Mjema Vushanje
Senior Member
- Sep 24, 2017
- 159
- 353
Askari wa Tanzania waliouawa DRC na majeruhi waongezeka.
Idadi ya walinda amani wa Tanzania waliouawa kwenye jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeongezeka na kufikia 15 na majeruhi ni 53. Awali idadi ilikuwa vifo 12 na majeruhi zaidi ya 40.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji hayo dhidi ya walinda amani hao waliokuwa katika kikosi cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO.
Katika tamko lao lililosomwa na Japan ambayo inasimamia Baraza hilo kwa mwezi wa Disemba, wajumbe wameeleza masikitiko yao kufuatia vifo hivyo, wakisema mashambulio hayo ni uchochezi dhidi ya walinda amani.
(Pichani: Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiwa kikaoni).
[HASHTAG]#HabarizaUN[/HASHTAG] [HASHTAG]#Majonzi[/HASHTAG] [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] [HASHTAG]#DRC[/HASHTAG] [HASHTAG]#UNNewskiswahili[/HASHTAG] [HASHTAG]#MONUSCO[/HASHTAG]