Tunahitaji majasusi na magaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji majasusi na magaidi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zing, Jul 2, 2009.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nawasilisha hoja ya ajira ya magaidi na majasusi.ambazo nadhani ziko wazi

  Naposema magaidi na majasusi ninauhakia serikali yetu inaoa majasusi wakulinda utawala. serikali yetu ina majasusi wa kisiasa na majasusi wa aina hii amabao hawana mchango mkubwa kwenye maendeleo ya taifa

  Inabidi wawepo majasusi na magaidi wa kiuchumi na wa kitamaduni. Nadhani nafasi hizi ziko wazi na serikali haina ndo maana watani zetu kenya wanatuzidi kwenye utalii na watanatumua ujasusi na ugaidi wa kiuchumi kupata faida kubwa zaidi yetu

  Nasema ugaidi wa kiuchumi sababu mbili kubwa watalii wengi wanataka kutembelea mlima kilimanjaro si tu wanapitia kenye lakini hata makampuni ya kuwatembeza ndani ya tanzania mengi ni ya kenya. Kwa ugaidi wa kiuchmi kenya inaofanya usishangae hata watalii wengine wanatembelea tanzani bila kujua kuwa wako tanzania.sisi tumekalia kwenye ujasusi wa siasa tu.


  ugaidi wa kiuchumi unahitajika kufanyika kwa vitu , biashara na watu wanao potosha ukweli na hivyo maslahi ya kiuchumi kwa nchi yetu.Wenzetu wanfanya ndo maana wanafanikiwa sisi tumelala.

  Pale ambapo hakuna tatizo basi ifanyike ujasusi wa kiuchumi na kitamaduni ili kulinda image , biashara na maslahi ya tanzania yasiwe compromised.


  Ukitoa ujasusi na ugaidi wa kiuchumi kati ya nchi zetu za kiafrika kuna ugaidi mwingine kutoka mataifa ya nje na taasissi zao kama WB,IMF, EU nk. Mfano wa ugaid tuliofanyiwa ni kukatazwa kutoa ruzuku kwa wakulima lakini inashangaza wakulima wa ng'ombe wa matunnda huko ulaya wanapokea ruzuku. sasa kwa kuwa tumekuwa tunafanyiwa ugaidi wa kiuchumi na tumeshindwa kuhimili tunahitaji majasisi wengi zaidi kwenye sekat za uchumi utamaduni na hata michezo.

  China imetumia sana magaidi na majasusi wa aina hii kujipatia maendeleo. Kuna jasusi 1ja wa kichina kafungwa mwaka jana nadhani marekani. alikwua jasusi wa kuiba teknolojia. Huu ndo mfano ninaosema.

  Dunia ya sasa ni ya ushindani hakuna fair play. kwenye balozi zetu wawekwe econimic,sports and cultural attache na wapewe majukumu yatayoleta mabadiliko nyumbani Tanzania. ukweli ni kuwa duni hii sio huru.

  Nadhani tutapata faida zaidi kwa majasusi na magaidi wa aina hii kuliko wale wengine .
   
 2. Sanjara Honey

  Sanjara Honey Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  Dah! Kweli wengine chongo huita kengeza. Nashangaa mada nzuri kama hii inakosa wachangiaji hapa JF. Tumebobea kwenye pokopoko, mambo muhimu sijuhi tumemwachia nani?

  Kwenye orodha yako ya ugaidi na ujasusi wa kiuchumi, Kenya hawaibi utalii tu bali hata mazao. Sisi kwenye sekta ya maua na vyakula (Asali, Mboga mboga, matunda) tumelithibitisha hilo. Ninazo reports za kenya zikionyesha jinsi sekta ya maua ilivyokuwa kutokana na maua yanayotoka Tanzania, ninaoushahidi (ambao serikali pia inao) jinsi Mboga mboga na matunda ya Tanzania yavyopelekwa Ughaibuni kwa jina la Kenya na si Tanzania, nimesoma Strategic Plan ya Kenya Honey Council Ltd inasema wazi, mkakati mkuu wa kuongeza asali inayouzwa kwa jina la Kenya ni kuhakikisha wanapata asali yote nzuri toka Tanzania.

  Nitoe wito kwa wale wote wanao ona uzito katika hoja ya thread hii, ebu tufanye kitu kwa ajili ya vizazi vijavyo na taifa letu. Maneno mengi (pokopoko), lawama lukuki havijengi bali kuzidisha uhasama na kubomoa umoja tuliokuwa nao kama taifa.

  [​IMG]
   
  Last edited: Jul 3, 2009
 3. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
 4. Sanjara Honey

  Sanjara Honey Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  kumbe hata hizi ziara za nje ya nchi anazofanya Mh. Rais,kwa kisingizio cha kuvutia wawekezaji, zingepunguzwa na bajeti yake ikatengwa kuandaa competent cadres kwa ajili hiyo.
   
 6. Sanjara Honey

  Sanjara Honey Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  Tanzania ina ukosefu wa Wafanyabishara wa Dalaja la kati na wazawa wa dalaja la juu. Mara zote convoy ya Mh. JK imekuwa inakwenda na wafanyabiashara wa juu na kila mara ni walewale. Ni vema wanaoandaa safari hizi wangeshirikisha na vijana wanaoshipukia. Tatizo letu kubwa sisi (dot.com generation) wa dalaja la kati ni "limited exposure" basi. Ukitupa nafasi hiyo tunakwenda mbali sana na kwa muda mfupi. Rais Kagame analijua hili na hana ajizi katika kuwashirikisha vijana ipasavyo.

  [​IMG]
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu mnaolalamika sijui mmekuwa members kwa muda gani na sijui mnafuatilia post kwa kiasi gani. Hizo habari ambazo mnaona hazijadiliwi au hazichangiwi zimechangiwa sana ana wadau huko nyuma, sio hadithi mpya. Mengine ni mambo ambayo hayana haja ya kujadiliwa kwa kuwa yako wazi. Soma jinsi Umoja Wa Wanawake ulivyojadiliwa toka uongozi wake na utendaji wake mpaka muundo wake, na uozo ulioingia unaweza kuona kuwa hakuna jipya.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jamani mimi niliwahi kutoa thread kuhusu jinsi kitengo cha ujasusi wa kiuchumi cha CIA kilivyo isambaratisha Nyumbu yetu iliyokuwa imeanza kupata uhai miaka ya 80. Walichofanya, waliirubuni serikali ya TZ chini ya Mzee mwinyi kwamba itawapa technolojia mpya ya magari, na pia waliisha mnunua meneja wa nyumbu wakati ule, serikali kama kawaida ikakubali, lakini lengo la wamarekani ilikuwa tusiweze kutegeneza magari ya kijeshi, na baada tu ya wao kuona tumeingia mkenge wakajitoa na pesa walizo ahidi hawakutoa na ndo ukawa mwisho wa nyumbu.

  Economic intelligence ndiyo inasaidia nchi kujua nani anategeneza nini na anachokitegeneza kinaathiri vipi uchumi wa nchi yako na ufanye nini ili either umzidi au muwe sawa. Sisi serikali yetu chini ya CCM wamelala fofofo, wanadhani WB, IMF, n.k. inawapenda, hakuna....inatumaliza.

  Kuhusu jirani zetu, wala tusibabaike isipokuwa tujifunze kwa haraka na tutaendanao sambamba, wasi wasi wangu ni kuwa hatuna rais wala waziri mkuu wa kuthubutu, wao ni siasa tu....

  Hapo tunamkumbuka Lowasa pamoja na matatizo ya richmond lakini alikomaa mpaka mradi wa maji wa ziwa victoria ukaanza ingawa misri na UK zilikuwa zinapinga vikali. Kitu cha kushangaza, Kwa nini nchi zingine mashirika ya umma yanafanya vizuri lakini TZ mashirika ya umma yanakufa?? Hapa ndo kuna tatizo, na labda niseme tu kwamba hii imechangiwa na tabia ya CCM kuchukua pesa kila wakati wa uchaguzi na hiyo inwapa mwanya viongozi wa mashirika na wao kuchota kiasi wancho taka.......sina muda wa kutosha.....
   
 9. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Ni kweli kwamba tunachohitaji ni ujasusi wa uchumi,badala wa kisiasa.
  nchi nyingi za mashariki ya mbali baada ya vita baridi "cold war" zilibadilisha
  mbinu za kijasusi wakaanza ujasusi wa kiuchumi kuiba teknolojian.k
  lakini kabla ya hilo walikuwa wamejiandaa vyema waliwekeza vichwani mwa watoto wao "Kielimu" ili waweze kumudu kuiba teknolojia ya nchi za magharibi.lakini sasa sisi watoto wetu tumewapuuza vijana wetu walioko vyuoni tunawapuuza wanapotushauri dawa ni kuwavurumishia virungu vya "FFU". wale wakubwa waliokimbizia watoto wao ulaya wakapate elimu waliowengi wanaishia kulewa na kula madawa ya kulevya.
  Haya mambo tunatakiwa tuyaweke sawa kwanza,ujasusi ni kazi nyeti sana ukikurupuka utaenda na maji hata kabla hujanusa kitu.sasa kwa hali ya maandalizi kwa vijana wetu tusipoliona hilo hatutaiba teknolojia yoyote.
   
Loading...