Tunaelekea wapi?: PhD holders kuwa wanasiasa, na Re-Advertized jobs kwa walimu wa vyuo vikuu

Tatizo hili linaweza kuwa limechagizwa na nature ya watanzania tulivyo, na hata walioweka vigezo hivyo waliweka ufaulu huo mkubwa wa gpa ya 3.8 sababu watu wengi kama si wote wataofika ktika gpa hiyo ni watu wenye juhudi,uwezo na mapenzi na elimu na kiuhalisia ni watu wachache sana wa calibre hiyo

Na sisi kama watanzania wengi elimu imepita kombo, mapenzi na elimu hamna maana kuscore chini ya average ya B+ elimu ya chuo mtu kashindwa kuwa na spirit ya elimu. Elimu ya chuo ni rahisi maana mwalimu ndio pia necta huyo huyo isitoshe vitabu na mazingira ya kusomea ni bora kabisa sasa tatizo linabaki kwa vijana wenyewe, kusoma ni mpaka asukumwe na mitihani na si mapenzi natural ya kile anachokisomea. Na kazi ya uhadhiri ni kazi ya watu wenye mapenzi na kitabu na sio watu waliolazimishwa.

Nahitimisha kwa kusema kuwa watu ambao ni academic material ni watu pekeehivyo jamii na viongozi walitambue hilo na pia inabidi kuwe na recruitment policy sababu licha ya kuhitajika vyuoni pia wahadhiri hao hao wanahitajika katika nafasi potential za kiuongozi katika nchi.
 
mada nzuri sana, ingawa inaitaji utafiti ili kuja na taarifa sahihi kuhusu hali ya ajira za wahadhiri katika vyuo vikuu nchini Tanzania. Labda hapa tunaweza kuibua maswali yanayoweza kuwa muongozo wa utafiti, lakini kuchangia naishia hapa "no research no right to speak"
Ni bora wewe umejaribu ku digest! Kuna watu wanatoa majibu mpaka unajiuliza, hivi watu wengine huwa wanafikiria kwa ile masaburi style?
 
hili linaweza kuwa limechagizwa na nature ya watanzania tulivyo, na hata walioweka vigezo hivyo waliweka ufaulu huo mkubwa wa gpa ya 3.8 sababu watu wengi kama si wote wataofika ktika gpa hiyo ni watu wenye juhudi,uwezo na mapenzi na elimu na kiuhalisia ni watu wachache sana wa calibre hiyo
Point nzuri sana! Ni kweli ni idadi ndogo itakayofikia calibre hiyo hawa kizazi cha sasa! Sasa tufanyeje mkuu
 
Hii ni mada nzuri sana, ingawa inaitaji utafiti ili kuja na taarifa sahihi kuhusu hali ya ajira za wahadhiri katika vyuo vikuu nchini Tanzania. Labda hapa tunaweza kuibua maswali yanayoweza kuwa muongozo wa utafiti, lakini kuchangia naishia hapa "no research no right to speak".
Je, ni kweli kumekuwa na re-advertisement ya ajira za Wahadhiri? Kama ndiyo, kwa nini? Je, vigezo vya GPA bado ni vigezo sahihi kwa wakati huu tulionao? Mkuu tusaidie kwa hili. Natumai wewe ni Muhadhiri bila shaka
 
Kama unaweza kuwa na Ph.D msema ovyo kama Magufuli, au mtu asiyejali integrity anayeweza kupinga ma Ph.D kuteuliwa nafasi za kisiasa kwa sababu kufanya hivyo kunawanyima wanavyuo walimu na watafiti kama alivyofanya Dr. Kitila Mkumbo, halafu ukakubali uteuzi wa kisiasakama alivyofanya Dr. Kitila Mkumbo, swali halisi hapa linageuka.

Swali linageuka linakuwa si tu kwamba kwa nini Ph.D holders wanakuwa wanasiasa na jinsi hili jambo linavyoweza kuathiri maendeleo ya elimu na utafiti, swali linakuwa, hizi Ph.D zetu kweli zina maana yoyote zaidi ya kuwa makaratasi yenye sifa kubwa ambazo katika utekelezaji hazina maana?

Hilo, kwangu mimi, ndilo swali halisi.
 
linageuka linakuwa si tu kwamba kwa nini Ph.D holders wanakuwa wanasiasa na jinsi hili jambo linavyoweza kuathiri maendeleo ya elimuna utafiti, swali linakuwa,hizi Ph.D zetu kweli zina maana yoyote zaidi ya kuwa makaratasi yenye sifa kubwa ambazo katika utekelezaji hazina maana?
Nimefurahi sana kurejea kitila mkumbo! Maana alicomment vyuoni wanaisha walimu, pia akateuliwa na akukubali. Narudia sema, njaa haikuwahi kumuacha MTU salama
 
Je, ni kweli kumekuwa na re-advertisement ya ajira za Wahadhiri? Kama ndiyo, kwa nini? Je, vigezo vya GPA bado ni vigezo sahihi kwa wakati huu tulionao? Mkuu tusaidie kwa hili. Natumai wewe ni Muhadhiri bila shaka
Kimsingi hatuna majibu sahihi (hili jambo linahitaji utafiti) na mada yenyewe inazaa maswali mengi kuliko majibu. Mimi sijaona hizo re-advertisement nyingi zinazosemwa (walau kwa matangazo kupitia magazeti) bali ninachojua vyuo vikitangaza nafasi za ajira za wahadhiri vinapokea maombi mengi kuliko nafasi zilizopo hasa kwa ngazi za bachelors na masters (ingawa si kwa fani zote). GPA kimsingi inasaidia kutafuta wastani wa ufaulu, kwahiyo tukiita GPA au jina lingine lolote haiondoi umuhimu wa kuwa na wastani wa kiwango cha ufaulu ambacho ni kigezo cha kuwapima watahiniwa. Naendelea kisitiza hii mada ni nzuri, muhimu na pana sana inahitaji utafiti wa kina ili kujibu maswali na kukidhi haja.
 
Nimefurahi sana kurejea kitila mkumbo! Maana alicomment vyuoni wanaisha walimu, pia akateuliwa na akukubali. Narudia sema, njaa haikuwahi kumuacha MTU salama
Mimi siamini kama ni njaa, kwakweli hata kama Tanzania ni nchi ya DUNIA YA TATU huwezi kuniambia Profesa ana njaa kama mtanzania wa kawaida kiasi kwamba maamuzi yake yanaongozwa na njaa, la hasha. Tatizo ni uelewa tu na misimamo yetu ya kisiasa ndio inatupelekea kuona hivyo. Kiukweli hata wewe ukiitajika kutumikia nafasi ya juu katika nchi yako hutakataa, swaala linakuja wakitoka wote wanafunzi watafundishwa na nani? Hili swali nalo bado linazaa maswali, ebu tujiulize kabla hatujalaumu,
Je ni wahadhiri wa fani zipi hasa wamejiunga na siasa au kuteuliwa katika nyazifa mbalimbali serikalini?
Je kujiunga kwa na siasa au kuteuliwa kumeacha pengo kiasi gani?
Je kuna uwezekano wa pengo hilo kuzibwa kwa muda mfupi kiasi gani?
Je kwa kiasi gani kuondoka kwao kumeathiri masomo na naendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi na vyuo husika?

Haya ni sehemu tu ya maswali yanayoitaji majibu yanayotokana na utafiti, hapa tunakisia tu kitu ambacho sio sahihi kitaalamu.
 
. Kiukweli hata wewe ukiitajika kutumikia nafasi ya juu katika nchi yako hutakataa, swaala linakuja wakitoka wote wanafunzi watafundishwa na nani? Hili swali nalo bado linazaa maswali, ebu tujiulize kabla hatujalaumu,
Je ni wahadhiri wa fani zipi hasa wamejiunga na siasa au kuteuliwa katika nyazifa mbalimbali serikalini?
Je kujiunga kwa na siasa au kuteuliwa kumeacha pengo kiasi gani?
Je kuna uwezekano wa pengo hilo kuzibwa kwa muda mfupi kiasi gani?
Je kwa kiasi gani kuondoka kwao kumeathiri masomo na naendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi na vyuo husika
Mkuu omba fund ufanye utafiti huu. Naamini uko chuoni huko.
 
Kama unaweza kuwa na Ph.D msema ovyo kama Magufuli, au mtu asiyejali integrity anayeweza kupinga ma Ph.D kuteuliwa nafasi za kisiasa kwa sababu kufanya hivyo kunawanyima wanavyuo walimu na watafiti kama alivyofanya Dr. Kitila Mkumbo, swali halisi hapa linageuka.

Swali linageuka linakuwa si tu kwamba kwa nini Ph.D holders wanakuwa wanasiasa na jinsi hili jambo linavyoweza kuathiri maendeleo ya elimu na utafiti, swali linakuwa, hizi Ph.D zetu kweli zina maana yoyote zaidi ya kuwa makaratasi yenye sifa kubwa ambazo katika utekelezaji hazina maana?

Hilo, kwangu mimi, ndilo swali halisi.
Kazi ya prof ni Ku lecture sasa Huyu suka anawajaza na kuwapa nyadhifa mbalimbali..
Prof na uongozi wapi na wapi.....
Ma prof wetu washazoea wakitoka kufundisha kazi Yao ya ziada ni kufuga ngombe na kuuza maziwa

Ova
 
Kazi ya prof ni Ku lecture sasa Huyu suka anawajaza na kuwapa nyadhifa mbalimbali..
Prof na uongozi wapi na wapi.....
Ma prof wetu washazoea wakitoka kufundisha kazi Yao ya ziada ni kufuga ngombe na kuuza maziwa

Ova
Jamaa anapenda sana majibu mepesi kwa maswali magumu.

Tatizo la uongozi Tanzania ni nini? Viongozi hawana elimu.

Ufumbuzi ni nini? Jaza Ph.D katika uongozi. Uhakikiusio namwishohata kwa wafagizi.


Ph.D hata ya American Civil War sasa hivi inakutoa bongo.
 
Nakumbuka katika chuo nilichosoma katika department yetu walitoa maprofesa wawili ambao sizani kama leo au kesho pengo lao litazibwa!!
 
pole sana kwa kuumiza kichwa kwa manufaa ya taifa hili, mimi hili jambo limekuwa likinisumbua sana, watanzania ajira hatuna au tunawapa wenzetu wa mataifa mengine kwa kisingizio cha GPA, hii issue ya GPA ilishawahi kuzungumzwa sana hapa jamvini lakini mpaka leo sijawahi kuridhika. Kwanza nikiri kabisa GPA ni njia mojawapo ya kumfahamu au kumpata mhandhiri mzuri kwa maana ana anaelewa walau kile anachotakiwa kuwapa wanafunzi wake! Je hizi GPA zina uwiano sawa katika taasisi zetu za elimu ya juu? hapa naamanisha mwanachuo aliyehitimu UDSM, IFM, MUHAS, SUA , MZUMBE nk GPA zao zina uzito sawa? Je wahadhiri wa nje tunao waajiri na kuacha vijana wetu tuna husika au tuna uhakika na mfumo wao wa elimu hapa na maanisha tumejidhihirisha na upatikanaji wa GPA zao?.Kama jibu ni sawa basi ni vyema. TATIZO HAPA UPATIKANAJI WA GPA HIZI UNATOFAUTIANA BAINA YA CHUO NA CHUO.
unaweza kuwa na GPA nzuri lkn uwezo wa chini kwa maana ya master of content. pia naunga mkono kuwa GPA ni mwanzo wa kutambua mwenye uwezo hata hivyo zimetofautiana katika vyuo kwani masomo/kozi tofauti, content tofauti, mazingira tofauti, walimu/lecturers ni tofauti kwa hiyo ulinganisho unaweza kuwa tofauti na wengine kufaidika au kukosa fursa na mfumo wa GPA.
 
Wandugu kwema na misukosuko ya maisha kwa hapa na pale.

Kwa muda sasa kila nikisoma post za ajira za Tanzania, hasa upande wa vyuo vikuu naona matangazo yanakuwa "re-advertized" kwa maana ya kwamba hawakupata watanzania wenye sifa kupata nafasi hizo.

Sasa najiuliza, hivi hawa watoto wetu walioko vyuoni watafundishwa na akina nani wakati nafasi za ajira zikitangazwa hazipati walimu?

Pia najiuliza, au kurudiwa kwa kazi hizi ni kukosa sifa za nafasi hizo? Au kwa kuwa TCU wameendelea kukumbatia zile traditional means of recruitments(GPA za undergraduate 3.5, na Masters, 4.0)!

Je, hizo kazi zikiendelea kuwa re-advertized nini kifanyike? Maana wasomi wetu hawa wa PhD wanateuliwa nafasi za siasa na utendaji serikalini..!

TCU mnaweza kubadili vigezo ili wanafunzi wa vyuo vikuu wapate walimu?
Au kazi hizi zinakuwa re-advertized kwa kuwa wengi wanaona kuwa m taaluma ni njaa hivyo hailipi.

Tufanyeje sasa wandugu!
Nawasilisha.
Tcu kazen hivyi hivyo maana hatuwez kuajir walimu wasio na qualification kisa kuna uhaba wa wenye sifa.Kuliko hivyo ajiri kutoka nchi nyingine,.. Tuache kushusha elimu yetu
 
unaweza kuwa na GPA nzuri lkn uwezo wa chini kwa maana ya master of content. pia naunga mkono kuwa GPA ni mwanzo wa kutambua mwenye uwezo hata hivyo zimetofautiana katika vyuo kwani masomo/kozi tofauti, content tofauti, mazingira tofauti, walimu/lecturers ni tofauti kwa hiyo ulinganisho unaweza kuwa tofauti na wengine kufaidika au kukosa fursa na mfumo wa GPA.
mbaya zaidi hata upatikanaji wa GPA husika vigezo ni tofauti sana lakini wakati wa kuajiri kigezo kinakuwa sawa mfano UDSM ukipata 70-100 ni A (GPA-5), 60-69 ni B+ (GPA-4), 50-59 ni B (GPA 3), 40-49 ni C (GPA -2), SUA ni tofauti 70-100 ni A (gpa -4.4-5) , 65-69 ni B+(GPA 4-4.3), 60-64 ni B (GPA -3-3.9), 50-59 ni C (2.1-2.9), 40-49 ni D (GPA -1-1.9), HII NI SANA NA KUCHANGANYA MAHARAGE NA KARANGA! SIJUI TCU WANAREGULATE KITU GANI
 
Back
Top Bottom