Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Nakumbuka Rais Kikwete alipoulizwa msimamo wa Tanzania kuhusu Mashoga, alizungumza kidiplomasia kwamba Watanzania bado hawajawa tayari kuhusiana na mambo hayo.
Naye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe alisema wazi kwamba Watanzania hawataki ushoga na waliwakatalia wazungu walipojaribu kuipenyeza ajenda hiyo kinyemela..Sasa leo tunapoambiwa tulisaini mikataba ya kimataifa kutambua Haki za Binadamu ikiwemo ushoga. Nani alisaini? Kikwete? Mbona hatukujulishwa?
Tamko la Wizara ya Mambo ya Ndani limejikuta indirectly linathibitisha kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokubaliana na suala la ushoga kama haki nyingine za binadamu. Yaani kama ni siri basi imebumburuka!
Huu ni ukombozi kwa wahusika wa vitendo hivyo. Kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi kwa kunyanyapaliwa na kuonekana hawafai lakini kumbe serikali imesaini mikataba na jumuiya za kimataisha katika kuwatambua na kuwapatia haki zao.
Nashauri kuanzia sasa;
1. Zile NGOS zilizokuwa zikiwapatia washiriki wa mapenzi ya jinsia moja vilainishi na elimu kuhusu njia salama za kushiriki ngono bila madhara sasa zisibughudhiwe tena..
2. Polisi wawakamate na kuwafikisha mahakamani wale wote watakowafanyia dhihaka na kuwabughudhi mashoga
3. Sheria zinazokataza mapenzi ya jinsia moja zifutwe na adhabu ziondolewe
4. Jamii ielemishwe umuhimu wa kutambua haki zote za binadamu na kuziheshimu
5. Serikali iwe inawashirikisha wananchi kwa uwazi kuhusiana na mikataba mikubwa inayoingia na Jumuiya za Kimataifa ili kuepusha migogoro isiyo na ulazima.
Najua hili jambo ni zito na lina utata mkubwa hata huko juu kwa wakubwa hivi sasa. Naamini JPM amefura kwa hasira, lakini atafanyaje? Itambidi akubali tu, ndivyo mambo yalivyo!
Njia mbadala tuliyonayo ni kupitia upya mikataba ya kimataifa na kubadili mambo tusiyoyakubali kama taifa. Lakini tujiandae na consequences maana sisi ni taifa nyonge mbele ya wababe.
Swali muhimu ni; Je, tuko tayari kwa lipi?