Tunafaidika vipi kule DRC?

Mjema Vushanje

Senior Member
Sep 24, 2017
159
500
Askari wa Tanzania waliouawa DRC na majeruhi waongezeka.

Idadi ya walinda amani wa Tanzania waliouawa kwenye jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeongezeka na kufikia 15 na majeruhi ni 53. Awali idadi ilikuwa vifo 12 na majeruhi zaidi ya 40.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji hayo dhidi ya walinda amani hao waliokuwa katika kikosi cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO.

Katika tamko lao lililosomwa na Japan ambayo inasimamia Baraza hilo kwa mwezi wa Disemba, wajumbe wameeleza masikitiko yao kufuatia vifo hivyo, wakisema mashambulio hayo ni uchochezi dhidi ya walinda amani.

(Pichani: Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiwa kikaoni).

[HASHTAG]#HabarizaUN[/HASHTAG] [HASHTAG]#Majonzi[/HASHTAG] [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] [HASHTAG]#DRC[/HASHTAG] [HASHTAG]#UNNewskiswahili[/HASHTAG] [HASHTAG]#MONUSCO[/HASHTAG]
 
kikuna

JF-Expert Member
May 26, 2015
2,212
2,000
Hv unavamiage kambi na kuua askar 12 na mageruh kadhaa hv woote ni wa Tanzania??!...wanajeshi wanatakiwa kuwa tayar kwa lolote sasa wao walikaa tu au hawana bunduk ....au training mbovu...kuna maswal ya kujiuliza ....na kuhoji...by da way mungu ibarik tz....na tukalipe kisasi kwa waliofanya huu unyama
 
kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,355
2,000
Kuna kipindi iliripotiwa dada yake Kagame hapa Dar anashirikiana biashara ya madini na mke wa kibopa!!!!

Ila umenikumbusha ile enzi za Kikwete na Membe ambapo jeshi letu lilishiriki kwenye vita kule Comoro kumtoa major Bakary sijui na ndio tuliongoza vita!!

Vijana wa kaifanyie kazi kwa ufanisi,iila ikasemekana fungu kubwa likatolewa kama shukrani halfu aliyekuwa waziri wa protocol akafanya yake na wachache bila ya vijana wa jeshi kufidiwa jasho lao!!
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,972
2,000
Hv unavamiage kambi na kuua askar 12 na mageruh kadhaa hv woote ni wa Tanzania??!...wanajeshi wanatakiwa kuwa tayar kwa lolote sasa wao walikaa tu au hawana bunduk ....au training mbovu...kuna maswal ya kujiuliza ....na kuhoji...by da way mungu ibarik tz....na tukalipe kisasi kwa waliofanya huu unyama
Walifanyiwa ambush
 
LAMBOFGOD

JF-Expert Member
Aug 12, 2016
1,536
2,000
hizi mishe za congo wajeda achaneni nazo na pia ndoto za kusema nikirudi nakuwa million kadhaa, tunza mshahara wako na uupangilie
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
13,631
2,000
Askari wa Tanzania waliouawa DRC na majeruhi waongezeka.

Idadi ya walinda amani wa Tanzania waliouawa kwenye jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeongezeka na kufikia 15 na majeruhi ni 53. Awali idadi ilikuwa vifo 12 na majeruhi zaidi ya 40.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji hayo dhidi ya walinda amani hao waliokuwa katika kikosi cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO.

Katika tamko lao lililosomwa na Japan ambayo inasimamia Baraza hilo kwa mwezi wa Disemba, wajumbe wameeleza masikitiko yao kufuatia vifo hivyo, wakisema mashambulio hayo ni uchochezi dhidi ya walinda amani.

(Pichani: Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiwa kikaoni).

[HASHTAG]#HabarizaUN[/HASHTAG] [HASHTAG]#Majonzi[/HASHTAG] [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] [HASHTAG]#DRC[/HASHTAG] [HASHTAG]#UNNewskiswahili[/HASHTAG] [HASHTAG]#MONUSCO[/HASHTAG]
Hata mimi hua najiuliza kama nchi tunafaidikaje?!
Ninapokumbuka Mozambique, Ushelisheli, Uganda, Rhodesia, South Africa , Dafur Sudan, Comoro na sasa Zaire. Koote huko tumepoteza raslimali watu, uchumi na muda. Najiuliza nini faida kama taifa tunapata huko??!!
 
Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
924
1,000
Nimepokea taarifa za kuuawa kwa walinda amani wetu huko DR Congo kwa mshituko, masikitiko na maumivu makubwa sana kama mtanzania mzalendo, sasa sijui kwa ndugu jamaa na marafiki wa wafiwa watakua katika hali gani, pole nyingi ziwafikie.

Hali ni mbaya, tunapoteza watu muhimu katika taifa hili, hivi tunapata faida gani kupeleka majeshi yetu Darful sudan na huko Congo?
Mbona hatupeleki Somalia na bado tuko shwari kabisa hakuna tunalopungukiwa?
Hivi ni lazima nchi zote Afrika zichangie wanajeshi wake huko Congo na Sudani?

Ni wakati sasa, Rais tunaomba uwarejeshe askari wetu nyumbani waendelee kulinda mipaka ya nchi na majukumu yao mengine ya kila siku.

Nawasilisha
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,370
2,000
kwenye nchi inayofuata katiba na yenye bunge imara hili sio swala la rais
ni swala la wabunge kupitisha azimio na mchezo unaisha
tatizo bunge la tanzania limejaa wachumia tumbo kama ndugai
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
10,083
2,000
hizi mishe za congo wajeda achaneni nazo na pia ndoto za kusema nikirudi nakuwa million kadhaa, tunza mshahara wako na uupangilie
Tatizo ni kwamba wanajeshi wapiganaji hawana uamuzi wa kukataa amri. Mtoa amri ndo anayeweza kuondoa vikosi vyake ila Mataifa yanayonufaika na hizi vita yanatoa hela kwa mataifa ili yakapigane. Wao wanatoa pesa sisi tunatoa uhai.
 
hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
575
500
Hv unavamiage kambi na kuua askar 12 na mageruh kadhaa hv woote ni wa Tanzania??!...wanajeshi wanatakiwa kuwa tayar kwa lolote sasa wao walikaa tu au hawana bunduk ....au training mbovu...kuna maswal ya kujiuliza ....na kuhoji...by da way mungu ibarik tz....na tukalipe kisasi kwa waliofanya huu unyama
Hukosi mojawapo/yote katika haya

hujui lolote kuhusu kifo
hujui lolote kuhusu jeshi
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
6,213
2,000
rudisheni askari wetu walinde mipaka yetu
Ni makubaliano ya kimataifa .Wanalinda Amani Nadhana kuna kupata uzoefu pia kuna Haja ya kuweka nguvu Za ziada hilo ndilo la Msingi Askari 12 Ni wengi sana hata km Angelikuwa ni 1 Mungu Awa Rehemu
 
KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,530
2,000
Hv unavamiage kambi na kuua askar 12 na mageruh kadhaa hv woote ni wa Tanzania??!...wanajeshi wanatakiwa kuwa tayar kwa lolote sasa wao walikaa tu au hawana bunduk ....au training mbovu...kuna maswal ya kujiuliza ....na kuhoji...by da way mungu ibarik tz....na tukalipe kisasi kwa waliofanya huu unyama
Kuna mbinu inaitwa "ambush". Hutumika kumvamia adui akiwa hana uwezo wa kujibu mapigo. Hicho kitendo hufanyika haraka sana na kwa muda mfupi.
 
SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,974
2,000
Ukishaenda kulinda Amani sehemu zisizo na amani, lolote laweza kutokea mkuu.

Vita ni vita tu. Vita ni timing na kuviziana tu. Anayemuwahi mwenzio ndiye mshindi.

Askari wetu kwenda kulinda Amani DRC ni moja ya mchango wetu kwa bara letu la Afrika.

R.I.p. Askari wetu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom