Tunahitaji kufumuliwa na kuundwa upya kwa TAKUKURU na DPP, na sii Mahakama ya Ufisadi

LENDEYSON

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
2,996
2,659
Kumekuwa na taarifa za kukamilika kwa mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi. Swali ni kama tunaihitaji Mahakama hii kwa sasa ilihali kuna Mahakama zenye uwezo wa kushughulika na Jinai zote.

Maoni yangu ni kuwa, suala la Ufisadi ni gumu na zito, ila ukweli ni kuwa, mahakama zilizopo hazijashindwa kushughulikia. Wanaoshindwa katika suala hili ni TAKUKURU pamoja na Ofisi ya DPP.
Kesi nyingi za Rushwa huitaji go ahead ya DPP, hali inayowafanya TAKUKURU kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja ya kushughulikia Kesi hizi.
Jambo jingine ni Uwezo katika kutekeleza majukumu yao, DPP na TAKUKURU, mara nyingi wamekuwa Wakishindwa katika Kesi kubwa kubwa,hususani za Rushwa. Uwezo katika Ukusanyaji wa Ushahidi limekuwa ni tatizo kubwa, na Mahakamani kwenye jinai ni Ushahidi usioacha shaka yoyote.
Yapo mengi ya kushughulikia katika Idara hizi mbili, ila kwa Uchache

1. Sheria zibadilishwe ili kuwaruhusu TAKUKURU ku prosecute cases zao bila kupitia Ofisi ya DPP. Kesi nyingi za Takukuru zimekwamia ofisini kwa DPP.
2. Wajengewe uwezo wa kutosha katika kushughulika na kesi za Ufisadi. UWEZO hapa namaanisha ni Mafunzo, Vitendea kazi vya Kisasa, na Uwezo wa Kifedha na ki hali. Unampeleka Wakili wa Serikali ku prosecute case ya Ufisadi wa mabilioni ya shilingi ilihali mshahara unamlipa Laki Nane? Yeye ni Robot au ni binadamu sawa na hao mafisadi?

3. Kiundwe chombo ndani ya TAKUKURU kushughulika na Grand Corruption. Kiwezeshwe kimfumo na kiufundi ili kukabiliana na Grand Corruptions.

4. FIU nayo Iboreshwe kuendana na maboresho ya DPP na TAKUKURU.

Yapo mengi,na mengine wadau watayaongezea.

Tusipofanya Marekebisho ya kutosha kwa vyombo tajwa hapo juu, hata tuwe na Mahakama za kila Jinai, ni kazi ya Kuweka Maji kwenye Gunia!
Tunahitaji mfumo imara na Madhubuti kwa hizi Idara/ Taasisi kuliko tunavyohitaji iitwayo Mahakama ya Mafisadi.

Siku Njema
 
sidhani pia hawa jamaa wa pccb mikoani na wilayani kama wanakitengo cha upelelezi, ni kitengo ambacho kingewasaidia sana kufanya kesi zao nyingi zisiharibike.
 
sidhani pia hawa jamaa wa pccb mikoani na wilayani kama wanakitengo cha upelelezi, ni kitengo ambacho kingewasaidia sana kufanya kesi zao nyingi zisiharibike.
Ni kweli kabisa mkuu! Maboresho yanahitajika sana kwa hizi Taasisi ili ziweze kutekeleza Wajibu wao.
 
Back
Top Bottom