavyopigana vikumbo kwa ajili ya 2015!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Nyie pigeni kelele mwisho wa siku nani wa kutunga hiyo sharia !? kama hao ndugu zenu magamba ! kina tundu lisu walimsifia Rais bungeni na kuwasihi wenzake kupitisha muswada wa sharia ! leo nani wa kutunga na kupitisha kanuni hizo za katiba! mwacheni mheshimiwa Rais ajinafasi ! ponda mali kufa kwaja RAis wetu mstahiki!
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi tunavyofilisiwa na safari za rais zisizoisha sheria ya kudhibiti safari zake za nje inahitajika.
   
 14. M

  Makunga JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 772
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 80
  Nadhan ktk dunia nzima watz ndo tuna rais kilaza mchumia tumbo.Hili linchi mi limeshanichosha nataman ht vita itokee tuvuruge kl kitu hlf tuanze upya.
   
 15. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  arooo.. yaani unareta maneno ya uchochezi.. yaani unariambia geshi ripindue nchi..? majenerali ni makada ya magambaa.. harafu nayo yanaiba hayo.. arooo hayapindui haya maji2..
   
 16. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete leo ataungana na viongozi wakuu wa Serikali na nchi 50 pamoja
  na mashirika ya kimataifa, katika mkutano wenye lengo la kupata suluhisho la kimataifa katika mgogoro wa Somalia yenye uongozi wa mpito chini ya Sheikh Sharif Ahmed.

  Mkutano huo umeitishwa na Uingereza kuzungumzia hali ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ambayo haina Serikali kwa zaidi ya miongo miwili na kwa sasa imegeuka kuwa maficho ya
  ugaidi na uharamia.

  Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi wamekubali kushiriki katika mkutano huo unaotarajiwa pia kuhudhuriwa na
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hilary Clinton na Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa, Ban Kimoon.

  Khabari ndio hiyo , na source Habari Leo!
   
 17. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,216
  Likes Received: 10,579
  Trophy Points: 280
  Tuombe Mungu 2015 ifike mapema pamoja na mchakato mzima wa katiba uende salama....
   
Loading...