Tunahitaji akili ya juu zaidi kuweza kutatua matatizo ya nchi hii, walioko madarakani wamechoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji akili ya juu zaidi kuweza kutatua matatizo ya nchi hii, walioko madarakani wamechoka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, Jun 28, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali iliyoko madarakani imechoka kwa kila hali na zaidi uwezo wa kufikiri kwa sababu hawana mbinu mbadala za kutatua matatizo yanayo likabili taifa hili. Suala la madaktari wameona mbinu ni kukimbilia mahakamani na kuanza utekaji, mauaji na vitisho. Baadhi ya wabunge wameanza kulalamika kwa nini Bunge haliletewi ripoti ya kamati iliyoundwa kushughulikia suala hilo ili waisimamie serikali kwenye utekelezaji.

  Hivyo basi tunahitaji akili ya juu zaidi kuweza kutatua matatizo yetu. Watu walewale walio sababisha matatizo hawawezi kuyatatua kwa kutumia mbinu zilezile. Wananchi tulione hili, hakuna jambo ambalo ni zito na limetatiza umma na likatatuliwa kwa njia mbadala kila mtu akaridhika kutokana na kumbu kumbu zangu. Wana jamvi kama lipo basi mwenye nalo alilete hapa. Mfano ukianzia mafuriko, ufisadi, migomo na mengine mnaweza kuongezea.
   
Loading...