Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,640
- 729,672
Kizaramo wangesema kiherehere cha nini ila mimi binafsi siwezi kufanya hivyo.....
Hapa kuna mambo yanatokea ambayo yatakuja kuwa tatizo kubwa huko mbeleni, kama si mtanziko wa miradi kukwama basi itakuwa zigo zito la madeni yasiholipika huku miradi mingi ikiwa na mushkeli na kasoro za wazi.
Hata kama hatushauriki lakini kufanya kazi kimfumo na kitaaluma kunaweza kuliokoa Taifa kutoka kwenye tope la hasara kubwa na miradi iliyo chini ya kiwango.
Tayari DAR pekee tuna miradi itakayogharimu trilioni za shilingi.
Je hii pesa tunayo? Kama hatuna tutaipata wapi? Je tutapata kama msaada ama mkopo?
Masharti yake yanasemaje? Bunge lina taarifa hizi? Timu za wataalamu wa fedha uchumi na miundombinu nk wanasemaje? Je kuna ushirikishwaji wa wazi na wa kizalendo?
Mikataba kuanzia upembuzi yakinifu mpaka kukamilika kwa miradi ukoje? Bunge inaifahamu? Iko kwenye dira ya maendeleo na vipaumbele vyetu?
Miradi ya barabara za juu na mzunguko kwenye makutano ya Tazara na Ubungo
Highway ya Chalinze Dar
Miradi ya treni za umeme na kawaida
Mradi wa barabara daraja kupitia ufuko wa Coco beach nk nk nk.
Mambo yasiwe mengi kiasi hiki kwa wakati mmoja, tunahangaika na DAR as if hatuhami na tunaandaa makao makuu ya nchi.
Ilishajulikana wazi kuwa kipaumbele ni kuhamia Dodoma na baadhi ya wizara na watendaji wameshahamia huko japo hakuna ofisi wala miundombinu ya kutosha. Ghafla ile speed imepungua na sasa ni DAR tena.... what a confusion!
Tutoe kipaumbele kimoja basi, ili tujue tunashika lipi ili tusije tukaharibu kote, tukapigwa na kuumizwa tena kama ilivyotokea kwenye ile meli ya uvuvi Au ile Mv Dar es Salaam Au zile terrible teens!!! Nk nk
Kwanini hatukujifunza? Tulikatae hili pepo la uharibifu lisijenge madhabahu yake hapa, tukiliachia litaharibu bila kutengeneza na hata likitengeneza kasoro zitakuwa nyingi kwakuwa haliwezi kutenda kwa ukamilifu kutokana na roho yake ya uharibifu