Tunahitaji kuwa na mfumo wa mabunge mawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji kuwa na mfumo wa mabunge mawili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Jun 29, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wajumbe nilipenda kwenye katiba mpya tulipigie mchapuo swala la tanzania kuwa na mabunge mawaili la kila moja kuwa na wabunge chini ya 80 na ili kuongeza usimamizi wa serikali na kupunguza gharama ili taifa likuwe. kwani mabunge mawili yatapunguza pia ukilitimba wa bunge moja kudhani ndio linalokuwa na hati miliki ya taifa
   
 2. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Kwahiyo tutakua na mawaziri wawili wawili kila wizara... Mawaziri wakuu wawili... Spika wawili... Wanasheria wakuu wa serikali wawili.... Majengo ya bunge mawili...
  Umefikiria kweli!?
   
 3. T

  Tata JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Hatuhitaji mabunge mawili. Hili moja tu limejaa upupu ukiweka mawili ndio kabisa. Kwa mtazamo wangu tunahitaji kulipunguza hili bunge wabaki wabunge ishirini na moja wakiwakilisha mikoa au wachache zaidi ya ishirini wakiwakilisha majimbo kwa utaratibu utakaokubalika. Wabunge wasiwe waajiriwa wa muda wote kama walivyo hivi sasa. Wawe na kazi ya kusimamia serikali kama ambavyo Bodi za wakurugenzi zinavyo simamia makampuni. Spika ndiye atakuwa mwenyekiti wa bodi. Baraza la mawaziri ltawajibika kwa bunge na watakuwa na wajibu wa kuwaajiri na kuwaondoa mawaziri kwa mikataba maalumu ya utendaji (performance contracts). Kwa mtaji huo mawaziri hawatakuwa wanasiasa bali wataalamu wa sekta wanazosimamia na watapatikana kwa utaratibu wa wazi wa kushindanisha watu kwenye interview.
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  haimaanishi kuwa na mabunge mawili kila moja lazima liwe na ukumbi wake kwani ukitazama katika bunge letu la sasa kuna kumbi nyingi ambazo mabunge yote yanaweza kulitumia na pia tunaweza kugawa muda wa bunge moja kukaa kwa mfano bunge moja linaweza kuwa ni bunge la kutunga shaeria na lingine ni la bajeti sasa hili la kutunga sheria wabunge wake wanaweza kukutana mara mbili tu kwa mwaka na vikao visivyozidi mwezi mmoja . na hili la bajeti pia linaweza kukaa mara mbili tu kwa mwaka bajeti kuu na bajeti ya dharura. pia kama kila moja likawa na wabunge 80 ina maana mabunge yote mawili yatakuwa na wabunge jumla ya 160 wakati sasa bunge moja linakuwa na wabunge 360 hii ina maana kutakuwa na punguzo la wabunge 200 kwa hiyo ukiangalia na siku za vikao vyake zinavyopungua tunaweza kupunguza matumizi ya bunge kwa zaidi ya asilimia hamsini( 50%)
   
 5. Ibrahim K. Chiki

  Ibrahim K. Chiki Verified User

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Dawa si mabunge mawili, tunachotakiwa kufanya ni kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni. thats the only solution...
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hivi wabunge waTanzania wanafanya kazi gani??? Je ni sheria gani imeanzia bungeni na ni budget gani imewahi kubadilishwa au kukataliwa na bunge!!!. Bunge ni wawakilishi ambao hawana nguvu zaidi ya kutumia pesa za masikini wa Tanzania na kupiga kelele!!. Hakuna kitu wanachofanya
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  tunapokuwa na mabunge mawili tunaweza kufika wakati tukatunga sheria ya ni namna gani ya kupata wabunge wazuri kwa mfano hili la kutunga sheria tunaweza kutenga nafasi 20 kwa ajiri ya walimu mabingwa wa sheria kutoka vyuo vikuu vyetu hii itasaidia kwani wabunge wengi ni watu wasio na misingi ya kufahamu sheria
   
Loading...