Tunahitaji kufanya hili, ili kutunza hadhi ya Jamii Forums(JF). | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji kufanya hili, ili kutunza hadhi ya Jamii Forums(JF).

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msafiri Kasian, Aug 30, 2012.

 1. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,780
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Natumaini wote ni wazima,pole kwa wote wenye matatizo mbalimbali.
  Mara nyingi nimekuwa nikitafakari hatima ya JF bila kupata suluhisho hasa katika lugha inayotumiwa na baadhi ya wanaJF. Watu wanatumia vifupisho vya maneno,ambavyo kwa mtazamo wangu vinashusha hadhi ya JF. Hapa chini ni baadhi tu ya maneno ambayo watu wengi hupenda kutumia;
  >Kwasababu-Kwa7bu.
  >Mtu-M2.
  >Tusibibishane-2cbishane.
  >Siku-cku.
  >...................
  >...................
  >...................
  Haya ni baadhi tu!
  Kuna mengi zaidi,naamini hata nyie mmekutana nayo. Matumizi haya ya lugha hayajengi bali kuibomoa lugha. Kusema kweli,ukiingia Jukwaa la Elimu,mambo kama haya utayakuta kwa wingi zaidi,na kwa tafsiri yangu mimi,hizi ni lugha za kitoto zinazopaswa kutumiwa kule facebook,twitter na mitandao mingine ya kijamii(ambapo kuna makundi ya watu wanaolingana umri) lakini SIO humu JF penye vijana kwa wazee. Wito wangu kwenu ni kwamba,kila mtu ajitahidi kutumia lugha iliyokamilika,ili kuendelea kutunza hadhi ya JF pamoja na kuendeleza lugha.
   
 2. cheupe sr

  cheupe sr Senior Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa hizo ni childish languages na hapa JF hizi staili kutumika.
   
 3. javascript

  javascript Senior Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  co mbaya, ni mtazamo wako 2
   
 4. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,967
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja mia kwa mia. Tubadilike. VIVA JF.
   
 5. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,780
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mkuu naona hata hapa umetupia hivyohivyo,je,hii inamaanisha kwamba haujaunga mkono hoja?
   
Loading...