Tunahitaji Sheria ya Haraka, Sera na Mjadala Mpana wa GMO Tanzania

Verily Verily

Senior Member
Jan 4, 2007
188
143
Teknolojia ya Uhandisi Jeni au Genetically Modified Organisms (GMO) inaenea kwa kasi sana dunia kote katika Nyanja za Kilimo (Mbegu za Vyakula), Afya (Madawa na Chanjo), Biodiversity (Bayoanuai yaani maisha ya viumbe hai vyote, mimea, wanyama, wadudu nk).

Uhandisi Jeni huonekana kama teknolojia yenye faida. Hata hivo madhara yake ni makubwa kuliko faida, japo dhana hio wengi hawataki kuikubali au kuiongelea.

Madhara ya magonjwa yatokanayo na vyakula vya GMO ni makubwa mno kuanzia kwenye Kansa, Allergies, Ugumba, Magonjwa ya Kuzaliwa (Congenital Anomalies) nk. Ijulikane kuwa baada ya muda mfupi madhara ya GMO yatapita madhara ya Virusi vya Ukimwi miaka michache iliyopita!

Madhara ya baadae zaidi ni Njaa ya Dunia (Global Famine) baada ya mbegu zote za asili za mimea na wanyama kutoweka na GMO kutopatikana kwa wenye kuzihodhi kasa kampuni ya Monsanto na hapo ndipo dunia nzima tuseme itaangamia!

Ni wakati mwafaka sasa kwa Serikali kuchukua hatua za Dhati, Kina na Makusudi kupitisha sheria na sera juu ya Uhandisi Geni ikiwa ni pamoja na kuanzisha mjadala mpana kuhusu mwelekeo wetu kama taifa kuhusu GMO.

Mambo ya haraka kwa sasa hata kabla ya Sheria/Sera ni kuhakikisha:
1. Chakula chenye chembe za GMO kinakuwa na Label ya "GMO"
2. Mamlaka za udhibiti kama TFDA/TBS nk kuwa na Uwezo wa kugundua GMO katika vyakula/mbegu
3. Mbegu za GMO hazisambazwi kwa wakulima mpaka Sheria/Sera ya kitaifa ipitishwe
4. Tahadhari nyingine zinachukuliwa.

Mwisho, inabidi kupaza sauti zetu sote kwa ajili yetu na vizazi vijavyo. Kusema tumesema, watu wasije wakajuta na kulalamika baada ya madhara kuwa makubwa na yasiyoweza kudhibitiwa tena. WAKATI WA KUCHUKUA HATUA NI SASA!!
 
Back
Top Bottom